Prof. Lipumba: Haingii akilini gaidi na mhaini akapelekewa salamu za rambirambi tarehe 8 Julai 2021 na Rais ambaye ana taarifa zote za usalama wa nchi

Mh Mbowe ni mhanga wa utawala usio fuata sheria. Kuna watu wanafaidika na mfumo huo, ndio watoa hoja ya katiba si lipa umbele cha wananchi. Katiba ni mkataba wa mtawala na mtawaliwa, lakini leo serikali imekuwa msemaji wa mwananchi kuhusu mahitaji ya katiba. Rasilimali za nchi zinatapanywa. Magufuli anatumbukiza hela kuhamia Dodoma, anakuja Samia anasema haiwezekani ikulu kuwa huko, mambo yote ni Dar.
 
Reactions: BAK
Kwani wenye tuhuma mbalimbali hawafiwi?Kumpa mtu pole haimaanishi hana tuhuma
 
Ukweli ni kwamba mama anashurutishwa na jeshi kuua upinzani!!mama anashangaa tu mambo yanayofanyika!!!ETI MBOWE NA TUHUMA ZA UGAIDI ZA 2020 JE UNADHANI MWENDAZAKE ANGEMUACHA KWELI?IKIWA LEMA ALIPOTEZWA KWA MIEZI MINNE KWA KUOTA NDOTO??!!!!LIPUMBA KAPATIA!!!
 
Namba 2 hapo inawezekana pia alipewa taarifa ila alijiona na kuwaza kuwa yeye ni mwenyekiti wa CCM badala ya kulichukua kama Amiri Jeshi na Rais wa JMT.Akiruhusu uzito wa cheo cha Mwenyekiti wa chama cha magaidi ukawa zaidi ya Urais wa JMT,Rais SSH atapata wakati mgumu sana.
Salama ya Mh.Samia ni kuruhusu Mchakato wa Katiba ya JMT uanze haraka sana kuanzia pale alipoishia Mh.Jaji Warioba na Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoiongoza.
Tunamkumbusha Mh.Rais"Watanzania siyo wajinga" na mwisho wa mtifuano huu Wananchi lazima wapate Katiba yao!
 
Huyu anaemhoji Profesa anawaiga mno wenzake wa BBC na CNN. Ingekuwa vyema zaidi kama angepunguza kumkatishakatisha. Wengine tungependa kumsikia Profesa kuliko yeye.

Amandla...
 
Reactions: BAK
Issue ya Mbowe ata kama hauna akili utajua tu ni kesi ya kubumba.

Alietunga hii kesi ya Mbowe ningekuwa Rais ningemfukuza kazi, amemdharirisha Rais kwa kutengeneza movie hafifu ambayo ata vipofu sasa wanaona.
 
Issue ya Mbowe ata kama hauna akili utajua tu ni kesi ya kubumba.

Alietunga hii kesi ya Mbowe ningekuwa Rais ningemfukuza kazi, amemdharirisha Rais kwa kutengeneza movie hafifu ambayo ata vipofu sasa wanaona.
Most likely ni Sirro,ulitegemea atengeneze movie yenye maana?
 
Usaliti wa Lipumba ni upi?
Umesahau mara hii......alijiuzulu akawakimbia wenzake akanunuliwa akarudishwa kwa nguvu za dola akaue CuF......ruzuku akalamba zote......malizia sasa leo anasema nini ? Nani ana trust ? Labda kina buku 7 nyie
 
Rais Samia anakoleza moto kuligawa Taifa...Mama utajengaje uchumi wa nchi wakati wana familia hawapo pamoja? Unazidi kuwagawa ...lazima utakwama tu.

Hata familia husonga mbele kimaendeleo kama baba, mama na watoto pamoja na dada wa kazi wote ni wamoja.
 
Polisi ya Tanzania imekuwa hovyo kabisa Siro awajibishwe!
 
Reactions: BAK

Aliyesema:

".. but you can't fool all the people all the time."

Kwa hakika hakukosea.
 
Reactions: BAK

Mwache aendelee kulitafuta
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…