Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Nitajenga zahanati kila kijiji, vituo vya afya katika kila kata ili tutoe huduma bora ya afya na kudhibiti vifo vya wajawazito

Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Nitajenga zahanati kila kijiji, vituo vya afya katika kila kata ili tutoe huduma bora ya afya na kudhibiti vifo vya wajawazito

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
Screenshot_20201015-163923.png


NJOMBE- MAKAMBAKO
Nitahakikisha kuwa Bajeti ya Wizara ya Afya inapanda na kufikia asilimia 15 ya Bajeti ndani ya miaka 10 ijayo.

Ongezeko la bajeti litawezesha katika kuandaa miundombinu ya kisasa, wataalam, vifaa tiba na vipimo vya kutosha kwa maradhi yote.

Aidha ongezeko la bajeti litawezesha kutenga fungu maalum kwa ajili ya kukabili maradhi ya milipuko kama COVID-19 kwa kadri yatakavyojitokeza.

Ili kuhakikisha kuwa kila raia ana haki na anapata huduma za msingi za afya, Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF
itahakikisha asilimia 70 ya Watanzania wote wana Bima ya Afya ifikapo 2025 na asilimia 100 ifikapo 2028.

Hatua maalumu zitachukuliwa kuhakikisha kuwa huduma za uzazi bila malipo zinapatikana kwa kila mama mjamzito ili kupunguza vifo vingi vinavyotokea ambavyo vinadhibitika.
 
Back
Top Bottom