Prof. Jay ft Black Rhino, Complex, AY and Adili Chapakazi - Nawakilisha

Prof. Jay ft Black Rhino, Complex, AY and Adili Chapakazi - Nawakilisha

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
images-68.jpg
PROFESSOR JAY FT. ADILI CHAPA KAZI , COMPLEX, AY & BLACK RHINO - NAWAKILISHA ( STUDIO BONGO RECORD)

Chorus ( Professor Jay)

Nawakilisha...!!!
Ofisini na masela ndani ya gheto
Nawakilisha ...!!!
Kwa ma ding vijana mpaka watoto
Nawakilisha...!!!
Kenya , Uganda 🇺🇬 na Tanzania 🇹🇿
Huu ni hosia bila umoja hakuna njia.

Nawakilisha...!!!
Ofisini na masela ndani ya gheto
Nawakilisha ...!!!
Kwa ma ding vijana mpaka watoto
Nawakilisha...!!!
Kenya , Uganda 🇺🇬 na Tanzania 🇹🇿
Huu ni hosia bila umoja hakuna njia.

Verse.. 1 ( adili chapa kazi)

"Stadi za Tenzi, Adili upeo fanisi Taasisi ya taaluma halisi,ni zaidi ya maarifa / vumbua mistari ambayo haipo katika uwezo wa fikra/ sasa mtazamo wa viwango jumuhiya batili / ma saa arobaini ya ziada na nane ya Zaida ni waooshe ubongo/ adili na beti kamili zenye mizani thamanii zaidi ya madini/ Mwanana kwenye mic na bariki kama yohana / kwani tamati, imewadia machozi na majonzi kama jay dee mnalia/ weka mbali malenga mnaosifia huu ubongo ni Shakespeare / kwenye anatomi za ma mceez mithili ya kasa nimeingia / daraja la juu la ma umahiri wa Tenzi shuhudia/ wengi mnajuta kushindana uwezo zaidi ya 🖥 computer.."

Verse.2 ( black rhino)

Niko underground ndani ya town sina papara/ full mkoba taratibu ndani ya msafara/ usilete mkwara ipo siku nitatawala/ wakati umefika nimekita kama namadala / kenge wengine wote mi nawaona mafala/ night kisa Bongo ,Visiwani mpaka Bara/ nimekuwa kinara kila kitengo mi nang'ara/ Mc kichwa ngumu hata mbele ya mnyapara/ niko imara siongopi kufanya kafara/ nyumbani mi nimehaga kwa matambiko na sala/ sifanyi mashindano ya Ku Rap na masakara/ wenye ubongo mdogo na mawazo ya kifara/ vichwa vya panzi wasio tambua hii biashara/ wanafikiri Rap ni sawa na mduara/ ndio maana Album zao zimejaa hasara / "jay" nipe mistari "p" naomba Ala / ili niwakilishe maneno yenye busara/ moja kwa moja rhino napiga goti kwa Allah / sina papara / na wala simaindi dini uchara / wanaotupiga vita na tuwafanye tohara / ...

Verse..3( professor jay)

Swadata..!! Toka utotoni sauti inawika/ nami napiga goti kwa watu nakubarika/
Najenga imani kwa mashabiki wengi ma dingi/ vinapo chekechea na hata shule za msingi./

Yooh .!! Mam sapu nipoze moyo mama/ baadhi ya wanafiki naona sasa wanapana/ jina linapo kua na kashfa zinashamiri/ watu wenye hekima bado wananipa ujasiri /

Jay endelea kuifunza jamii yoh!! Natumia mifano ya kweli ndani ya fasihi / wakilisha pande zote mbeya na sumbawanga/ mwanza na kikita na Tanga na nina pepeta na twanga / natoa heshima sawa kwa professor na tahira/ vigumu kuniringajisha na mc Asie na dira / waga naona hawataki, wengine naona wana zira/ nauliza thamani ya Zidane na runyamila

Chorus ( professor jay)

Nawakilisha...!!!
Ofisini na masela ndani ya gheto
Nawakilisha ...!!!
Kwa ma ding vijana mpaka watoto
Nawakilisha...!!!
Kenya , Uganda 🇺🇬 na Tanzania 🇹🇿
Huu ni hosia bila umoja hakuna njia.

Chorus ( professor jay)

Nawakilisha...!!!
Ofisini na masela ndani ya gheto
Nawakilisha ...!!!
Kwa ma ding vijana mpaka watoto
Nawakilisha...!!!
Kenya , Uganda 🇺🇬 na Tanzania 🇹🇿
Huu ni hosia bila umoja hakuna njia.

