Private sector lazima iwe holela kidogo

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Private sector inajiendesha bila kutumia kodi wala kupata ruzuku. Ingini kubwa ya private sector ni kuwa holela, njia za mkato, ukwepaji kodi, utoaji ajira zisizo na uhakika sana na kutengeneza faida kubwa ya chapuchapu.

Mitaji kwenye private sector inatokana na ama kukwepa kodi au kupunja wafanyakazi. Hii ndiyo maana hata makampuni ya wakoloni yalikusanja mitaji kwa njia haramu kama vile kufanyisha kazi watumwa, kufanyisha kazi watu masaa mengi hata watoto, kupora ardhi, kukodisha ardhi, kuiba madini na maliasili nyingine.

Duniani kote watu wengi huwa hawapendi ajira za private sector kwakuwa security yake ni ndogo sana. Kudumu kwenye ajira za private sector kunategemea na uhodari, uchapakazi na uwaminifu wa mfanyakazi. Mfanyakazi anapokosea (mwizi, mvivu, utoro, afya mgogoro, majungu) kwenye private sector kufukuzwa kwake ni jambo rahisi na la haraka lisilohitaji vikao vingi. Na hiyo ndiyo ingini kubwa ya private sector, hakuna uzembe wala utu bali uzalishaji wenye tija.

Faida ambayo serikakali inatakiwa kupata kutoka private sector ni:

1. Ajira za wananchi wake zinazotolewa na private
2. PAYE (kodi ya mapato) kutoka kwa waajiriwa
3. Kodi ya VAT kwa wafanyakazi wanaponunua bidhaa/huduma
4. Kodi kwa wafanyabiashara wa bidhaa kutoka private sector
5. Huduma kwa wananchi wake kama shule, hospitali, mgahawa, barabara, usafiri zinazotolewa na private sector
6. masoko ya bidhaa/mazao ya wananchi

Hivyo serikali haipaswi kuingilia saana utendaji na utaratibu wa private sector ili ufanane na ule wa ajira za serikali. Vijana wetu wetu wengi wana tabia ya kutaka faida na mafanikio ya harakaharaka, kila mtu anapenda kumiki nyumba, gari, simu nzuri, na kusaidia wazazi wake nyumbani. Hii inasababisha wawe:

1. Wezi wa mali na muda za mwajiri
2. Wavivu wa kazi
3. Walalamike kila wakati
4. Waondoke kazini mara kwa mara kwa visingizio mbalimbali

Kazi ya private sector imewachinda watu wengi wakiwemo hata wasomi wakubwa. Wasomi wetu wengi wameajiriwa na serikali wanashindwa kujiari. Hivyo Wakuu wa wilaya, mikoa, wabunge na mawaziri wana kazi ya kuilea private sector ikue nchini. Wasiwe wepesi wa kutoa matamko ya kufungia viwanda na biashara za watu binafsi bali watoe ushauri wa kuboresha wakti wakiendelea na uzalishaji.
2. Wizi sehemu za kazi

Vijana
 
Umenena ukweli.....wachache watakuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa mdau wa kudumu wa private sector naungana na wewe kwa 100% , huo ndio ukweli halisi.
 
Iwe holela??
Ingini kubwa ya private sector ni kuwa
i) holela,
ii) njia za mkato,
iii) ukwepaji kodi,
iv) utoaji ajira zisizo na uhakika sana na
v) kutengeneza faida kubwa ya chapuchapu.

Hayo mengine nakubaliana na wewe ila haya kwenye paragraph ya kwanza kwa kweli hapana, maana hayana na utofauti na wizi kama wizi mwingne wowote tu ule!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…