Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Kuna taarifa nimekutana nazo mahali kuwa ingawa ITV na AZAM wali-confirm jana kuwa watarusha LIVE (Mubashara) Press Conference ya Chadema leo hii wametoa sababu kuwa hawataweza kufanya hivyo kama walivyokuwa wameahidi, ITV kwa upande wao wamedai mitambo yao ina matatizo kidogo kwahio hawataweza wakati AZAM wamesema wamepeleka mitambo yao Zanzibar (huenda kuna shughuli nyingine).
Bas tunaendelea kushukuru kwa kila figisufigisu! Tunachukulia majibu hayo positively kama ni kweli au ni uongo! Huenda kesho na baadhi ya magazeti yasiripoti kabisa, tusishangae.
Au CCM wanaogopa ile taarifa ya siri kuwa Makada wao wengi watakikimbia Chuma Chakavu kwenye Press hii??
Bas tunaendelea kushukuru kwa kila figisufigisu! Tunachukulia majibu hayo positively kama ni kweli au ni uongo! Huenda kesho na baadhi ya magazeti yasiripoti kabisa, tusishangae.
Au CCM wanaogopa ile taarifa ya siri kuwa Makada wao wengi watakikimbia Chuma Chakavu kwenye Press hii??
TAARIFA KUHUSU PRESS CONFERENCE YA CHADEMA KUWA LIVE..
Binafsi nimeongea na mkuu wa Idara ya ya Habari na Mawasiliano CHADEMA Kamanda Tumaini Makene.
Ameniambia kwamba mpaka jana Saa 5usiku walikubaliana na CHANNEL TATU ZA TALEVISHENI kuonesha Mkutano wa CHADEMA na waandishi wa habari moja kwa Moja (LIVE) ikiwa ni pamoja na ITV NA AZAM.
Leo asubuhi ameambiwa na ITV kwamba hawataweza kurusha live Mkutano huo kwa sababu za kiufundi ambazo ziko juu ya uwezo wao......
AZAM TV nao wametoa taarifa kwamba hawataweza kurusha Mkutano huo Live kwa sababu vyombo vyao vimepelekwa Zanzibar ingawa jana walikubaliana na CHADEMA kurusha Mkutano Huo LIVE....
"Kutokana na hayo, imeshindikana kurusha Mkutano huo Live na kwa hiyo Chadema tutarekodi Mkutano huo na kurusha kipindi usiku au Jioni......... "Amemalizia Makene.
Binafsi nimesikitika Sana........
Daniel Ezekiel Daniel