Nafikiri alichosema profesa hamjamuelewa.
Yeye alitaka ifanyike HR Audit ambayo kimsingi huwa inafanywa ili kujua majukumu yaliyopo na idadi ya watumishi inayotakiwa.
Bila kufanya hili Serikali inaweza kuajiri na kujikuta inawatumishi wengi kuliko kazi zilizopo.
Kwa mfano, Chuo Kikuu Huria Tanzania kina maafisa Rasilimali watu na Utawala zaidi ya kumi lkn utakuta wamewekwa kwenye vitivo ila kazi zote za kiHr zinafanywa centrally na wa kwenye vitivo kubaki bila cha maana cha kufanya na kufanya kazi ambazo Sektratari angepaswa kufanya.
Audit ingetuonyesha wapi kuna watumishi wengi ambao hawatumiki ipasavyo na hivyo kusaidia kufanya uamuzi hata wa kuwarelocate wengine.
Si vema km hufahamu jambo usimshambulie mtu tulia wenye ujuzi waje wakuelimishe.