Prof. Kabudi: Imani, uelewa na msimamo wako kuhusu Utumishi wa Umma ni nguzo kuu ya kuzaliwa Taifa mfu

Prof. Kabudi: Imani, uelewa na msimamo wako kuhusu Utumishi wa Umma ni nguzo kuu ya kuzaliwa Taifa mfu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Nimemsikiliza Profesa Kabudi akieleza nini Mtumishi wa Umma anapaswa kufanya, baadhi ya Mambo anayosisitiza ni pamoja na mtumishi wa Umma:

1. Kutii (obey) mamlaka iliyopo juu yake.

2. Kama ataki kuendana na mamlaka iliyopo juu yake aache kazi.

Katika karne ya sasa utii wa mamlaka za kibinadamu zilizopo juu ya mwanadamu imekuwa moja ya njia inayotumiwa kudhoofisha nguvu ya Mataifa mengi ya Afrika.

Kutii kila mamlaka au neno na maelekezo ya mamlaka zilizopo juu yako ni dalili ya woga na nidhamu ya uoga. Kwa kuwa watumishi wa Umma wanatumikia umma wanapaswa kutii na kutekeleza amri halali tu na si amri halali kwa mujibu wa mkubwa bali amri na maelekezo halali kwa mujibu wa mazingira halisi.

Viongozi wengi wamefanya ubadhirifu wa Mali za umma kupitia utii wa mamlaka, wanatoa maelekezo yanayokinzana na maadili lakini yanafuatwa kwa sababu ya kuzingatia principles za Prof.

Tubadilike, America wangetii mamlaka iliyo juu yao leo Trump angekuwa anasikilizwa lakini wameacha kumsikiliza si kwa sababu siyo kiongozi wao bali kwa sababu maelekezo yake yapo kinyume na matakwa ya jamii na umma.

Mzee Kabudi waelekeze watu watii amri na mamlaka halali kwa umma na wasitekeleze mamlaka zisizo halali. Si kila mkubwa wa cheo anania nzuri na umma , wakubwa wengi wana nia njema na matumbo yao na ndugu zao.

Hao unaotaka waheshimiwe wameheshimiwa na wakaliangamiza Taifa.

Tujifunze kupingana na mamlaka zinazotenda kinyume na kuungana na mamlaka zinazokwenda sawa na matakwa ya umma.

Hakuna mtumishi anayetakiwa kuacha kazi kisa mkubwa ni fisadi, fisadi ndiye anapaswa kuacha kazi. Tusiruhusu wakubwa wasio waadilifu wakalazimisha walio waadilifu kuacha kazi...tusimame imara kushughulika nao bila kujali ukubwa wao
 
Back
Top Bottom