Prof. Mkenda: Bei ya Mafuta ya Kupikia imepanda kwa Sababu 55% ya Mafuta yanaagizwa kutoka Nje

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema bei za mafuta ya kupikia zimepanda kwa kuwa 55% ya mafuta ya kupikia yanayotumiwa nchini yanaagizwa kutoka nje hasa Malaysia.

Amesema Malaysia hutumia vibarua kuvuna chikichi, kutokana na #COVID19 vibarua wamekosa uhuru wa kwenda Malaysia na kufanya uzalishaji kuwa mdogo na bei kupanda.

Sababu nyingine ni kupanda kwa bei ya soya ambayo pia hutumika kuzalisha mafuta ya kupikia na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji duniani.

Hii serikali imeamua kupandisha kila kitu. Tuendelee kupanda wazee
 
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema bei za mafuta ya kupikia zimepanda kwa kuwa 55% ya mafuta ya kupikia yanayotumiwa nchini yanaagizwa kutoka nje hasa Malaysia.

Amesema Malaysia hutumia vibarua kuvuna chikichi, kutokana na #COVID19 vibarua wamekosa uhuru wa kwenda Malaysia na kufanya uzalishaji kuwa mdogo na bei kupanda.

Sababu nyingine ni kupanda kwa bei ya soya ambayo pia hutumika kuzalisha mafuta ya kupikia na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji duniani.

Mbona hata ya alizeti yanayozalishwa Tz yamepanda?
Anaogopa kusema ni TOZO !
 
Wazee wa soko la dunia 😂😂 ila uzuri wenyewe hawaathiriki na huu mfumuko wa bei ko haiwashtui hata kidogo zaidi tu ya kutoa taarifa kama hivi....😂😂😂 Soko la dunia bana
 
Uongo mtupu,,hiyo wizara imekushinda,,ww ulisema hutoi vibali vya kununua sukari nje,umelipuliwa na Mama,.Leo unakuja na uongo mwingine;
 
Bidhaa zikitoka nje sii ndiyo hua zinapungua bei maana wao kule hawana bei za ajabu...
 
Soon atakuja mtu na kuropoka neno “nonsense”. Not presidential at all…
 
Back
Top Bottom