Principle of Causality

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
28,481
Reaction score
28,749
Habari ya usiku wakubwa. Leo nimejikuta nipo katika mood ya kuwasilisha mada ya yenye kichwa hicho hapo juu.

Je ni kweli kwamba nadharia hiyo ndio sababu au miongoni mwa sababu ya wanasayansi kuupinga uwepo wa Mola muumba kwa maana ya kuwa yeye ndio chanzo wa kila kilichopo hapa duniani ?

Lakini je ni kwelo au kuna haja ya yule wa mwanzo muhimili kuwa na chanzo ?

Leo nataka tujikite kwenye hii nadharia na kuleta hoja zenye nguvu na kielimu.

Leo nataka tuiweke kando au tuitupilie mbali ile imani ya wakana Mungu kwa kukataa kwao uwepo wa Mola mlezi kisa kuna mabalalaa na dhiki hapa duniani na mfano wake.

Sababu nadharia hii ni maarufu sana,hapa sina haja ya kuiarifisha nadharia hiyo.

Nipo ....
!
 
Hapa nilitarajia ungeielezea japo kidogo hiyo principle kisha ndio tuanze kujadili. Sidhani kama kila mtu anaelewa unaongelea kitu gani. Next time ukiwa unaanzisha mada, nakushauri uzingatie hilo.

Kwa ufupi, Principle of Casuality ni Kanuni inayoelezea uhusiano uliopo kati ya SABABU na MATOKEO (Cause and Effect). Hii ni miongoni mwa nadharia zinazotumika kuelezea mambo mbalimbali yanayoendelea duniani.

Kanuni hii inaaminisha kwamba kila jambo lina sababu yake. Kwamba, kila matokeo ya jambo fulani, nyuma yake yana kisababishi. Yaani hakuna jambo linalolotokea hivi hivi tu. Na kimsingi ni kanuni inayofuatwa sana kwenye imani za Ubudha (kupitia Karma), kwenye kupata takwimu na hata huko kwenye taaluma ya Uhandisi wa kudhibiti ubora wa vitu.

Kwa watu wa dini, kanuni hii ndiyo imeleta nadharia ya uumbaji. Kwamba hapo Mwanzo dunia iliumbwaje, binadamu alitokea wapi, mwanamke alitokea wapi, shetani alitokea wapi, dhambi zilianzia wapi na kadhalika.

Nadhani nimesaidia kwa kiasi fulani kujenga msingi wa thread yako mkuu wangu Zurri
 
Nahisi mmeongelea vitu viwili tofauti, CAUSALITY AND CASUALITY kama sio makosa ya tahajia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…