GE2025 Prof. Norman Sigalla King amechukua na kurejesha Fomu ya Kugombea Ubunge jimbo la Makete

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
230
Reaction score
793

Profesa Norman Sigalla King amerejesha Fomu za kugombea nafasi ya Ubunge jimbo la Makete kupitia CCM leo Julai 2, 2025. Prof. Norman ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo anakumbukwa na Wananchi wa Makete kutokana na kufanikisha ujenzi wa Barabara ya Lami kutoka Njombe - Makete.

Pia, miradi mingine ya Kimkakati ilifanikiwa wakati akiwa Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu ambayo husimamia masuala mbalimbali ikiwemo Barabara. Huduma nyingine ni Maji Safi na Salama ndani ya Jimbo hasa tarafa za Matamba, Lupalilo, Ukwama na Lupila pamoja na kufanikisha upatikanaji wa Nishati ya Umeme katika wilaya yote ya Makete.

Prof. Norman Sigalla King amewahi kutumikia nchi katika nafasi za Mkuu wa Wilaya, Mratibu wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, na Rais wa Wataalam wa Uchaguzi Kanda ya Afrika. Nafasi nyingine ni Afisa Tawala Tume ya Taifa ya Uchaguzi na DAS Temeke.
 

Attachments

  • 1000017167.jpg
    102.5 KB · Views: 71
Mtoa Taarifa unaweza kutuhabarisha huyu Norman ni Profesa wa kitu gani? Alikuwa anafundisha vyuo/chuo kikuu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…