process za kuomba passport kwa mtanzania aliyezaliwa nje ya nchi

process za kuomba passport kwa mtanzania aliyezaliwa nje ya nchi

yeto

Member
Joined
Aug 23, 2010
Posts
59
Reaction score
40
Habari waungwanaNaomba msaada wa hili swala kwa wazee wa fikra pevu, kuna rafiki yangu alizaliwa nje ya nchi baadae familia ikarudi tz, akasoma primary mpaka college hapa nchini, juzi alienda kuomba passport akakutana na waungwana wakamtisha wakamwambia yeye sio raia je process ya kuomba passport ikoje,viambatanisho gani aweke, anacheti cha kuzaliwa cha hiyo nchi akikiweka kitamsaidia au ndio kitaharibu?natanguliza shukrani
 
Uongo mkubwa wa hao watishaji,mtu akizaliwa nje na wazazi watanzania na yeye ni mtanzania,aweke cheti cha huko alikozaliwa,ana haki ya kupata passport
 
Uongo mkubwa wa hao watishaji,mtu akizaliwa nje na wazazi watanzania na yeye ni mtanzania,aweke cheti cha huko alikozaliwa,ana haki ya kupata passport
Nilishawahi kushuhudia case kama hii, mtu alizaliwa nje ya Tanzania na wazazi wote wa-Tanzania. Kasoma shule ya msingi hadi Secondary Tanzania, akapata nafasi kwenda kusoma nje ya nchi; kwenda uhamiaji waungwana wakamnyima passport ya Tanzania, jamaa akaenda ubalozi wa nchi aliyozaliwa hapo bongo,huo ubalozi wa nchi aliyozaliwa wakampatia passport ya hiyo nchi aliyozaliwa~mpaka leo jamaa anakula bata huko kwao!.
 
All in all kama yupo above 18,ana option ya kuchagua uraia wa Tz au huko alikozaliwa
 
Mimi binafsi nilikuwa kwenye same position. Nilichokifanya ni kuukana uraia wa nchi niliyozaliwa mara nilipofikisha miaka 18. Kuna form nilijaza pale ofisi za uhamiaji karibu na ofisi za UN na Halmashauri ya Jiji (Sijui kama bado ipo hapo). Nilipoenda kuomba passport niliambatanisha na hiyo form nikapata bila ya matatizo.
 
Pasipoti za Tanzania nijuavyo mimi hazitolewi kirahisi sana....Kwa maana nyingine si haki ya kila raia kuwa nayo. Hapo zamani nakumbuka NCCR ikiwa inavuma walikuwa na sera kwamba pasipoti iwe haki ya kila mtz. Haki ya kwenda kokote utakako pasipo kuvunja sheria ipo kikatiba. Utekelezaji unamashaka ndani ya uhamiaji. Hata hivyo, kabla ya mtu kupewa pasipoti ni lazima athibitishe pasina shaka kuwa yeye ni raia wa Tanzania. Kama huyu ndugu alizaliwa nje ya nchi...jamaa watahitaji kujiridhisha kuwa yeye kweli ni mtanzania na hakupata uraia wa huko alikozaliwa.
Zipo nchi ambazo ukizaliwa tu unakuwa raia! Kwa mantiki hiyo itabidi uthibitishe kuwa hili halikukutokea wewe, na kama lilikutokea, ukifika miaka 18 amua kuukana huo uraia wa ugenini,ili ubakiwe na uraia wa Tz peke yake. Ukithibitisha hayo pasipoti utapata.
 
Back
Top Bottom