RIP Prof Nzali,
Nimepatwa ma masikitiko makubwa baada ya kupata habari za msiba huu.
Namkumbuka Prof Nzali tangu aliponipokea UDSM akiwa First Year Convernor pale Faculty of Engineering na baadaye akawa mwalimu wangu katika Power Systems. Nilijifunza mengi kwe msomi huyu ambaye hakuwa na makuu.
Nashukuru nimepata fursa ya kuhudhuria asubuhi hii shughuli ya kutoa heshima ya mwisho pale Chuo kikuu. Kwa taifa tumempoteza mtu aliyeandaa wataalam wengi na amekufa angali akiwa na nguvu za kuendelea kutumikia taifa lake tena akiwa amechota maarifa lukuki.
Pole kwa familia, ndugu, marafiki, wahandisi na wote tulioguswa na msiba huu.
Msiba huu uwe changamoto kwetu tumuenzi Prof kwa kuchapa kazi kwa bidii zaidi kwani ni mmoja wa wale walioamini kuwa elimu tuliyo nayo ni utajiri tosha kwa taifa letu.
Amen