unataka kushitaki wamekufanyia nini, je ni kesi ya madai au ni keshi ya jinai? yaani, wamekutendea kosa la jinai? au una madai nao ya aina fulani hivi sasa unataka mahakama iamue wakulipe?...<br />
<br />
kama ni madai unawadai kitu, hiyo ni kesi utakayoianzisha wewe mwenyewe. lakini kama ni kosa la jinai wamekutendea, sio wewe utakayewapeleka mahakamani, ila Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Republic) ambao wana dhamana ya kukulinda wewe kama raia wake, watakushitakia hao watu badala yako. ila unachotakiwa kufanya ni kupeleka hilo jambo polisi, polisi watawakamata hao watu na kuwafungulia shitaka la jinai, mahakamani atakayeendesha shitaka hilo ni Public prosecutor (PP) au state attorney (kulingana na eneo ulipo kwani state attorneys hawajaenea tz nzima, sehemu zingine polisi baadhi wanaact kama public prosecutors, baadaye mashitaka yote yataendeshwa na mawakili wa selikali tu).