Makamu Mkuu wa chuo wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof Rwekaza Mkandala amekiri wazi kuwa katika jambo ambalo ameshindwa kulitatua ni malazi ya wanachuo wa wanaodahiriwa katika chuo hicho. Prof Mkandala ameyasema hayo kwa kujiamni katika mkutano na wafanyakazi wa shule kuu ya elimu uliofanyika leo saa 8 na nusu alasir katika ukumbi wa mazoezi karibu na Bar maarufu ya Daruso kampasi ya Mlimani.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wahadhiri na wafanyakazi wasiowahadhiri. Akijibu swali la Prof Mosha aliyetaka kujua nini mkakati wa chuo wa kuhusu kuongeza fursa ya malazi kwa wanachuo ambapo pia Prof Mosha hakusita kusema kuwa akiulizwa kuwa chuo kikuu cha Dar es Salaam kuna wasagaji jibu atatoa kuwa wapo kutokana hali mbaya na hatarishi ya msongamano wa wanachuo katika chumba kimoja kufikia nane na zaidi katika chumba chenye kubeba wanafunzi wawili hadi wanne.
Makamu huyo aliyembatana na naibu mkuu wa chuo utawala prof Mgaya na naibu mkuu wa chuo taaluma prof Maboko. Alieleza mikakati mbalimbali inayofanywa kulitatua suala hilo ambayo kwa mujibu wake yeye bado itakuwa ngumu kumaliza. Katika kukabiliana na chagamoto nyingine Prof Mkandala amewaeleza wafanyakazi hao kuwa chuo kimefanikiwa kupata mabasi matatu makubwa yatakayosaidia kukabiliana na changamoto ya usafiri.
Zaidi, makamu huyo mkuu wa chuo, aliwashangaza wengi kwa kuwazima midomo wafanyakazi waliokuwa wakitoa hoja ambazo yeye hakukubaliana nazo, mfano kuna hoja ilitolewa na Dr mmoja kuhusu changamoto za ufanyaji kazi chuoni kwa kumwambia akae kwani alichokuwa anaongea ni kitu mambacho sio hot issue kwa chuo na kuwa awasilishe kwa dean na kuambiwa kuwa hata udokta wake una mashaka kama hawezi kujua ni maswali gani ya kuuliza, alimnyamazisha pia Prof Njabili maarufu km prof Bibi ambaye liambiwa akae kwa kumfokewa mara kadhaa mfano aliambiwa kwa sauti ya ukali na ya juu" wewe mama kaa chini vipi…".
Prof Mkandala aliwaponda sana wahadhiri kwa kutofanya tafiti na kuandika miradi na kuwa anashangazwa na wahadhiri kukimbilia kuwa mapart time kwenye vyuo vingine badala kujikita katika uandishi wa miradi ambayo ndiyo unalipa zaidi katika hilo katolea mfano wa yeye mwenyewe na wakongwe wengine kujijenga zaidi kimaisha kwa uandishi wa tafiti.
Alisikitishwa na baadhi ya wahadhiri kudiriki hadi kufundisha shule za sekondari kitendo alichokitafsri kuwa ni kukidhalilisha hata chuo.
Source: Mimi mwenyewe nilikuwepo.