Prof. Kitila Mkumbo: Wapinzani Wanauza Malalamiko, CCM inauza Mafanikio

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
My Take
Wapinzani wa Tanzania ni uchwara na hawajitambui .
👇👇

"Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetekeleza miradi mingi ya maendeleo hasa kwenye Jimbo letu la Ubungo ndio sababu tunasema wapinzani wanauza malalamiko lakini sisi CCM tunauza mafanikio" Prof. Kitila Mkumbo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo.

Naunga mkono hoja,kazi iendelee 👇👇

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) William Lukuvi ametembelea Mradi wa Maji Mshikamano uliopo Kata ya Mbezi, Wilaya ya Ubungo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Ubungo ambapo amemshukuru na kumpongeza Raisi Samia kwa kumaliza kwa kiasi kikubwa chagamoto ya huduma ya maji wilaya ya Ubungo.

Waziri Lukuvi amesema Mradi wa Maji wa Mshikamano ni moja ya miradi ya kimkakati iliyolenga kuleta ahueni kwa wakazi wa Kata ya Mbezi ambao wamekuwa na changamoto ya maji kwa mda mrefu.

“Kwa wale wanayoifahamu Ubungo ya enzi hizo hali ya upatikanaji wa maji ilikuwa ya shida sana lakini kupitia mradi huu wananchi wanapata nafuu, itoshe kusema Rais hadaiwi na Wanaubungo, changamoto zipo haziwezi kukosekana, DAWASA (Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam) ndiyo wakati wenu kuhakikisha mnazifanyia kazi wananchi wapate maji” amesema Waziri Lukuvi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hassan Bomboko amesema hali ya upatikanaji wa maji kwa wilaya ya Ubungo ni ya kuridhisha maeneo mengi na hayo ni matunda ya uwekezaji uliofanywa na serikali ya awamu ya sita, na kwa maeneo machache ambayo huduma ya maji ina changamoto, DAWASA wanatoa ushirikiano katika kuhakikisha changamoto zinafanyiwa kazi.

“Wananchi zaidi ya 200,000 wananufaika kupitia mradi huu, malalamiko yamepungua kwa hali ya juu, kwa maeneo ambayo bado huduma haijatengemaa tunashirikiana na DAWASA kuhakikisha huduma inapatikana na kazi iliyobaki ni kufikisha huduma kwa wananchi zaidi” amesema Bomboko.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA amesema Mradi wa Mshikamano ni moja ya miradi ya kimkakati iliyolenga kutatua changamoto ya maji kwa wakazi zaidi wa 200,000 wa Kata ya Mbezi, Mshikamano, Msakuzi, Mpiji- Magoe, Machimbo na Majengo Mapya ambapo mradi umekamilika na unaendelea kutoa kutoa huduma kwa wanufaika.
 
My Take
Wapinzani wa Tanzania ni uchwara na hawajitambui .
👇👇

"Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetekeleza miradi mingi ya maendeleo hasa kwenye Jimbo letu la Ubungo ndio sababu tunasema wapinzani wanauza malalamiko lakini sisi CCM tunauza mafanikio" Prof. Kitila Mkumbo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo.

Naunga mkono hoja,kazi iendelee 👇👇

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) William Lukuvi ametembelea Mradi wa Maji Mshikamano uliopo Kata ya Mbezi, Wilaya ya Ubungo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Ubungo ambapo amemshukuru na kumpongeza Raisi Samia kwa kumaliza kwa kiasi kikubwa chagamoto ya huduma ya maji wilaya ya Ubungo.

Waziri Lukuvi amesema Mradi wa Maji wa Mshikamano ni moja ya miradi ya kimkakati iliyolenga kuleta ahueni kwa wakazi wa Kata ya Mbezi ambao wamekuwa na changamoto ya maji kwa mda mrefu.

“Kwa wale wanayoifahamu Ubungo ya enzi hizo hali ya upatikanaji wa maji ilikuwa ya shida sana lakini kupitia mradi huu wananchi wanapata nafuu, itoshe kusema Rais hadaiwi na Wanaubungo, changamoto zipo haziwezi kukosekana, DAWASA (Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam) ndiyo wakati wenu kuhakikisha mnazifanyia kazi wananchi wapate maji” amesema Waziri Lukuvi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hassan Bomboko amesema hali ya upatikanaji wa maji kwa wilaya ya Ubungo ni ya kuridhisha maeneo mengi na hayo ni matunda ya uwekezaji uliofanywa na serikali ya awamu ya sita, na kwa maeneo machache ambayo huduma ya maji ina changamoto, DAWASA wanatoa ushirikiano katika kuhakikisha changamoto zinafanyiwa kazi.

“Wananchi zaidi ya 200,000 wananufaika kupitia mradi huu, malalamiko yamepungua kwa hali ya juu, kwa maeneo ambayo bado huduma haijatengemaa tunashirikiana na DAWASA kuhakikisha huduma inapatikana na kazi iliyobaki ni kufikisha huduma kwa wananchi zaidi” amesema Bomboko.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA amesema Mradi wa Mshikamano ni moja ya miradi ya kimkakati iliyolenga kutatua changamoto ya maji kwa wakazi zaidi wa 200,000 wa Kata ya Mbezi, Mshikamano, Msakuzi, Mpiji- Magoe, Machimbo na Majengo Mapya ambapo mradi umekamilika na unaendelea kutoa kutoa huduma kwa wanufaik
 
Back
Top Bottom