SI KWELI Prof. Kabudi asema aliyevujisha mkataba wa DPW katuvua nguo

SI KWELI Prof. Kabudi asema aliyevujisha mkataba wa DPW katuvua nguo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Inadaiwa kuwa Prof. Palamagamba Kabudi amenukuliwa kwenye Mtandao wa Clubhouse akisema alievujisha huu Mkataba wa Bandari ametuvua Nguo, tumeweka Ujinga wetu wote hadharani.

IMG_8087.jpeg

Ni kwei Prof. Kabudi kazungumza maneno haya?
 
Tunachokijua
Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi alizaliwa Februari 24, 1956 mkoani Singida. Alianza kusoma shule ya msingi Kilimatinde mwaka 1964 kisha 1965 hadi mwisho wa 1966 akaenda shule ya msingi Kitete.

Mnamo 1967 alihamia Shule ya Msingi ya Berega kabla ya kumaliza masomo yake ya msingi katika Shule ya misheni ya Mvumi.

Mwaka 1971 alijiunga na shule ya upili ya Tosamaganga alipomaliza kidato cha 4 mnamo 1974 kisha Shule ya Milambo, Tabora kwa elimu ya Kidato cha 5 na 6 mwaka 1975-1976.

Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alisoma sheria hadi kuhitimu na shahada ya uzamili mnamo mwaka 1986.

Mwaka 1989 hadi 1995 alisoma Chuo kikuu cha Berlin, Ujerumani akapokea shahada ya uzamili (PhD) ya sheria.

Alikuwa profesa ya sheria kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi mwaka 2017 alipoitwa na Rais Magufuli kuwa mbunge wa kuteuliwa na kuwa waziri wa sheria.

Mwaka 2019 alibadilishwa kazi kuwa waziri wa mambo ya nje. Mwaka 2021 alipangwa tena wizara ya sheria na katiba.

Prof. Kabudi na Sakata la DP World
Tangu taarifa za Tanzania kuingia mkataba na Kampuni ya Dubai ya DP World kuanza kuenea mnamo Juni 5, 2023 mwaka huu na Azimio la mkataba huo lilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Juni 10, 2023, watu wengi wamekuwa wanamuulizia Prof. Kabudi.

Juni 16, 2023, mdau wa JamiiForums aliweka chapisho lililohoji ukimya wa Profesa huyu maarufu wa Sheria nchini juu ya suala la Bandari kupitia andiko lenye kichwa cha habari “Baba wa mikataba Prof. Kabudi yuko wapi mjadala wa mkataba wa kuuza bandari?.”

Kuhoji huku kwa wananchi kunatokana na uwepo wa historia isiyotiliwa shaka ya Ushiriki wa Prof. Kabudi kwenye mikataba mingi ya wawekezaji nchini.

Mojawapo ya majadiliano ya kimkataba yaliyowahi kusimamiwa naye ni pamoja na yale yaliyohusisha Sakata la Makinikia na Kampuni ya Barrick Gold ambapo Oktoba 17, 2017, makubaliano ya kuilipa Serikali ya Tanzania hisa ya asilimia 16 na mgawo wa 50% ya mapato ya mauzo ya dhahabu kutoka migodi 3 inayoimiliki yalifikiwa.

Pia, Barrick walikubali kutoa Dola za Kimarekani milioni 300 kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kutokana na biashara ya kampuni hiyo.

Baadae Oktoba 4, 2022, Prof. Kabudi kama mpatanishi Mkuu wa Serikali aliibuka na madai ya kuwa Pesa zinazokadiriwa kufikia Tsh. Trilioni 360 ambazo Acacia walisema watalipa kama malimbikizo na faini ya ukwepaji kodi hakikuwa kiwango sahihi, yaani ilikuwa Kanyaboya.

Kumbukumbu za mjadala huu zilichapishwa pia na JamiiForums kwenye andiko lenye kichwa cha habari “Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”.

