OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Katika Mjadala wa ClubHouse wa kuhusu mageuzi ya elimu nchini, uliiongozwa na Gerson Msigwa na Waziri wa Elimu akiwa mzungumzaji, nimependa mambo mengi waliyozungumza kuhusu umuhimu wa tafiti.
Katika hoja zilizotajwa kulikuwa na hoja ya kuwa na tafiti nyingi nchini, suala ambalo Waziri wa Elimu ameonesha kukubaliana nalo. Kujibu hoja iliyokuwa raised mwanzo, juu ya kuboresha journals za ndani ya nchi, prof alisema watafiti wayatumie majarida mazuri ya nje.
Suala la wakufunzi, amesema suala sio ufaulu tu, bali ni wakufunzi kuandika na kuwa na machapisho ya kutosha kwenye majarida yanayofamika kimataifa.
Kiukweli hili ni jambo jema lakini je, taifa limejipangaje kuhakikisha tunakuwa na machapisho yenye impact kimataifa? Je, tutaendelea kutegemea hela za wahisani wa nje, huku ndani kukiwa hakuna mtu anayetoa funds za tafiti?
Je, kisheria ipoje, na mlolongo wa kupata ithibati ya kufanya tafiti ikoje? Maana kuna wakati mtu anapata hela nje ya nchi lakini akija nchini anakumbana na mlolongo wa sheria ambazo zinazuia baadhi ya tafiti kufanyika, au zinatumia muda mwingi kiasi cha donors kudai fedha zao wanapoona tafiti hazifanyiki, kumbe ni kwa sababu tu mtu amenyimwa ithibati huko COSTECH, kipi kitafanyika katika kipengele hiki?
Aidha, kama mtu anapata ithibati COSTECH ili kufanya tafiti yake, kwanini kuwe na mlolongo mwingine kwa data collectors mathalani kupata idhini ya Statician General ili kukusanya data?
Ili tafiti zifanyike kwa urahisi nchini, yafuatayo ni lazima yazingatiwe
1. Sheria zisibane as if kufanya tafiti ni uhalifu.
2. Sheria ziwe chache, na tafiti ziwe authorized na taasisi moja.
3. Serikali ijitahidi kukusanya data kwa wingi ili kwa wanaoweza kufanya kwa kutoenda field watumie data za serikali.
4. Serikali iwe na vipaumbele na iwe inatoa funds kwa kufanya tafiti hizo.