Private car: Je ni salama kusafiri mwenyewe up country

Mimi natoka Igunga via pori la ibembampazi,chunya to mbeya na Land Rover 109(mwarobaini)
Wewe kwenda hapo tu Arusha unajuiliza uliza hivi?tena rav4 model 2004.halaf unakaujuzi kaufundi hata ukipata Pancha unajua kupiga jeki na barabara lami tupu
Mkuu piga machine usiwe MTT wa mama gari ya Mgumu hairudi nyuma
Punda Afe lkn Mzigo,,,,,,,
 
Duuhh...anaenda kibiti au
 
Mkuu, huyu bwana kwani anaenda vitani?? πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kuna chalii ni fundi magari anatokaga Dar-Arusha kwenye saa 10 alfajiri...
By saa 3 asubuhi yupo Arusha mjini.. Muhimu uwe makini tu barabarani, jamaa anatembeza noah speed 140 hapo ndio wastan wake akipata mnyooko anakandamiza 160km/h
Kwa barabara ZA TANZANIA NA SPEED HIYO UNATAFUTA KABURI
 
Endesha asubuhi mpaka jioni. Malori yaliyoharibika huegeshwa kiholela barabarani bila tahadhari yoyote kwa watumia barabara wengine.
 

Are you real asking this Question? AU UNATAKA KUTUAMBIA UMENUNUA RAV 4?
 
EN
Kuna chalii ni fundi magari anatokaga Dar-Arusha kwenye saa 10 alfajiri...
By saa 3 asubuhi yupo Arusha mjini.. Muhimu uwe makini tu barabarani, jamaa anatembeza noah speed 140 hapo ndio wastan wake akipata mnyooko anakandamiza 160km/h
Enzi za ujana wangu nilikua natemba 180KM/H nikiwa na SUBARU, nashukuru MUNGU leo hii bado ni mzima
 
Kwa wastani kila baada ya masaa manne Magogo huwekwa njiani .na watu wasiojulikana na kila baada ya masaa 2 tochi za za yangeyange beware of road!
 
Siku moja nilikuwa natoka Dar kwenda mkoani, kufika maeneo ya Mbezi nikajikuta nimeshasinzia na kuanza kuota ndoto nzuuri! Kuja kushtuka nakumbuka kuwa naendesha gari! Ikabidi nipaki pembeni fasta nikalala kidogo. Nahisi kwa muda ambao nilikuwa nimelala, malaika wa Bwana alishika usukani maana isingekuwa hivyo, ningeshajikuta mtaroni!
 
Kitu muhimu kabisa ndg ni kujua uimara wako upo wapi na udhaifu wako upo wapi kuhusu mwili wako, kwa mfano kama unajijua kabisa usingizi wakati wa usiku huwa ni shida kuuzuia kwa hali yoyote ile, basi avoid kusafiri usiku na piga mashine mchana. Kutembe mwenyewe si shida, ila kama unauwezo wa kuwa na company ni bora na salama zaidi. Mengine uliyo andika ya usalama na ubora wa gari, pamoja na kuzingatia sheria na alama za barabarani ni lazima kwa safari salama.
 
Pia usisahau kuoverspeed wale jamaa wa tochi hujificha kwenye vichaka.
 
Kama hakuna anayekufuatilia nyuma na Toyota Land Cruiser nyeupe au Premio ni salama kabisa kusafiria mwenyewe kwenda huko mashinani / upcountry / mikoani Mkuu.

Haa haaπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ haa....

Sasa wewe wataka kumfanya mwenzio akaanze kupata tiba ya kisaikolojia India kwa mshtuko na woga... !!
 
Ukipatwa na majanga ndio utajua nlioandika hapo kina umuhim gani

Uko sahihi sana mkuu...

Mimi kisu ninacho na natafuta kibali cha kumiliki mkuu wa kuku ama SMG kabisa na itakuwa chini ya siti...

Siko tayari kufanywa kama alivyotendwa Tundu Lissu....

Laiti jamaa angekuwa na hii kitu, angepata nafasi na yeye pengine angeweza kumlaza chini hata mmoja wa majahiri hayo..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…