Prof. Kabudi sasa kuongoza Vyombo vya Habari vya serikali kushinda propaganda / information war kuelekea 2025 na mbele zaidi

Prof. Kabudi sasa kuongoza Vyombo vya Habari vya serikali kushinda propaganda / information war kuelekea 2025 na mbele zaidi

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Uteuzi wa Profesa Palamagamba Kabudi, ni hatua nzito ya serikali kujipanga kushinda vita ya habari yaani propaganda.
1733669810370.jpeg

Vyombo kama TBC, TBC radio, Habari Leo Daily News, Idara ya Maelezo vimekuwa vikisinzia kuitetea serikali ya awamu ya 6 kiasi ya kuwa vyombo vya mitandao ya kijamii vimeibuka washindi katika kuunda sura (ku shape ) ya yanayoendelea nchi huku vyombo vya umma vikikosa wasikilizaji, wasomaji na wachangiaji (comments) iwe katika lugha ya KiSwahili au Kiingereza

Hivyo hatua ya uteuzi wa leo ni kujaribu kurudisha mizania kuegemea upande wa serikali na chama tawala au angalau kuweka mzania sawa balanced kutoka hali ya sasa ambapo vyombo vya habari vya umma vya kieletroniki, radio, televisheni vimeshindwa vita hii ya habari information war

Soma Pia: Rais Samia afanya uteuzi: Masauni apigwa chini Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Profesa Palamagamba Kabudi sasa kuendeleza propaganda :
Vita ya habari au information war ni zana muhimu kutetea uhalali wa maamuzi, matukio na mafanikio

USIPITWE TAZAMA KIPINDI AGENDA 2020 | MADA : FAIDA NA ATHARI ZA PROPAGANDA KWA TAIFA
  • White propaganda kutafuta heshima kupitia taarifa za kweli
  • Black propaganda chanzo hakitambuliki na pia taarifa siyo za kweli
  • Grey propaganda ipo katikati baina ya ukweli na uwongo

View: https://m.youtube.com/watch?v=OwLNl_fv_CY

Source : Star TV Habari
 
Juzi serikali ilijaribu kumpeleka Profesa Kitila Alexander Mkumbo katika mjadala mzito ya tathimini ya matokeo ya Uchaguzi 2024 uliosimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI na ikaonekana dhahiri serikali kushindwa kujieleza nini kimejiri

1733670805959.jpeg
 
Uteuzi wa Profesa Palamagamba Kabudi, ni hatua nzito ya serikali kujipanga kushinda vita ya habari yaani propaganda.
View attachment 3172343
Vyombo kama TBC, TBC radio, Habari Leo Daily News, Idara ya Maelezo vimekuwa vikisinzia kuitetea serikali ya awamu ya 6 kiasi ya kuwa vyombo vya mitandao ya kijamii vimeibuka washindi katika kuunda sura (ku shape ) ya yanayoendelea nchi huku vyombo vya umma vikikosa wasikilizaji, wasomaji na wachangiaji (comments) iwe katika lugha ya KiSwahili au Kiingereza

Hivyo hatua ya uteuzi wa leo ni kujaribu kurudisha mizania kuegemea upande wa serikali na chama tawala au angalau kuweka mzania sawa balanced kutoka hali ya sasa ambapo vyombo vya habari vya umma vya kieletroniki, radio, televisheni vimeshindwa vita hii ya habari information war

Soma Pia: Rais Samia afanya uteuzi: Masauni apigwa chini Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Profesa Palamagamba Kabudi sasa kuendeleza propaganda :
Vita ya habari au information war ni zana muhimu kutetea uhalali wa maamuzi, matukio na mafanikio

USIPITWE TAZAMA KIPINDI AGENDA 2020 | MADA : FAIDA NA ATHARI ZA PROPAGANDA KWA TAIFA
  • White propaganda kutafuta heshima kupitia taarifa za kweli
  • Black propaganda chanzo hakitambuliki na pia taarifa siyo za kweli
  • Grey propaganda ipo katikati baina ya ukweli na uwongo

View: https://m.youtube.com/watch?v=OwLNl_fv_CY

Source : Star TV Habari
 
Attachments

  • IMG_2374.jpeg
    IMG_2374.jpeg
    197.8 KB · Views: 7

Mimi nafikiri mama amecheza na Prof kama alivyotaka na prof kachezewa sana.
 
