Prof. Kabudi atakuwa busy kujifunza majina ya wasanii, wachezaji na wanamichezo mbalimbali

Prof. Kabudi atakuwa busy kujifunza majina ya wasanii, wachezaji na wanamichezo mbalimbali

Minjingu Jingu

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2023
Posts
1,072
Reaction score
2,384
Navyomjua mwalimu wangu kwa mudaa huu anakaa sana sebuleni kuangalia michezo ya kuigiza na kuwauliza watoto wake. Hapa yupi ni Bamboo? Yupi ni Kingwenduh?

Rayvanny ni yupi kati ya hawa? Lwiza Mbutuh? Ahoua yupo Simba au Yanga? Uwanja wa footaball jumla wanaocheza ndani ni wangapi?

Kisha hapo anafanya mazoezi ya kushika kauli mbiu ya mikia. UBAYA UBWELA.... Anaulizia Ally Komwe na Ahmed Ally ni mtu na baba yake?

Kisha ataanza kununua magazeti ya udaku na kuanza kuwafollow akina shilole, diva, harmorapper. Kwa sasa hata connection atakuwa anaomba aforwardiwe awe ana check kuhakikisha kabla hajaenda kukemea. Ataonana na kukaa na akina amber ruty wajadiliane mustakabali wa sanaa na usanii.

Steve mengele atakuwa ndo mshauri mkuu wa Prof Kabudi P. Rais akiondoka na wasanii kwenda nao sehemu Prof Kabudi atakuwa nao watoto wake akiwaelekeza ku behave. Kisha watakaa mezani kubadilishana mawazo.

Matches za Taifa Stars atakuwepo na pia atazunguka vyombo vya habari kuhamasisha watu kuhudhuria....akiwa na akina ally na ahmed. Watataniana pale wakiitana mikia na mwingine akiita utopolo.

Halafu siku moja atahojiwa na media atasema Utopolo wanapocheza na Mkia tunataka kuona ndondi safi kabisa uwanjani. Waandishi watacheka atakoleza. Utopolo wanatuwakilisha kombe la CUF na hawa Mkia wao wapo Kombe la Loser.

Baadaye watakuja mwambia. Uliharibu hayo majina uliyotumia si rasmi. Na mashindano yao hayaitwi vivyo. Atasema aaaaah....kumbe.
 
Navyomjua mwalimu wangu kwa mudaa huu anakaa sana sebuleni kuangalia michezo ya kuigiza na kuwauliza watoto wake. Hapa yupi ni Bamboo? Yupi ni Kingwenduh?

Rayvanny ni yupi kati ya hawa? Lwiza Mbutuh? Ahoua yupo Simba au Yanga? Uwanja wa footaball jumla wanaocheza ndani ni wangapi?
Ahahahahaha! Wamfundishe na neno Ubaya Ubwela na kwa Mkapa hatoki mtu! Ahahahahaha!!
 
Ila kuna ukweli, ile sekta inahitaji kidogo uwajuejue, Kabudi anawajua kweli kina harmorapa na vituko vyao, anasikiliza kweli nyimbo za hovyo na mashtaka yao ya kila leo basata..

Sema kama FA kabaki atakua anampiga tafu, mambo mengi bwanamdogo alikua anayamaliza kisanii.
 
Back
Top Bottom