Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Katika Salam zake alizotoa akiwa pamoja na baadhi ya Walimu wa Mkoa wa wa Njombe Prof. Mkenda amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Walimu katika ujenzi wa Taifa kwa kuelimisha na kulea watoto na vijana wa Kitanzania.
Amesema: "Leo ni siku ya kuwashukuru walimu na kwa niaba ya wananchi wa Tanzania nasema Asanteni Walimu, leo ni siku ya kuwatia moyo walimu."
Aidha, amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau imeandaa mwongozo wa kutoa motisha kwa Walimu ili kuwapa hadhi stahiki na kwamba ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 inayotaka walimu kutaminiwa na kutambulika
Kauli mbiu ya kimataifa ya Siku ya Walimu Duniani Mwaka huu inasisitiza usikilizwaji na ushirikishwaji wa walimu katika masuala ya elimu