Profesa Palamagamba Kabudi kuongoza Wizara ya Ukweli - Wizara ya Habari Propaganda

Serikali ya CCM inahagaika sana kujisafisha baada ya uchafuzi uchaguzi TAMISEMI 2024. Hii inakumbusha kazi ya mtunzi wa riwaya George Orwell na kitabu chake maarufu duniani kiendacho kwa jina 1984 ambapo kuna wizara ya ukweli.

Mfano Ni nini kinashangaza kuhusu jina la Wizara ya Ukweli? (ya CCM) itakayowaleta waziri Kabudi, katibu mkuu SG balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, Mzee S.Wassira, Prof. Kitila Mkumbo, CPA Amos Makalla n.k kwenu wananchi wapenzi mubashara kila mara kupitia TBC ikijiunga na kituo huru cha Channel Ten siku ya jumapili usiku muda kuanzia saa 3 usiku kuzungumzia HAKI

Wizara kubwa na muhimu kupita zote ni Wizara ya Ukweli. Hapa ndipo Winston (kinara waziri Prof. Kabudi ) anafanya kazi.

Kinachoshangaza ni kwamba, Wizara ya Ukweli imejikita katika kuunda uwongo. Wafanyakazi katika idara ya Winston na kule mtaa wa Lumumba ofisi ndogo ya CCM kupitia UVCCM hutumia siku yao kubadilisha rekodi za kihistoria ili ziakisi chochote kinachotokea wakati huo, ikiwemo ya mwendazake aliyoiacha katika miradi ya vitu n.k .

Je, kazi ya Winston kada wa chama katika nukuu ya Wizara ya Ukweli ni ipi?

Winston anaenda kufanya kazi katika idara ya kumbukumbu ya Wizara ya Ukweli. Anakaa kwenye meza yake, akiangalia maandishi yake, mashine ambayo huandika kile anachozungumza ndani yake.

Kazi yake profesa itakijikita zaidi kusasisha taarifa zozote za maandishi ambazo zimethibitishwa kuwa si sahihi au zenye madhara kwa Chama - George Orwell 1984

Je, Wizara ya Ukweli inatumia msemo gani? Wizara ya Ukweli ina kauli mbiu tatu: "Vita ni Amani," "Uhuru ni Utumwa," na "Ujinga ni Nguvu." Mistari hii mitatu imeandikwa nje ya jengo ya Ofisi Ndogo ya Chama mtaa wa Lumumba . - George Orwell

George Orwell :

Je, ni nukuu gani kuhusu ukweli na uongo George Orwell 1984?
"Na ikiwa wengine wote walikubali uwongo ambao Chama kiliweka - ikiwa rekodi zote zilisema hadithi moja - basi uwongo huo ulipitishwa katika historia na kuwa ndiyo ukweli wote.

'Ni nani anayedhibiti yaliyopita' aliendesha kauli mbiu ya Chama, 'anadhibiti siku zijazo: ni nani anayedhibiti sasa anadhibiti yaliyopita. ni mwanazuoni mkubwa ...'” - George Orwell

'The Ministry of Truth: A Biography of George Orwell's "1984"
 
Toka maktaba :

Wasifu wa Profesa Palamagamba Kabudi, mtetezi wa mazoea, haamini katika mabadiliko ya kikatiba, ailinganisha Tanzania na Ujerumani

View: https://m.youtube.com/watch?v=cDkfy9jeEaU

Prof. Palamagamba Kabudi aliyesoma digrii yake ya Ph.D Ujerumani kwa miaka 7 na kuzaa baadhi ya watoto wake nchini Ujerumani anasema Ujerumani mpaka leo 2024 hawana Tume Ya Uchaguzi na kukumbushia kuwa Tanganyika mwaka 1958 hatukuwa na Tume ya Uchaguzi ...

