Prof. Jay amekiri kuwa msoto ni mkali nje ya uheshimiwa, atangaza kurudi na albamu kali

Prof. Jay amekiri kuwa msoto ni mkali nje ya uheshimiwa, atangaza kurudi na albamu kali

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Prof. J. Mzee wa Mitulinga leo ndani ya 360 amekili kurudi mchangani alikotoka baada ya kuiambia 360 kuwa mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani zile singo zilikuwa cha mtoto. Profesa huyo ambaye hata historia yake ya shule haijulikani vizuri kama aliishia fomu foo au wapi amejinasibu kuleta mziki kama kitabu yaani kisomi, ambacho kitakuwa na sulat, aya na vichwa vya habari, mafunuo na umuhimu wa mwanamke.

Ameliki kipindi cha kuwatumikia wanchi kimepita sasa anaanza kutumikia mziki tena, kwani kipindi cha uheshimiwa alibanwa sana na kale kamuda. Yaani kwa jinsi nilivyo muelewa ni kuwa anawataadharisha wapinzani wake kuwa sasa anakuja kama HEAVY WEIGHT uzito kuliko ule uzito wa kwanza na yeye apigi kwingine ila anapeleka za uso tupu yaani kama anamchakaza shoo ya mbele ya mtu/wapinzani wake.

Kipekee mimi kama Mtoto wa Mchungaji nimempenda sana Profesa Jay kupitia wimbo wake wa NDIYO NA SIYO MZEE kutujulisha kuwa siasa za Afrika ni uongo na ndiyo maana hata yeye imekuwa ngumu kuendelea katika kipindi cha pili kwani alijitabilia tayari katika SIYO MZEE.

Ukizisikiliza zile nyimbo za NDYO MZEE na SIYO MZEE utaweza kuona jinsi Profesa alivyokuwa mkomavu katika tasnia hiyo ya mziki wa kufokafoka na alikuwa kweli kwa zaidi ya 900% ndiyo maana hata kule jimboni Mikumi hakuna hata kitu alichofanya, kwa mtu mwenye akili atasema hiki tutamkumbuka Profesa hakuna, akibisha azikatae nyimbo zake.
 
Mzee wa mitulinga tunakusubiri kwa hamu ingawa naamini hautakua na uwezo ule wa zamani kipindi kile njaa kalii ila kwasasa umeshiba
 
Mi naona angetulia tu aitumie hela ya ubunge kuwekeza kwenye vitu vya maana, muziki afanye for fun tu. Hii miziki anayoifanya sahivi hawezi kucompete na vijana wa sasa kwanza haendani nayo, zaidi naona atajifutia legacy kubwa aliyonayo. Hamuoni mwenzake Sugu?
 
Mi naona angetulia tu aitumie hela ya ubunge kuwekeza kwenye vitu vya maana, muziki afanye for fun tu. Hii miziki anayoifanya sahivi hawezi kucompete na vijana wa sasa kwanza haendani nayo, zaidi naona atajifutia legacy kubwa aliyonayo. Hamuoni mwenzake Sugu?
Upo sahihi mkuu. Nafikiri kuna vitu umri ukishakutupa mkono ni bora ukaachana navyo na kufanya ishu zingine tu. Unless otherwise atafute jinsi ya ku blend muziki wake na hawa vijana wa sasa, kwa maana ya kufanya sana collabo na vijana kitu ambacho hata ivyo bado kinaweza kisiwe rahisi sana..
 
Afungue club Kali atatoboa .muziki Ni kama udereva una mwisho
 
Kama mwenzetu aliekua mbunge anasema hali ngumu huku akiwa na uhakika wa mafao sie tulio kitaa itakuaje?
Mungu atutetee tu
Kweli kabisa mkuu,inashangaza Sana kumsikia former mbunge kudai vyuma vimekaza upande wake na sisi wamachinga tusemeje?
 
Back
Top Bottom