Pia, umaarufu wa Prof. Kabudi ulishika kasi mwaka 2020, akiwa Waziri wa Mambo ya Nje baada ya kwenda Madagascar kwa kutumia ndege ya Rais kufuata dawa iliyodaiwa kuwa na uwezo wa kutibu Maradhi ya COVID-19.

Haya ni miongoni mwa matukio machache kati ya mengi yaliyomfanya Prof. Kabudi kuwa maarufu miongoni mwa Watanzania hadi kuuliziwa uwepo wake kwenye sakata hili la uwekezaji wa Kampuni ya DP World kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Baadae Julai 20, 2023, Kauli inayodaiwa kuwa imetolewa na Prof. Kabudi kwenye mtandao wa Clubhouse ilianza kusambaa.

Kauli hiyo inasema;

“Alievujisha huu Mkataba wa Bandari ametuvua Nguo, tumeweka Ujinga wetu wote hadharani"

Ni kweli Prof. Kabudi kaamua kuvunja ukimya?
JamiiForums imefuatulia mijadala inayofanyika mara kwa mara kwenye mtandao wa Clubhouse ili kupata uhakika wa madai haya.

Katika ufuatiliaji wa awali, imebainika kuwa Prof. Kabudi hatumii Mtandao huo.

Japokuwa madai ya wanaosambaza ujumbe huo yanasema yeye binafsi alipigiwa simu wakati mjadala unaozungumzia masuala ya Bandari unaendelea ili atoe maoni yake, JamiiForums hajapata uthibitisho wowote wa sauti au chumba mahsusi kilichofanya mjadala huo.

Aidha, hakuna kumbukumbu zozote zilizohifadhiwa mtandaoni zinazotoa taarifa, dokezo au tetesi za Prof. Kabudi kutoa maoni yake kuhusiana na sakata la Bandari.

Uchunguzi wa JamiiForums umebaini kuwa Prof. Kabudi alizungumza hadharani mara 2 mfululizo kwenye tarehe za mwisho za mwezi Mei wakati akichangia kwenye vikao vya Bunge la 12, Mkutano wa 11 Kwenye mijadaa inayohusu uraia pacha na Uunganishwaji wa Bahari ya Hindi na Atlantinki.

Hivyo, taarifa zinazosambazwa zikimhusisha ni uzushi ulioanzishwa pengine kwa lengo la kuongeza ukubwa wa mjadala unaohusu Sakata la uwekezaji wa Kampuni ya DP World Bandarini linaloendelea nchini hivi sasa.

Pia, hata baada ya kuombwa mara nyingi ushahidi wa sauti inayonukuu maneno hayo, watu wanaosambaza madai hayo wameshindwa kuitoa hadharani. Huu ni uthibitisho mwingine wenye tafsiri ya kutokuwepo wa ushahidi wa kile wanachokiandika.
"Alievujisha huu Mkataba wa Bandari ametuvua Nguo, tumeweka Ujinga wetu wote hadharani" Kabudi Clubhouse https://t.co/lOPJprSTCv
Jitu lililotumwa na Jiwe likachoma mafuta ya ndege zetu mpaka Madagascar kuchukua mitishamba eti dawa ya COVID na likajisikia fahari kubwa sio jitu la kusikiliza. Napinga mkataba mbovu wa bandari lakini sitasikiliza hoja za professa wa jalalani hata kidogo.
 
Rejea historia yake kielimu. Kwa umri wake haiwezekani awe high school mwaka 1971 na 1972. Tuliokuwa Operation Tujisahihishe mwaka 1977 pale Ruvu huyu alikuwa mwenzetu akitokea huko Tosamaganga. Tafadhali rekebisheni mapungufu haya.
 
Sasa tunaomba jamii check ifanye appointment na na mwamba ili kubaini yeye kwa mtazamo wake anasemeje juu ya mkataba huu wa DP WORLD
 
Back
Top Bottom