Prof. Palamagamba Kabudi alipata kuwasimulia makada wa CCM wanafunzi chuo cha Mwalimu Nyerere Kigamboni DSM kuwa alianza kuandikia magazeti ya chama na serikali yaliyojikita katika propaganda ya kuisemea mazuri serikali kama mwandishi mwanafunzi, kabla ya kujiunga chuo kikuu cha DSM UDSM Mwaka 1980 hadi 1983 alipopata digrii ya kwanza ya sheria maarufu LLB.

Prof. Kabudi baadaye mwaka 1984 hadi 1986 alisomea digrii ya pili ya sheria LLM chuoni hapohapo UDSM . Ndipo akapata ufadhili kusoma Freie Universitãt mjini Berlin Ujerumani udokta wa sheria Juris Doctor.

TOKA MAKTABA:

TOKA MAKTABA :

Prof. Kabudi awachana waandishi " Hamna uwezo, nawaambia ukweli

View: https://m.youtube.com/watch?v=_2LDzddp-eQ
Prof. Kabudi - Nitawatembelea kuwapa somo kuhusu misimamo inayo sigana ili Tanzania isifike na kuonekana ..amesema leo August 21, 2019 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza na Wakuu na Wahariri Wakuu wa Vyombo vya habari, katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini DSM....
1733681708667.jpeg
 
Aliwahi kuwa mwenyekiti wa kamati ya uhariri Bodi ya Mwananchi ( MCL) kwa hiyo katika haya mambo yumo muda mrefu. Huku amepelekwa kwa kazi maalumu 'kuwakodolea macho' na 'kuwayumbisha' kina Chief Odemba,Kikeke katika mahojiano kuelekea jambo kuu la 2025
 
Kabudi na Mwakyembe professionally ni wanahabari, walikuwa katika propaganda enzi ya vita vya Idd Amin kabla ya kugeukia sheria
 
TOKA MAKTABA:

2019 10 Julai

Mahojiano moto
:FIRE: BBC

PROFESA KABUDI NA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA

View: https://m.youtube.com/watch?v=y_Rd6QiccgY
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi ametetea sifa ya uhuru wa vyombo vya habari vya nchi hiyo katika mahojiano na Zuhura Yunus kuhusu kufungiwa magazeti, kupewa karipio, maonyo .... kufungiwa leseni

Tanzania Daima gazeti la CHADEMA linaandika kwa uhuru kabisa ... soma gazeti la Uhuru la CCM ...
 
Wizara ya Habari, Michezo sasa kuzitumia Yanga na Simba vizuri kupitia waziri mpya Profesa Kabudi

Siku za karibuni tasnia ya habari kwa kiwango kikubwa imetumika na watawala kuduwaza waTanzania kwa kuwaelekeza muda wote kuzungumza, kuchambua, kutoa maoni kocha gani atimuliwe haraka n.k

Huku wananchi wakiacha kujadili hzbari za changamoto katika mazingira yao kama za kiuchumi, kijamii, kushirikishwa katika maamuzi, demokrasia, haki
 
Profesa Palamagamba Kabudi sasa kuendeleza propaganda :
Vita ya habari au information war ni zana muhimu kutetea uhalali wa maamuzi, matukio na mafanikio
Jinsi radio Tanzania ilivyotumika katika mapambano ya ukombozi :

Historia kutoka Afrika ya Kusini:

A Call to Action. Message over Radio Tanzania to the people of South Africa by O. R. Tambo, 26 June 1969​

Published date​

04/09/2017

Wito wa Kuchukua Hatua. Ujumbe kupitia Redio Tanzania kwa watu wa Afrika Kusini na Oliver R Tambo, 26 Juni 1969​

Tarehe iliyochapishwa​

04/09/2017

Makala hii Ilisahihishwa mara ya mwisho 05/09/2017​

Wito wa Kuchukua Hatua. Ujumbe kupitia Redio Tanzania kwa watu wa Afrika Kusini na OR Tambo, 26 Juni 1969

(Maandishi yaliyofupishwa)
Kwa zaidi ya miaka hamsini, chama cha African National Congress kimewaongoza watu wa Afrika Kusini katika harakati za kupigania uhuru.

