SoC02 Prof. George Wajackoyah na sera yake dhidi ya bangi

SoC02 Prof. George Wajackoyah na sera yake dhidi ya bangi

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Sep 12, 2022
Posts
24
Reaction score
12
“Hempu ni hitaji la kwanza la ulazima kwa utajiri na ulinzi wa nchi…huduma kubwa/ nzuri ambayo inaweza kupewa taifa lolote ni kuongeza mmea wenye manufaa kwenye utamaduni wake.” –Thomas Jefferson, Raisi wa tatu wa Marekani na muasisi wa taifa hilo.

1.jpg


Mgombea Uraisi wa Kenya Prof. G. Wajackoya, kupitia chama cha Roots Party, 2022 ni shujaa na kiongozi wangu. Shujaa ni kufanya jambo ambalo watu huliogopa kwa sababu mbalimbali kama vile kuchekwa, kuchukiwa, kuhatarisha maisha na kuchukuliwa vibaya na watu wengine. Shujaa anasifa za uthubutu na kujiamini. Maana rahisi ya kujiamini ni kupita katikati ya chumba bila kujali nani anakuangalia. Prof. Wajackoyah amesimama katikati ya majukwaa ya kisiasa na vyombo vya habari kueleza kilimo cha kanabisi hususani hempu huku akifahamu kuna watu watamshambulia na kumkejeli elimu yake na kile anachokifanya. Prof. Wajackoya sehemu ya wasifu wake ni msomi wa digrii takribani 16 na alikuwa mkimbizi wa kisiasa nchini Uwingereza na Marekani, mataifa ambayo hempu ni kilimo halali.

2.jpg


Sio kwa sababu vitu ni vigumu ndio hatuna uthubutu, ni kwa sababu hatuna uthubutu ndio maana vitu ni vigumu. Sehemu kubwa ya wasomi wa Afrika hasa waliopo/waliokaa njee si kwamba hawaelewi kile alichokuwa anakipigania Prof. Wajackoya bali hawana uthubutu na kujiamini. Hakuna DIASPORA waliojitokeza kukemea kejeli na upotoshaji wa viongozi wa dini na maafisa wa serikali ambao kimaadili hawapaswi kuingilia sera za wanasiasa wakati wa kampeni.

Sifa ya kiongozi ni kuongoza na sio kuongozwa na ili kiongozi asiongozwe ni lazima awe na uwezo wa kubeba maono au kuona mambo nje ya ufahamu wa kawaida wa watu waliomzunguka ndani ya jamii yake. Sifa hii ndio inayomfanya kiongozi kuongoza na sio kuongozwa na jamii. Kiongozi anayeongozwa na jamii mara nyingi huzungumza mambo ya kufuraisha watu wengi hata kama ni uongo au hayaamini lakini anataka kura/ kuungwa mkono.

Prof. Wajackoya katika kampeni zake hakujikita katika kutoa ahadi bali namna atakavyo pata mapato ya kuendesha serikali yake na kulipa deni la taifa. Moja kati ya vyanzo alivyovitaja ni kilimo cha mimea jamii ya kanabisi hususani kanabisi sativa au hempu/ hempu ya viwanda ambayo haina ulevya na inastawi vizuri kwenye ardhi yeyote inayostawi mahindi.

Hempu ni nini?
Hempu (Hempu ya Viwanda) ni mmea wenye kufanana na mmea wa maruhana/ daga. Yote ni mimea ya jamii ya kanabisi. Tofauti ya hempu na maruhana/ daga ni kiasi cha ulevya (Tetrahydrocannabinol/ THC) na urefu. Maruhana/ daga ina kiasi kikubwa cha THC, 5%-20% ukilinganisha na hempu 0.3%-1%. Hempu ni ndefu zaidi ya maruhana/ daga. Hempu hukua hadi kufikia urefu wa mita tano wakati maruhana/ daga haizidi mita mbili.

4.jpg

3.png

Matumizi ya hempu:
Hempu hutumika kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo ya uzalishaji bidhaa za; nishati, chakula, chakula cha mifugo, viinilishe, nguo, madawa.

