Kutokana na kuwepo kwa vikundi vingi vidogovidogo vya wajasiriamali vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo za vyakula wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro, vikundi hivyo vimeahidiwa kutafutiwa wakala wa Vipimo hapa nchini TBS ili waweze kuwafikia wajasiriamali hao na kupima bidhaa zao ikiwa kama njia yakuziongezea thamani ili ziweze kuuzika ndani nanje ya nchi.
Ahadi hiyo imetolewa na Mbunge wa Rombo Prof.Adolf Mkenda Jumanne ya March 11, 2025 wakati akiwahutubia wanawake wawilaya ya Rombo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyoadhimishwa na wanawake wilayani humo.