The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 9,436
- 10,944
Akisoma taarifa ya Hali ya Uchumi wa Nchi kwa mwaka 2023/24 na matarajio ya 2024/25 Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema, hadi mwezi machine deni la Serikali limefikia takribani Shilingi Trilioni 91.7. Deni hilo linajumuiaha deni la ndani na deni la nje.
Amesema ongezeko la deni limepanda kutoka Trilioni 77 Hadi Trilioni 92 kutokana na sababu kadha wa kadha zikiwemo:
- Serikali kupokea mikopo mipya na ya zamani
- Onvezeko la riba kwenye masoko ya Kimataifa (floating exchange)
Hadi Machi 2024, deni la Serikali lilikuwa shilingi Trilioni 91.7 ikilinganishwa na shilingi Trilioni 77 katika kipindi kama hicho mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 19.1.
Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo wakati akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2024/25 kuelekea kusomwa kwa bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha.
Amesema kati ya kiasi hicho, deni la ndani lilikuwa shilingi Trilioni 30.7 na deni la nje lilikuwa shilingi Trilioni 60.9 na kwamba ongezeko la deni lilitokana na Serikali kuendelea kupokea fedha za mikopo ya zamani na mipya kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme na maji.
Aidha, amesema ongezeko la deni lilichangiwa na kupanda kwa viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kuongezeka kwa riba kwenye mikopo ya nje ambayo riba zake hutegemea mabadiliko ya hali ya soko (floating rates).
-
My Take
Serikali ijikite kuongeza uzalishaji na Mauzo ya Nje.
Pili, kuvutia zaidi Mitaji ya uwekezaji.
Tatu Kuongeza juhudi kwenye Kuzalisha bidhaa zile ambazo tunaagiza Nje ya Nchi kama ngano,Mafuta,maziwa, furnitures na bidhaa za mifugo.
Mwisho kutoa kipaombele Kwa kampuni za Wazawa kufanya miradi badala ya Wachina.
Mwisho kukopa kunaendana na Ukubwa wa Uchumi pia, deni letu ni asilimia 60% tuu ya Ukubwa wa Uchumi wa Nchi na asilimia 40% tuu ya uwiano wa deni la Nje.👇👇
Mwaka 2023, pato halisi la Taifa lilifikia shilingi Trilioni 148.4 kutoka shilingi Trilioni 141.2 mwaka 2022, sawa na ukuaji wa asilimia 5.1 ikilinganishwa na asimilia 4.7 mwaka 2022.
Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2024/25 kuelekea kusomwa kwa bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha.
Amesema ukuaji huo ulichangiwa na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo mikakati ya kukabiliana na athari za vita kati ya Ukraine na Urusi pamoja na uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu na usafirishaji; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini, hususan dhahabu na makaa ya
mawe; na kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi iliyochachua shughuli za kiuchumi.
Hata hivyo amesema kiwango cha ukuaji wa Pato la Taifa kwa mwaka 2023 cha asilimia 5.1 kipo chini ya lengo la mwaka la asilimia 5.2.
Pia soma