Uchaguzi 2020 Prof.Lipumba akiwa Ushetu, Shinyanga: Nichagueni Oktoba 28, niwe Rais nitaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Uchaguzi 2020 Prof.Lipumba akiwa Ushetu, Shinyanga: Nichagueni Oktoba 28, niwe Rais nitaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
IMG_20200929_184931_521.jpg


NICHAGUENI OKTOBA 28,NIWE RAIS NIUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA " PROF.LIPUMBA"

USHETU, SHINYANGA.

Nchi yetu imejaa ufisadi, ubinafsi, migawanyiko, kuumizana, ubaguzi, kutokuaminiana, chuki, kukata tamaa na huzuni. Haya ni majeraha
yanayohitaji kutibiwa na kuwarejeshea wananchi matumaini. Tumefikia hapa tulipo kutokana na Tanzania kukosa taasisi imara za kusimamia uendeshaji wake. Taasisi zilizoko uimara wake ni wa kinadharia kuliko wa uhalisia.

Katika mazingira haya mustakabali wa nchi umekuwa ukitegemea Zaidi haiiba na matakwa ya rais aliyeko madarakani kuliko taratibu za kitaasisi. CUF inataka nchi iwe na taasisi imara zinazounda mfumo madhubuti ambao utahakikisha kuwa nchi iko salama bila kujali ni chama gani kiko kwenye madaraka.

Kuunda mfumo huu kunahitaji nguvu ya pamoja na ushirikishwaji wa kila Mtanzania. Kwa sababu hii CUF inapendekeza serikali ya umoja wa kitaifa. Serikali hii jumuishi itakuwa na jukumu la kujenga mfumo unaohitajika. Serikali ya Umoja wa Kitaifa chini ya CUF itaweka misingi ya kuhakikisha kuwa taifa linakuwa na Demokrasia ya kweli. Serikali ya umoja wa kitaifa itakamilisha mchakato wa kupata katiba mpya yenye misingi imara ya demokrasia na utawala bora. Katiba ambayo pamoja na mambo mengine itatenganisha kikamilifu mamlaka na nguvu za mihimili mbalimbali, italinda misingi ya ushindani wa kisiasa, itapanua na kukuza haki za kiraia, na itahakikisha uwepo wa uhuru wa kutosha wa vyombo vya habari na fursa ya kujieleza.

Tunahitaji kuwa na katiba nzuri inayompa kila Mtanzania uhuru wa kweli wa kuchagua na au kuchaguliwa. Tunahitaji kuwa na Muungano wa Watanganyika na Wazanzibari usio na mashaka ndani yake kwa pande zote mbili. Tunahitaji Umoja wa Kitaifa wa kweli ambapo ubaguzi wa aina yoyote iwe ni wa jinsia, rangi, dini au ulemavu utakuwa ni jinai inayoadhibiwa kwamujibu wa sheria. Aidha tunahitaji kuwa na katiba inayojilinda isivunjwe na wanasiasa walioko madarakani kwa ajili ya maslahi yao binafsi na maslahi ya
makundi wanayoyashabikia.

Katiba ya sasa haikidhi vigezo vinavyohitajika ili kuchochea maendeleo ya demokrasia nchini mwetu. Chini ya Sera za HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE, serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itaandaa utaratibu unaofaa wa kupata Katiba Mpya ya wananchi.
 
View attachment 1584697NICHAGUENI OKTOBA 28,NIWE RAIS NIUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA " PROF.LIPUMBA"

USHETU, SHINYANGA.

Nchi yetu imejaa ufisadi, ubinafsi, migawanyiko, kuumizana, ubaguzi,
kutokuaminiana, chuki, kukata tamaa na huzuni. Haya ni majeraha
yanayohitaji kutibiwa na kuwarejeshea wananchi matumaini. Tumefikia hapa
tulipo kutokana na Tanzania kukosa taasisi imara za kusimamia uendeshaji
wake. Taasisi zilizoko uimara wake ni wa kinadharia kuliko wa uhalisia.
Katika mazimgira haya mustakabali wa nchi umekuwa ukitegemea zaidi
haiiba na matakwa ya rais aliyeko madarakani kuliko taratibu za kitaasisi.
CUF inataka nchi iwe na taasisi imara zinazounda mfumo madhubuti ambao
utahakikisha kuwa nchi iko salama bila kujali ni chama gani kiko kwenye
nadaraka.
Kuunda mfumo huu kunahitaji nguvu ya pamoja na ushirikishwaji wa kila
Mtanzania. Kwa sababu hii CUF inapendekeza serikali ya umoja wa kitaifa.
Serikali hii jumuishi itakuwa na jukumu la kujenga mfumo unaohitajika.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa chini ya CUF itaweka misingi ya kuhakikisha
kuwa taifa linakuwa na Demokrasia ya kweli. Serikali ya umoja wa kitaifa
itakamilisha mchakato wa kupata katiba mpya yenye misingi imara ya
demokrasia na utawala bora. Katiba ambayo pamoja na mambo mengine
itatenganisha kikamilifu mamlaka na nguvu za mihimili mbalimbali, italinda
misingi ya ushindani wa kisiasa, itapanua na kukuza haki za kiraia, na
itahakikisha uwepo wa uhuru wa kutosha wa vyombo vya habari na fursa ya
kujieleza.
Tunahitaji kuwa na katiba nzuri inayompa kila Mtanzania uhuru wa kweli wa
kuchagua na au kuchaguliwa. Tunahitaji kuwa na Muungano wa
Watanganyika na Wazanzibari usio na mashaka ndani yake kwa pande zote
mbili. Tunahitaji Umoja wa Kitaifa wa kweli ambapo ubaguzi wa aina yoyote
iwe ni wa jinsia, rangi, dini au ulemavu utakuwa ni jinai inayoadhibiwa kwamujibu wa sheria. Aidha tunahitaji kuwa na katiba inayojilinda isivunjwe na
wanasiasa walioko madarakani kwa ajili ya maslahi yao binafsi na maslahi ya
makundi wanayoyashabikia.
Katiba ya sasa haikidhi vigezo vinavyohitajika ili kuchochea maendeleo ya
demokrasia nchini mwetu. Chini ya Sera za HAKI SAWA NA FURAHA KWA
WOTE, serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itaandaa utaratibu unaofaa
wa kupata Katiba Mpya ya wananchi.
Tupe dondoo kwanza wewe Lipumba na Maalim Seif Sharif Hamad nini kilitokea ili tujue unafaa kupewa nchi ama la!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom