Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
PROF. KABUDI: HISTORIA YA WANAWAKE WALIOPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Siku mbili hizi zimekuwa siku za furaha kwangu kwa kuona katika hadhira kubwa sana za CCM wapigania uhuru waliosahauliwa kwa miaka mingi wakitajwa.
Katika kongamano la UWT lililofanyika Dodoma kutangulia sherehe ya kuadhimishwa kuzaliwa kwa CCM Prof. Kabudi alizungumza historia ya UWT.
Katika kuwasilisha mada yake aliwataja baadhi ya wanawake waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Prof. Kabudi aliwataja Shariffa bint Mzee wa Lindi, Mama bint Mwalimu na Halima Selengia wa Moshi na Bint Maftah Karenga mwasisi wa TANU Dodoma.
Prof. Kabudi alimweleza bint Maftah Karenga kuwa alikuwa mama wa Kimanyema.
Jingine ambalo ni muhimu ni kuwa katika waasisi wa TANU Bint Maftah Karenga alikuwa mwanamke peke yake.
Prof. Kabudi alimtaja pia Bi. Hawa bint Maftah wa Mtaa wa Mkunguni, Dar-es-Salaam kama mhamasishaji mkubwa katika TANU kupitia Lelemama.
Prof. Kabudi akahitimisha kwa kueleza historia ya Bibi. Titi na mchango wake Mombasa alipokwenda kuwatia moyo Wakenya wasikate tamaa kwa viongozi wao akiwemo Jomo Kenyatta kuwekwa jela.
Mkutano huu Bibi Titi aliufanya Tononoka Hall ukumbi maarufu Mombasa.
Kwa hakika huu ni utamaduni mpya na udumishwe kuwaenzi mashujaa wetu waliopigania uhuru hadi ukapatikana kwa amani na salama.
Napenda kuweka majina ya waasisi wa TANU Dodoma 1955 : Alexander Kanyamara (President); Haruna Taratibu (Vice President); Abdu Mohamed Mwamba, (Secretary); na Omari Suleiman (Treasurer); Miongoni mwa wanachama waasisi ni Binti Maftah Karenga, Bakari Yenga, Maalim Khalfan, Idd Waziri na Said Suleiman.
Historia ya TANU unaweza kuisoma katika kitabu hicho hapo juu kipo Tanzania Publishing House (TPH), Samora Avenue kwa Kiswahili na Kiingereza.