The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
“Mara ya mwisho mimi kunywa Juisi au Soda ni Mwaka 2000. Iko hivi, kuna tofauti kubwa ya kula chungwa na kunywa juisi ya Chungwa. Nikinywa Juisi nakunywa Sukari moja kwa moja hata kama haijawekewa sukari. Mfano, ili nipate glasi moja ya Juisi ya Chungwa nahitaji Machungwa matano. Asubuhi umekunywa glasi moja ya juisi, hayo ni Machungwa Matano. Mchana umekunywa glasi ya pili, hayo ni machungwa 10. Jioni umekunywa glasi nyingine, yanakuwa machungwa 15 kwa siku. Kwa siku 10 ni machungwa 150, Kwa mwezi ni machungwa 450. Umekula shamba”
Prof. Janabi alitoa ushauri huu Oktoba 8, 2024 kupitia Afya Podcast ya Muhimbili TV wakati anatoa Elimu juu ya Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza huku akisisitiza kuwa matunda huwa na sukari ya Fructose ambayo ikitumika kwa wingi inaweza kuwa na hatari kwa afya.
Alibainisha kuwa Juisi huwa na Mjumuiko wa Matunda mengi hivyo ni Muhimu kula tunda lenyewe kwani ni ngumu mtu kula matunda mengi kwa wakati mmoja, pia huwa na nyuzilishe zenye manufaa kwa afya