CUF Habari
JF-Expert Member
- Dec 12, 2019
- 239
- 234
Mwenyekiti wa CUF- Chama Cha Wananchi Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, kwa kutumia Mamlaka ya Kikatiba, amemsimamisha Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mhe. Faki Suleiman Khatib katika kutekeleza Agizo la Baraza Kuu la kuondoa Mapungufu na Kuimarisha Kamati Tendaji. Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar itajazwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linalotarajiwa kuketi mwishoni mwa mwezi huu.
Aidha Mwenyekiti amemteua Mhe. Nadhira Ali Haji kuwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Haroub Mohammed Shamis.
Mwenyekiti ameyafanya hayo asubuhi ya leo huko Zanzibar kwenye Ziara fupi ya kumtambulisha Katibu Mkuu Mpya na kushughulikia Maagizo aliyopewa na Baraza Kuu lililoketi wiki iliyopita Ukumbi wa Shaaban Khamis Mloo, Dar es Salaam.