Kwa zaidi ya miaka hamsini imekuwa upanga na ngao ya watu.

Chama cha African National Congress sasa kimewaita watu kwenye mapambano ya silaha, na sasa tuko vitani.

Tangu Agosti 1967, wapiganaji wetu jasiri, pamoja na ndugu zao wa Zimbabwe, wamekutana na risasi ya mkandamizaji kwa risasi nchini Zimbabwe, na wamemwona akikimbia. Hadithi ya ukuu wa wazungu imelipuka katika uwanja wa mapigano ya silaha. Wanajeshi wa Vorster na Smith wamefunzwa somo ambalo hawawezi kusahau kwa urahisi. Wanaogopa waasi wetu.

Lakini huu ni mwanzo tu. Bado watajua hasira ya watu ambao wameteseka kwa karne nyingi za ukandamizaji wa wazungu, na sasa wameazimia kuvunja minyororo ya utawala wa wazungu.

Tuko vitani. Lakini si peke yake. Nchini Msumbiji na Angola, ndugu zetu wanapigania kujikomboa kutoka kwa ugaidi wa utawala wa kikoloni wa Ureno na Ureno inapata pigo kali kutoka kwa watu wajasiri wa Guinea-Bissau huko Afrika Magharibi.

Nchini Namibia watu waliodhulumiwa wamechukua silaha dhidi ya wageni kutoka Pretoria. Nchini Zimbabwe, utawala wa Smith unaishi kwa muda ulioazimwa na kutegemea wanajeshi wa kizungu walioazima kutoka kwa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.

Kusini mwa Afrika yote iko katika moto - miali ya mapinduzi na uhuru.

Siku hii, Juni 26, tunatazama nyuma katika rekodi ya utawala wa wazungu katika nchi yetu.

Wadhalimu wameiba ardhi yetu, wametutoa katika nyumba zetu, wametufanya watumwa chini ya sheria zao za kupita.

Wanaishi kama mabwana juu ya utajiri wa nchi yetu na jasho la kazi yetu. Tunataabika kama watumwa na kuishi katika umaskini.

Maelfu kwa maelfu ya watoto wetu na vijana wetu wanakufa kwa njaa kila mwaka; wanawafukuza maelfu ya watu wetu kwenye jela zao kila wiki;

viongozi wetu wanafungwa maisha, wanauawa jela, wananyongwa; wana na binti zetu wajasiri waliteswa katika seli za polisi.

Hadithi nzima ya ukandamizaji wa wazungu ni hadithi ya mateso ya kikatili: Chifu Albert Luthuli - kifo chake cha kikatili bado hakijaelezewa. Caleb Mayekiso - nani alimuua jela? Wilson Khayinga, Vuyisile Mini na wengine - walinyongwa. Babla Saloojee, Looksmart Solwandle, Lenkoe na wengine - waliteswa hadi kufa. Simon Mkele, Sindile Ncaphayi, Marks, Florence Matomela na wengine - walikataliwa matibabu wakiwa jela na wamefariki dunia.

Mandela, Sisulu, Mbeki, Kathrada, Motsoaledi, Fischer, Goldberg, Steve Dlamini, Dorothy Nyembe, Lawrence Phokanoka, Lungephi Lengisi, na wengine wengi wanateseka kwenye kisiwa cha Robben, kwenye jela ya Pretoria, Baberton, Leeukop na kwingineko - majina haya yanatujaza. hasira na wanaandika adhabu ya utawala wa wazungu.

Hakuna mauaji, hakuna mauaji, hakuna kifungo, hakuna mateso ya watu wetu yanaweza kuokoa adui. Vorster, van den Bergh - bosi wa BOSS Bureau of State Security - Swanepoel na Tawi lake Maalum watashindwa.

Tayari wameshindwa kuiangamiza African National Congress. Wameshindwa kuwatiisha watu wetu au kuwafanya wakubali baaskap. Wanajeshi wao hawalingani na askari wa Umkhonto we Sizwe.