Verse..4 ( Ay) mzee wa commercial


Hizi si dude zako ni tele mwiko mzuri hapa ni chuma cha pua/ panipo dili dume hautakiwi kutambua/ nayo sababu mtoto wa mama we unaweza kutimbua/ kwangu wewe bwetere , mkia wako fyetere/ kama ni ndege mi ni tai we utabaki tetere/ mwendo wa kucheba tu / mbele ya sura hizi utie mguu we dhubutu/ mi nipo na mwendo wangu hado hado / ndani ya game midi lenye makubwa na madogo/ Ay at Rap star dot. Com/ ni tatu pata somo toka C.b.m / karabao salam kwa wasubaa hao/ wanaotengemea maisha kwa vyeo vya baba zao/ unajibweteka tu uta olewa bila mali/ usi lale lale bwana ndani ya life we weka msuli/Mtu bila malengo hai ni mwana mpotevu/ njoo uonyeshe njia nami au hauna mti mkavu/ Ay na jay ama snoop doggy , Dr. Dre / chele limeiva ila lakini ndio limejaa mawe / undwazi wako mbali hapa kwetu usisongee

Verse.. 5 (Complex.)

Na bado mkwanja unatesa viwanja/ ni vichwa vya nyanja/ maumivu kote na ganja / tawala mic kijanja/ sasa mc vizuri muda hu kudanja/ na tupa mawe fikra miba vichaka vyote nachanja/ tafadhali kaa mbali .. kaa mbali ni hatari/ hapa utalamba tope maktaba kwisha labda ukakope/ unauliza nini jivukoni nilipowaziba babazoni / yeah!... babazoni Usoni vipi maji shingoni/ sema..!!.. P funk ......!!

Yeah naona vigongo wa chance Donge la wakaba Angani ninapoleta mambo haya/ mambo yangu si haba mwanga Course nyunyiza vina kwenye vibaba..

Chorus ( professor jay)

Nawakilisha...!!!
Ofisini na masela ndani ya gheto
Nawakilisha ...!!!
Kwa ma ding vijana mpaka watoto
Nawakilisha...!!!
Kenya , Uganda 🇺🇬 na Tanzania 🇹🇿
Huu ni hosia bila umoja hakuna njia.

Nawakilisha...!!!
Ofisini na masela ndani ya gheto
Nawakilisha ...!!!
Kwa ma ding vijana mpaka watoto
Nawakilisha...!!!
Kenya , Uganda 🇺🇬 na Tanzania 🇹🇿
Huu ni hosia bila umoja hakuna njia.

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202

Album ya Profesa Jay, Machozi Jasho na Damu. Ndio Album Bora ya HIP HOP ya muda wote?

Miaka ya 1990 ilishuhudia kuibuka kwa wasanii wa kwanza wa Hip Hop wa Tanzania. Kundi la Hard Blasters, ambalo lilikuwa na wasanii kama Profesa Jay, lilikuwa mojawapo ya makundi ya kwanza kutambulika katika tasnia hii. Walianzisha muziki wa Hip Hop uliochanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza na kuanza kueneza ujumbe wa kijamii na kisiasa kupitia nyimbo zao.

Kutoka kwa mtindo wa awali wa Hip Hop uliotumia sampuli za muziki wa Magharibi, wasanii wa Tanzania walikuwa na hamu ya kujenga miondoko inayojumuisha sauti za Kiafrika. Hii ilisababisha kuibuka kwa muziki wa Bongo Flava, ambao ni mchanganyiko wa Hip Hop na vyombo vya asili vya Kiafrika.

#funguka
Nani alipasuka zaidi ya mwezake katika collabo hii ya wakilisha nyimbo iliyopatikana katika Album ya Profesa Jay machozi jasho na damu
Kati ya .

Profesa Jay,
Black rhino
Ay
Adili chapa kazi

Na marehemu complex. .
 

Attachments

  • images-69.jpg
    images-69.jpg
    23.1 KB · Views: 4
  • images-66.jpg
    images-66.jpg
    41.6 KB · Views: 6
  • 600x600bf-60.jpg
    600x600bf-60.jpg
    83.6 KB · Views: 6
Bonge la ngoma ,haijawahi kuchuja mpaka Leo, verse ya AY ilikuwa ngumu sana .
 
Back
Top Bottom