CUF Habari
JF-Expert Member
- Dec 12, 2019
- 239
- 234
MULEBA KAGERA
Nchi yetu imejaa ufisadi, ubinafsi, migawanyiko, kuumizana, ubaguzi, kutokuaminiana, chuki, kukata tamaa na huzuni.
Haya ni majera hayanayohitaji kutibiwa na kuwarejeshea wananchi matumaini.
Tumefikia hapa tulipo kutokana na Tanzania kukosa taasisi imara za kusimamia uendeshaji wake.
Taasisi zilizoko uimara wake ni wa kinadharia kuliko wa uhalisia. Katika mazimgira haya mustakabali wa nchi umekuwa ukitegemea zaidi haiiba na matakwa ya rais aliyeko madarakani kuliko taratibu za kitaasisi.
CUF inataka nchi iwe na taasisi imara zinazounda mfumo madhubuti ambao utahakikisha kuwa nchi iko salama bila kujali ni chama gani kiko kwenye nadaraka.
Kuunda mfumo huu kunahitaji nguvu ya pamoja na ushirikishwaji wa kila Mtanzania.
Kwa sababu hii CUF inapendekeza serikali ya umoja wa kitaifa. Serikali hii jumuishi itakuwa na jukumu la kujenga mfumo unaohitajika.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa chini ya CUF itaweka misingi ya kuhakikisha kuwa taifa linakuwa na Demokrasia ya kweli.
Serikali ya umoja wa kitaifa itakamilisha mchakato wa kupata katiba mpya yenye misingi imara ya demokrasia na utawala bora.
Katiba ambayo pamoja na mambo mengine itatenganisha kikamilifu mamlaka na nguvu za mihimili mbalimbali, italinda misingi ya ushindani wa kisiasa, itapanua na kukuza haki za kiraia, na itahakikisha uwepo wa uhuru wa kutosha wa vyombo vya habari na fursa ya
kujieleza.
Tunahitaji kuwa na katiba nzuri inayompa kila Mtanzania uhuru wa kweli wa kuchagua na au kuchaguliwa.
Tunahitaji kuwa na Muungano wa Watanganyika na Wazanzibari usio na mashaka ndani yake kwa pande zote mbili.