KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Kila mara Prof. Kabudi anapoongea uwa nakuwa makini kutega sikio kuchota busara na hekima, hakika kwangu ni moja ya watu ambao sichoki kuwasikiliza. Kwa wengine inawezekana anaongea vitu vikubwa kuliko uelewa wao na wanashindwa kumuelewa lakini tunaomuelewa Prof. Kabudi hatuna mashaka na uchungu alionao juu ya kupotea kwa rasilimali za nchi hii. Ni mzalendo kwelikweli anayemsaidia kwa nguvu zote Rais wetu kulinda na kutunza rasilimali zetu dhidi ya mabeberu.
Siku ya jumamosi 23/11/2019, Prof.Kabudi katufundsha umuhimu wa utanzania wetu na hasa kuilinda Tanzania ili tuendelee kuitwa watanzania. Ni wachache sana wangemuelewa Mhe. Prof. Kabudi lakini ni ukweli pasina na shaka mtu huyu hachoki kukikumbusha kizazi hiki umuhimu wa Tanzania na jitihada zote zinazohitajika kuulinda utanzania. Prof. Kabudi anatukumbusha kuwa hakuna nchi utakayovinunia utanzania wako kama si Tanzania, leo kizazi za vijana wadogo kinashangilia utanzania wao unapoyumbishwa. Aibu kubwa sana hii.
Prof. Kabudi ni baba, mlezi na mwalimu; anatuelekeza, anatuasa na anatuonya popote pale anapopata fursa na muda wa kufanya hivyo. Kama mzazi, mlezi na mwalimu Prof. kabudi anatumia maneno ya Biblia kutoka kitabu cha Mithali 22:6 yanayosema “ mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee”. Prof. Kabudi ana jukumu la kutulea na kutukumbusha njia sahihi za kuulinda utanzania wetu ili nasi tuje kuwakumbusha vijana wetu. Vijana wanabeza njia hiyo wanataka kwenda njia wanayoiona wao, Prof. Kabudi hataki kuona hilo likitokea na matokeo ya hilo ni kuangamia kwa taifa.
Ukiachana na mapungufu ya kibinadamu aliyonayo Prof.Kabudi, hakika ni mzalendo wa kwelikweli na ana ujasiri mkubwa wa kusimamia rasilimali zetu bila kujali uhai wake, hakika vijana wa taifa hili wana mengi ya kujifunza kwa mtu huyu. Prof. Kabudi anahakikisha kila senti ya nchi hii inatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa na anajivunia utanzania wake kuliko chochote alichonacho, huu ni uzalendo wa kiwango cha juu sana.
Kardinali Pendo aliwahi kusema, namnukuu ‘ tunajiuliza baada ya Magufuli atakuwa nani ila mkiwepo wengi wa aina yako nisingekuwa na shaka ya kuwaza nani atafuata baada yake’, ni maneno aliyosema dhidi ya Makonda. Kwakuwa urais hautoki kwa mwanadamu, unatoka kwa Mungu nami naamini katika hao wengi waliosemwa na Kardinali Pengo wewe Prof. Kabudi ni mmojawapo. Nakutakia usaidizi mwema ya majukumu yako kwa Mkuu wa nchi.