Prof. Lipumba: Haingii akilini gaidi na mhaini akapelekewa salamu za rambirambi tarehe 8 Julai 2021 na Rais ambaye ana taarifa zote za usalama wa nchi

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba asema Haingii akilini gaidi na mhaini akapelekewa salamu za rambirambi tarehe 8 Julai 2021 na Rais ambaye ni amiri jeshi Mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, halafu tarehe 23 Julai 2021 Freeman Mbowe akakamatwe kwa ugaidi wa mwaka 2020.

Maana rais kila siku hupewa taarifa za usalama za nchi nzima, iweje tarehe 8 Julai 2021 Freeman Mbowe apelekewe salamu za pole za rambirambi za msiba wa kaka yake. Ina maana rais alikuwa hana taarifa za ugaidi wa Freeman Mbowe mpaka tarehe 21 Julai 2021 siku ya kongamano la CHADEMA juu ya katiba ya nchi, anahoji Prof. Haruna Lipumba.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba anakwenda mbali na kuhoji kuwa haiwezekani vyombo vya ulinzi na usalama kutomfahamisha Rais juu ya mipango ya kuwakamata watuhumiwa wa mipango ya ugaidi wa kulipua sehemu mbalimbali, njama za kuua viongozi na kufanya uhaini za mtuhumiwa Freeman Mbowe kiasi rais atatuma pole kwa mtu Mwenye kutuhumiwa nzito ambaye yupo mbioni kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka mazito ya ugaidi na uhaini.
 
7 August 2021

PROF: LIPUMBA AMZUNGUMZIA MBOWE KUHUSU SUALA LA UGAIDI.

Source : StarTV Habari
 
Mnaikumbuka hii🤣👇
images (1) (9).jpeg
 
Lipumba kuna wakati akili zinamrudia wakati mwingine zinafyatuka tena.

Hapa profesa ameuliza swali fikirishi sana.

Je rais wa awamu ya sita ananyimwa taarifa za kiintelejensia na wakuu wa vyombo vya usalama.

Nini dhima ya kumuweka gizani rais taarifa za kigaidi zilizo na muda unaokaribia mwaka, ndiyo amekuwa rais siku 100 zilizopita kwanini hawakumpatia taarifa nyeti kama hizi ktk kipindi chote za siku 100 baada ya kuwa rais na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Tanzania
 
Lipumba aunge mkono juhudi.Amekiuwa chama cha CUF kwa tamaa ya fedha
 
Hapa profesa ameuliza swali fikirishi sana.

Je rais wa awamu ya sita ananyimwa taarifa za kiintelejensia na wakuu wa vyombo vya usalama.

Nini dhima ya kumuweka gizani rais taarifa za kigaidi zilizo na muda unaokaribia mwaka, ndiyo amekuwa rais siku 100 zilizopita kwanini hawakumpatia taarifa nyeti kama hizi ktk kipindi chote za siku 100 baada ya kuwa rais na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Tanzania
Hapa kuna mawili.

1. Inawezekana kweli ananyimwa taarifa kama alivyonyimwa zile za kifo cha mwendazake then akapangiwa ziara ya Morogoro.

au

2. Rais nae anaujua ukweli, hii habari ya ugaidi wa Mbowe ni ya kutunga kwa lengo la kuyalinda maslahi ya CCM, ubaya wa hili ni kwamba siku wakishindwa kesi mahakamani Rais ataubeba mzigo wa aibu za kumuonea Mbowe,

Hili litazidi kuharibu mahusiano yake na Chadema na kuvuruga ile mipango ya Rais kuonana na wapinzani, hii inaweza kusababisha kuendelea hali ya kutoaminiana baina yao na mwishowe kuendeleza siasa za kuwindana kama tuzionazo sasa.
 
Lipumba huyu huyu msaliti pia yeye ....swali zuri fikirishi na tunayajua yote humo ndani mama hawamuheshimu kivile .....wanaona rahisi mpitaji tu lolote lawezekana
 
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba asema Haingii akilini gaidi na mhaini akapelekewa salamu za rambirambi tarehe 8 Julai 2021 na Rais ambaye ni amiri jeshi Mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, halafu tarehe 23 Julai 2021 Freeman Mbowe akakamatwe kwa ugaidi wa mwaka 2020.

Maana rais kila siku hupewa taarifa za usalama za nchi nzima, iweje tarehe 8 Julai 2021 Freeman Mbowe apelekewe salamu za pole za rambirambi za msiba wa kaka yake. Ina maana rais alikuwa hana taarifa za ugaidi wa Freeman Mbowe mpaka tarehe 21 Julai 2021 siku ya kongamano la CHADEMA juu ya katiba ya nchi, anahoji Prof. Haruna Lipumba.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba anakwenda mbali na kuhoji kuwa haiwezekani vyombo vya ulinzi na usalama kutomfahamisha Rais juu ya mipango ya kuwakamata watuhumiwa wa mipango ya ugaidi wa kulipua sehemu mbalimbali, njama za kuua viongozi na kufanya uhaini za mtuhumiwa Freeman Mbowe kiasi rais atatuma pole kwa mtu Mwenye kutuhumiwa nzito ambaye yupo mbioni kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka mazito ya ugaidi na uhaini.
MAMBO ya AJABU na YA AIBU yako TANZANIA
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom