Prof. Nabi anastahili pongezi

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Narudia ukishindwa kujenga kiwango chako chini ya Prof. Nabi hakika kama mchezaji utakuwa na shida, wachezaji wote wa Yanga wapo fiti, wachezaji wote wa Yanga wapo kamili, viwango vyao vipo juu, analisaidia sana taifa kuwa na wachezaji bora.

Nani aliamini mchezo wa leo muhimu ataanza na kijana wa Kinzanzibar Ibrahim Bacca binafsi baada ya line up nilishangaa sana ila baada ya mpira kwisha ndio nikashangaa zaidi Watunisia kutokuwa na onshot hata moja pamoja na kumwingiza mchezaji wao Tall ila bado hali ilikuwa tete kwao, ukuta wa Yanga ulikuwa solid.

Ibrahim Bacca amefanya makubwa, uzuri wa jamaa mpira wa nguvu anauweza, mpira wa akili yupo vizuri, mipira ya juu yupo njema, alikuwa beki mzuri ili chini ya mtaalamu Prof Nabi kaimarika zaidi. Nabi kocha mpole asiye na maneno mengi, ila anafahamu anachokifanya. Hakika hapa Yanga ilipata kocha, kaja Yanga kwa wakati sahihi.

Baada ya kijana Feisal kuleta mizaha na kazi yake, ilifika sehemu wakati wakaona kama Yanga imefika mwisho, ila wajuvi wa mambo walikwambia ukitaka kuimaliza Yanga chukua Nabi, hata ukimchukua Mayele ukamwacha Nabi ni kazi bure.

Pia tuwasifu viongozi wa Yanga kwa kumvumilia Nabi baada ya michezo miwili na Al hilal Wasudani yaliibuka maneno mengi sana yakiongozwa na wachambuzi mchongo wa Bongo, ila viongozi walitia pamba masikioni na kumwacha kocha afanye kazi yake.

Hongera Prof. Nabi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…