Prof. Ndalichako aibua ufisadi wa mamilioni ya fedha za mkopo wa Corona

Prof. Ndalichako aibua ufisadi wa mamilioni ya fedha za mkopo wa Corona

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, ameibua ubadhirifu wa mamilioni ya shilingi yaliyotolewa kutokana na mkopo wa UVIKO-19 kwa ajili ya ukarabati wa Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu Sabasaba.

Kufuatia ubadhirifu huo, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi katika chuo hicho kuangalia matumizi ya zaidi ya Sh. milioni 800 zilizotolewa kwa ajili ya ukarabati wa chuo.

Ubadhirifu alioubaini ni katika ununuzi wa vifaa vya ujenzi ambavyo vimenunuliwa kwa bei kubwa kuliko uhalisia, kuweka makadirio makubwa ya mahitaji ya vifaa vya ujenzi (BOQ) na kutopelekwa kwa baadhi ya vifaa katika chuo hicho wakati inaonyesha fedha zilishatolewa kwa ajili ya kuvinunua.

Prof. Ndalichako aliibua ubadhirifu huo baada ya kufanya ziara ya siku moja katika wilaya za Manyoni, Ikungi na Singida juzi kukagua miradi inayotekelezwa na serikali kupitia wizara yake.

NIPASHE
 
Back
Top Bottom