ally ngomanzito
Member
- Oct 7, 2015
- 86
- 108
Na John Marwa, Darmpya Blog
Mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Profesa Kitila Mkumbo, amewaahidi wafanyabiashara na wakazi wa kata ya Manzese kuwa ataboresha mazingira na miundombinu ya soko la Manzese ili wafanyabiashara wafanye kazi katika mazingira mazuri.
Profesa Mkumbo ameyasema hayo leo Jumatano Septemba 16, 2020 wakati akizungumza na wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Ukombozi katika kata ya Manzese wakati wa mkutano wa kampeni.
Profesa Mkumbo ameahidi kutatua kero zote zinazowakabili wafanyabiashara katika soko hilo ikiwemo kuweka mifumo thabiti na rafiki ya tozo kwa wafanyabiashara ili tozo watakazolipa ziwe na uwiano wa fedha wanazozipata.
Ameahidi pia akichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Ubungo, atahakikisha katika soko hilo kunakuwepo na sehemu maalum ya machinjio ili kulifanya soko kuwa safi kwa afya ya watumiaji wa soko hilo na wakazi wa maeneo jirani na wakati wote Lowe na madhari yenye kuvutia huku ikizingatiwa kuwa soko hilo ni miongoni mwa masoko makubwa kwa mkoa wa Dar es Salaam ambalo ni kiini cha uchumi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
Akizungumzia mikakati ya kumaliza changamoto za jumla katika masoko yaliyopo jimbo la Ubungo ambayo ni Soko la Manzese, soko la Mburahati, soko la Mahakama ya ndizi, soko la Big Brother na soko la Mawasiliano, Profesa Mkumbo amesema kwamba, ataweka program maalum ya kushughulikia kero zote masoko hayo ikiwemo urekebishaji wa tozo kwa wafanyabiashara kwa kuweka tozo ndogo na rafiki na hata kuondoa baadhi ya tozo sanjari na ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya masoko hayo.
Kwa upande wa miundombinu ya barabara katika kata ya Manzese na jimbo la Ubungo kwa ujumla, mgombea huyo wa ubunge amesema atapigania ili kuhakikisha kwamba, barabara zote za mitaani katika kata ya Manzese na jimbo la Ubungo kwa ujumla zinaingia katika Mradi wa Uendelezaji wa jiji la Dar es Salaam (DMDP) ambapo amesema matunda ya jitihada yameanza kuonekana kwani hadi sasa barabara nne zimeingizwa katika mpango huo ikiwemo barabara ya kutoka Kimara hadi Kinyerezi.
Vilevile Prof. Mkumbo ameapa kulishughulikia kikamilifu kero ya muda mrefu ya wananchi wanaodai fidia kwa kupisha ujenzi wa kingo za Mto Ng'ombe na kuhakikisha kwamba wanalipwa fedha zao na kuongeza kuwa, suala la ulipaji limeanza kushughulikiwa na liko katika hatua za mwisho kufanikiwa na endapo wananchi wa jimbo la Ubungo wamkichagua atalifanikisha hilo.
Mbali na hayo, Profesa Mkumbo amewataka wananchi wote wa jimbo la Ubungo kuwahoji wale waliopewa dhamana katika kuongoza halmashauri ya Manispaa ya Ubungo walifanya nini ikiwa kero ikiwemo kero ya miundombinu mibovu ya barabara za mitaani pamoja na kero za vyoo na miundombinu mibovu ya masoko ya jimbo hilo kuendelea kuwepo, licha ya kuongoza halmashauri kwa wakati huo huku wakikusanya zaidi ya shilingi bilioni 25 kwa mwezi sawa na shilingi bilioni 125 kwa kipindi cha miaka mitano walizokusanya kama kodi kwenye Halmashauri yetu.
Profesa Mkumbo, amewasisitiza wananchi wa jimbo la Ubungo kumchagua yeye kwa kuwa anafahamu maana ya uongozi katika utumishi wa nafasi ya bunge akiahidi kuwa atakuwa kiongozi kiungo kati ya wananchi na serikali, pia atakuwa ni kuongozi mlezi kwa wananchi wote pamoja na kuwa kiongozi jasiri na mwenye ushawishi kwa viongozi wakuu kwamba, keki itakayopatikana hata kama ndogo basi wananchi wa jimbo la Ubungo itawafikia.
Aidha, Profesa Mkumbo ametumia hadhara hiyo kumuombea kura Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akisema kuwa hata kama wananchi hawatoona mazuri yake lukuki kwa taifa basi watizame suala moja tu la namna alivyolishughulikia suala la Corona vizuri hadi sasa nchi ikiwa salama huku mataifa mengine yakiendelea kuteseka na ugonjwa huo, pia amewaomba wananchi wa kata ya Manzese kumchagua Manumbu Magafu ili kwa umoja wao wawaletee maendeleo wanachi wa kata hiyo, Jimbo la Ubungo na tuafa kwa ujumla.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa kitaifa wa Jumuiya za chama hicho akiwe Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Queen Mlozi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mwl. Raymond Mwangala na viongozi wa chama katika Wilaya ya Ubungo