structuralist
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 1,230
- 907
Katika mabadiliko yaliyofanywa na rais kikwete kwa makatibu wakuu,hatimae neema yamuangukia aliyekuwa mtendaji mkuu wa tume ya vyuo vikuu ( TCU) Prof Sifuni mchome baada ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi. Hebu wadau tujiulize je changamoto za wizara ya elimu zitapata ufumbuzi wa haraka kwa ujio wa prof mchome? kwanini unasema hivyo? Na je nini athari (nzuri au mbaya) za kuondoka kwa Prof Mchome TCU? Je taifa litajivunia nini hasa katika mfumo wa udahili na uendeshwaji wa vyuo vikuu enzi za Prof Mchome TCU?