Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Nitatumia elimu yangu kukuza uchumi na kufuta umasikini katika nyanja zote

Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Nitatumia elimu yangu kukuza uchumi na kufuta umasikini katika nyanja zote

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
Screenshot_20201002-170701.png

BUSEGA- SIMIYU

Ukuaji wa uchumi wa Tanzania haujaambatana na kasi kubwa ya kupungua kwa watu masikini. Idadi ya watu masikini kwa kutumia kipimo cha taifa cha umasikini (mtu mzima kutumia shilingi 50,000/ au zaidi kwa mwezi) imeongezeka toka watu milioni 12.3 mwaka 2011 na kufikia watu milioni 14 mwaka 2018. Kwa kutumia kipimo cha kimataifa cha umaskini, Watanzania zaidi ya milioni 27 ni masikini.

Utafiti uliofanywa na serikali mwaka 2016 kuhusu umaskini wa watoto (Child Poverty in Tanzania) ulibaini kuwa asilimia 74 ya watoto wa Tanzania wanaishi katika mazingira ya umaskini kwa tafsiri pana inayojumuisha lishe, afya, hifadhi iliyo salama, elimu, mazingira, maji na makazi.
 
Yule mzee wa ubwabwa mbona hana coverage? Huyu mtu wenu ni Pro-pesa Lipumbaf
 
mtu aliyezaliwa mwaka 1995 tangu mzee anaanza kuomba urais.. ana miaka 25. sasa..
 
Kama elimu yako haikukusaidia kukuepusha na kadhia ya kujirahisisha na kujiumbua katika jamii ukafanya mambo ya kijinga kabisa unadhani atakuamini nani saa hizi?

Hiyo elimu yako inakusaidia mwenyewe na tumbo lako hilo. Hao CCM uliojifanya kuwatetea kipndi kile wakakubeba ukataka kuiua kafu saa hizi hata hawajui unakula nini wala unalala wapi.

Hebu usitusumbue sisi elimu, elimu. Elimu yako ni kwenye makaratasi tu
 
Back
Top Bottom