Wafuasi wao wachache wa wazungu hawawezi kupinga mamilioni ya watu wanaokandamizwa wakiwa na ujasiri katika mishipa yao, uamuzi katika mioyo yao, silaha mikononi mwao na sababu ya haki ya kupigania.

Tunatoa wito kwa watu wetu wote wanaodhulumiwa na wenzetu wote kuamka na kupigana na adui wa kawaida; kumwadhibu kwa makosa yake dhidi ya watu, kumshambulia kila mahali, kumsumbua, kutompa raha. Tunawaomba leo mjitoe tena kwa mapambano haya makubwa ya uhuru katika nchi yetu mama.

Tunawaita vijana wa taifa letu - vijana wetu wa kiume na wa kike, tunawaita watu wetu wanaotaabika - baba na mama zetu; tunatoa wito kwa wafanyakazi na vibarua mashambani; tunatoa wito kwa watu wetu wa Kihindi na Warangi, kwa Waafrika Kusini wote wenye fikra sahihi na wenye kuona mbali; tunatoa wito kwa nyinyi nyote kuchukua udhibiti wa mustakabali na hatima ya nchi yenu wenyewe - mustakabali wenu, hatima yenu ambayo imefafanuliwa katika Mkataba wa Uhuru.

Chini ya bendera ya African National Congress awamu ya mapinduzi ya mapambano ya silaha imeanza.

Umesikia milio ya risasi kutoka nje ya mipaka yetu nchini Zimbabwe. Siku lazima ifike ambapo itasikika katika marefu na mapana ya nchi yetu mama.
Kuwa tayari. Vita vitakuwa vya muda mrefu, ngumu na chungu. Lakini itaisha kwa ushindi kwetu na UHURU HATIMAYE!

Maatla ke Arona!

Amandla Ngawethu!

Power to the People!

Nguvu ni Haruni!
Nguvu Ni Yetu!
Nguvu kwa Wananchi

Source : A Call to Action. Message over Radio Tanzania to the people of South Africa by O. R. Tambo, 26 June 1969 | South African History Online
 
TOKA MAKTABA :

24 April 2019

Spika wa Bunge la Afrika ya Kusini Bi. Baleka Mbete akizungumzia ushawishi wa Radio Uhuru Dar es Salaam

SIMULIZI ZA KADA WA ANC KUELEKEA DAR ES SALAAM RADIO UHURU
Vifaa vya utangazaji vilivyotumiwa na Radio Uhuru wakati wa siku za giza za ubaguzi wa rangi vinakabidhiwa kwa Afrika Kusini katika Makumbusho ya Uhuru huko Pretoria. Kwa habari zaidi, tembelea: sabcnews.com

View: https://m.youtube.com/watch?v=3NkeDy_L8Hw
Jinsi kiongozi Oliver Reginald Tambo rais wa ANC alivyofika Radio Tanzania na kuwapa somo watangazaji pia kuwaonya wawe makini wasimshambulie kiongozi fulani, kwani utangazaji ni mkakati siyo tu kutekwa na umarufu na nguvu ya kuwa studio unaweza kusema lolote. Utangazaji ni zana muhimu kufikia malengo makuu hivyo maneno katika utangazaji yanaweza kutibua agenda kubwa iliyopangwa asema OR Tambo alivyofika radio Tanzania kuongea na vijana watangazaji wa ANC studio mjini Dar es Salaam ...anasimulia spika wa bunge la Afrika ya Kusini Bi. Baleka Mbete aliyepata kuwa mtangazaji kijana mdogo katika studio maalum Radio Tanzania walizopewa na serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais mwalimu Julius Nyerere ...

Kuanzia Angola na Msumbiji, hadi Namibia, Zimbabwe na Afrika Kusini, teknolojia mpya ya redio ilivipa vyama vya ukombozi vilivyokuwa uhamishoni jukwaa la kuwahutubia wafuasi wao nyumbani, kueneza itikadi zao na kukabiliana na propaganda za tawala dhalimu za wazungu wachache. Kama njia ya bei rahisi na ya moja kwa moja, redio za msituni zilivuka mipaka iliyowekwa na tawala za walowezi na zilisikilizwa sana, ingawa ndani ya uwanja wa uharamu.

