kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Private sector inajiendesha bila kutumia kodi wala kupata ruzuku, ukifilisika umefilisika ndio maana hata wasomi wetu wengi hawapendi kujiajiri wenyewe wako tayari waajiriwe hata kwa ujira mdogo kabisa.
Ingini kubwa ya private sector duniani kote ni kuwa holela, njia za mkato, ukwepaji kodi, utoaji ajira zisizo na uhakika sana na kutengeneza faida kubwa ya chapuchapu ukilinganisha na public sector.
Mitaji kwenye private sector inatokana na ama kukwepa kodi au kupunja wafanyakazi. ndiyo maana hata makampuni ya wakoloni yalikusanja mitaji kwa njia haramu, kama vile kufanyisha kazi watumwa, kufanyisha kazi watu masaa mengi hata watoto, kupora ardhi, kukodisha ardhi, kuiba madini na maliasili nyingine.
Duniani kote watu wengi huwa hawapendi ajira za private sector kwakuwa security yake ni ndogo sana. Kudumu kwenye ajira za private sector kutategemea na uhodari, uchapakazi na uwaminifu wa mfanyakazi. Mfanyakazi anapokosea (mwizi, mvivu, utoro, afya mgogoro, majungu) kwenye private sector kufukuzwa kwake ni jambo la haraka lisilohitaji vikao vingi.
Faida ya serikali kwa private sector isitokane na kodi kubwa kwa wawekezaji bali itokane na
1. Ajira watakazopewa wananchi wake
2. Masoko kwa bidhaa za wananchi zitakazotumiwa na uwekezaji na wawekezaji
3. Kodi kwa wafanyabiashara wa bidhaa za wawekezaji.
4. Huduma kwa wananchi kutoka kwa wawekezaji.
Serikali ilee wawekezaji badala ya kuwatisha kwa matamko ya siku saba na kuwafungia wanapopatikana na kasoro ndogondogo.