5.png


Kwanini hempu ilipigwa marufuku?
6.png


Rushwa kutoka kampuni ya DUPONT iliwezesha katazo la hempu. Hempu imelimwa kwa zaidi ya miaka 10,000 na kuanza kukatazwa baada ya mwaka 1937 kufuaatia propaganda/ uongo ulioanzishwa na kampuni ya Dupont kulinda maslai yake kwenye biashara za mafuta/ nishati, nyloni, plastiki, karatasi, vilipuzi na mbao ambapo hempu ingezalisha bidhaa bora zaidi kufuatia uvumbuzi wa mtambo wa ‘‘decorticator’’ ambao hutumika kuondolea nyuzi kwenye mimea kama katani. Misri ndio taifa la Afrika ambalo halikuathiriwa na propaganda za Magharibi kuhusu hempu.

Nchi zinazolima hempu
Screenshot_20220913-223712.png



Nchi zote za viwanda zinalima hempu
Zaidi ya nchi 40 zinalima hempu zikiwemo:China,India,Korea ya Kusini, Marekani, Thailandi, Australia, Kanada, Chile, Austria, Denimaki, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Wingereza, Hungari, Urusi, Uspaniola, Uswizi, Ukraine, Japani, Uholanzi na uruguai. Hakuna nchi ya viwanda isiyolima hempu.

Nchi zinazojihusisha na hempu Afrika ni pamoja na; Misri, Afrika kusini, Malawi, Zambia, Uganda, Zimbabwe, Lesotho. Ukiacha Misri ambayo haikuwahi kuacha kulima hempu nchi nyingine za Afrika kilimo hiki kipo kwenye hatua za uchanga na hatua za majaribio.

Kwenye baadhi ya nchi kama Tanzania kilimo hiki kimeshindwa kuanza kwa sababu hakuna tofauti ya hempu na maruhana/ daga inayoonekana dhahiri kwenye sheria za nchi zilizopo.

Ibara ya 28 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa unaojulikana kama Single Convention on Nacortic Drugs, 1961, inaondoa kilimo cha hempu katika katazo.

Kwa mujibu wa kampuni ya India, Bombay Hemp Company (BOHECO) dhamani ya hempu inafikia $ 1.5 Trilioni takribani TZS 3 quatrilioni katika soko la dunia. Unaweza kutembelea tovuti ya BOHECO kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii kufahamu bidhaa za hempu zinazozalishwa na BOHECO.

Screenshot_20220913-223926.png

Screenshot_20220913-223838.png

Kwa mujibu wa gazeti la”EASTAFRICAN” Zambia inauwezo wa kuvuna $30 Mil. sawa na TZS 70 Trilioni kila mwaka. Kwa kuzingatia Geografia ya Tanzania, taifa hili linauwezo wa kuvuna zaidi ya TZS 90 Trilioni kama wakulima wake wa mahindi wataruhusiwa kulima hempu. Kufahamu jinsi kilimo cha hempu kilivyo tembelea tovuti na kurasa za kijamii za kampuni ya Malawi inayoitwa “INVEGROW.”

7.png

8.png

9.png

10.png


11.png

12.png


13.png

Kiongozi huonyesha njia. Prof. Wajackoya ametuonyesha njia ya kuachana na tozo na kufikia uchumi wa kati kabla ya 2025. Pato la maua ya hempu kwenye ekari moja ni $150,000 zaidi ya TZS 300 Milioni, linawezesha kila kaya kufikia uchumi wa kati na serikali kupitia taasisi zake kama, magereza, vyuo, jeshi la kujenga taifa, hifadhi za taifa, halimashauri n.k. kuzalisha hempu ya kutosha ili kuokoa fedha za kigeni, kuuza njee, kupunguza tozo n.k

Kufahamu zaidi kuhusu hempu soma kitabu au “E BOOK” bure inayoitwa Hempu kwa Afrika kwa kutembelea
“HEMPOWER AFRICA” kwenye mitandao ya kijamii.
IMG-20220716-WA0002.jpg



 

Attachments

  • Prof-3.doc
    Prof-3.doc
    2 MB · Views: 7
  • 6.png
    6.png
    154 KB · Views: 15
  • Screenshot_20220913-223926.png
    Screenshot_20220913-223926.png
    37.2 KB · Views: 13
  • Screenshot_20220913-223838.png
    Screenshot_20220913-223838.png
    24.4 KB · Views: 14
Upvote 2
Back
Top Bottom