Redio hizi kutoka maeneo yao ya utangazaji uhamishoni, mshikamano wa kimataifa, hadi mapokezi nyumbani ambapo wasikilizaji mara nyingi walikusanyika karibu na wapokeaji wao kusikiliza ujumbe kutoka kwa vyama vya ukombozi, mara nyingi zaidi ya macho ya jimbo. Redio hizi zilichagiza asili ya kampeni za upinzani ambazo vuguvugu la ukombozi lilianzisha katika nchi mbalimbali za kanda

Uhamisho: 1976-1990​

Akiwa uhamishoni kukimbia utawala wa kikaburu Afrika ya Kusini, Bi. Baleka Mbete alijiunga na chama cha African National Congress (ANC). Pia alifundisha katika shule ya upili ya Mbabane, Swaziland hadi 1977, alipohamia Dar es Salaam, Tanzania . [ 6 ] Jijini Dar es Salaam, alifanya kazi yake ya ANC kwa bidii, akijiunga na Idara ya Habari na Uenezi ya chama - haswa, alifanya kazi kwenye Radio Uhuru -kitengo cha Radio Tanzania Dar es Salaam pamoja na Sehemu. Mbete alikuwa katibu wa kanda wa Kanda ya Wanawake nchini Tanzania kuanzia 1978 hadi 1981.
 
21 December 2016

Uhusiano kati ya vyama vya upinzani na vyombo vya habari

Johannesburg, 21 Desemba 2016 - Kutana na Mwanahabari Eusebius Mckaiser yuko studio na Mbunge wa EFF Mbuyiseni Ndlozi na Mbunge wa DA Refiloe Ntsekhe wakijadili uhusiano kati ya vyama vya upinzani na vyombo vya habari.

View: https://m.youtube.com/watch?v=0Wp1Z7n9BSE
 
utangazaji ni mkakati siyo tu kutekwa na umarufu na nguvu ya kuwa studio unaweza kusema lolote. Utangazaji ni zana muhimu kufikia malengo makuu

Mkurugenzi wa TBC:

Happy Birthday Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayub Rioba Chacha​

1733754302239.jpeg
1733757779281.jpeg
 
Uteuzi wa Profesa Palamagamba Kabudi, ni hatua nzito ya serikali kujipanga kushinda vita ya habari yaani propaganda.
View attachment 3172343
Vyombo kama TBC, TBC radio, Habari Leo Daily News, Idara ya Maelezo vimekuwa vikisinzia kuitetea serikali ya awamu ya 6 kiasi ya kuwa vyombo vya mitandao ya kijamii vimeibuka washindi katika kuunda sura (ku shape ) ya yanayoendelea nchi huku vyombo vya umma vikikosa wasikilizaji, wasomaji na wachangiaji (comments) iwe katika lugha ya KiSwahili au Kiingereza

Hivyo hatua ya uteuzi wa leo ni kujaribu kurudisha mizania kuegemea upande wa serikali na chama tawala au angalau kuweka mzania sawa balanced kutoka hali ya sasa ambapo vyombo vya habari vya umma vya kieletroniki, radio, televisheni vimeshindwa vita hii ya habari information war

Soma Pia: Rais Samia afanya uteuzi: Masauni apigwa chini Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Profesa Palamagamba Kabudi sasa kuendeleza propaganda :
Vita ya habari au information war ni zana muhimu kutetea uhalali wa maamuzi, matukio na mafanikio

USIPITWE TAZAMA KIPINDI AGENDA 2020 | MADA : FAIDA NA ATHARI ZA PROPAGANDA KWA TAIFA
  • White propaganda kutafuta heshima kupitia taarifa za kweli
  • Black propaganda chanzo hakitambuliki na pia taarifa siyo za kweli
  • Grey propaganda ipo katikati baina ya ukweli na uwongo

View: https://m.youtube.com/watch?v=OwLNl_fv_CY

Source : Star TV Habari
 
Attachments

  • 1733756380754.png
    1733756380754.png
    392.1 KB · Views: 7
Back
Top Bottom