Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba (Ndala Nzega Vijijini): Tunahitaji Kuboresha Sekta Muhimu Za Uchumi Na Kilimo

Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba (Ndala Nzega Vijijini): Tunahitaji Kuboresha Sekta Muhimu Za Uchumi Na Kilimo

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
Screenshot_20200917-175952.png


TUNAHITAJI KUBORESHA SEKTA MUHIMU ZA UCHUMI NA KILIMO."PROF.LIPUMBA" NDALA NZEGA VIJIJINI

Historia ya maendeleo ya uchumi duniani inaonesha kuwa maendeleo ya viwanda hutanguliwa au kuambatana na mapinduzi
ya kilimo.

Ongezeko la uzalishaji na tija katika sekta ya kilimo huongeza upatikanaji wa chakula na kupunguza gharama yake na kuruhusu wananchi kuhama toka vijijini na kwenda majini kufanya kazi za viwandani.

Kilimo kinazalisha malighafi inayotumiwa na viwanda vinavyosindika nafaka, mbegu za mafuta, matunda, nyama na maziwa.

Viwanda vya nguo na bidhaa za Ngozi hutumia malighafi inayozalishwa na sekta ya kilimo na ufugaji kama vile pamba na ngozi.

Pato la wakulima linapoongezeka linakuza soko la bidhaa za viwandani - nguo na mavazi, viatu, sukari, samani na vifaa vya matumizi ya nyumbani.

Soko kubwa la ndani la bidhaa hizi huwezesha kuanzishwa kwa viwanda vyenye uwezo mkubwa na gharama za wastani za chini na kuvifanya viwanda hivyo kuweza kushindana na bidhaa za kutoka nje, na hata kuweza kuuza nje ya nchi.

Kuongezeka kwa mapato ya wakulima huongeza uwekaji wa akiba ambayo inaweza kutumiwa kuwekeza katika viwanda.

Mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya nchi hulipatia taifa fedha za kigeni za kuagizia mashine, vipuri na malighafi kutoka nje ya nchi.

Utafiti katika nchi nyingi zinazoendelea unaonesha kuwa kasi ya kukua kwa tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo kunapunguza
umaskini kwa kasi kubwa kuliko ukuaji wa sekta nyingine yeyote.
 
Hiyo picha uliyoweka ni ya uwongo mkutano wa lipumba kwa sasa haufikishi watu ishirini. Amejimaliza kisiasa kwa tamaa ya pesa alizohongwa na ccm ili kuimaliza Chadema matokeo yake kaishia kujimaliza mwenyewe.
 
Back
Top Bottom