Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi,
Sote tunafahamu serekali ya awamu ya tano chini ya Mh sana Marehemu Dr John Pombe Magufuli iliharibu diplomasia yetu katika kiwango ambacho hakijawahi kuonekana tangu kuasisiwa kwa Jamhuri Muungano wa Tanzania.
Ni rahisi sana kumtupia furushi la lawama Marehemu Dr John Magufuli, lakini tukienda mbele na kutafakari kwa kina Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa EA ndiyo iliyokuwa na dhamana ya kushauri na kutoa mwelekeo wa diplomasia yetu kimataifa na ushirikiano wa kikanda EAC na SADC.
Bahati mbaya sana Marehemu Dr Mahiga aliondolewa foreign affairs na Prof Kabudi kuchukua nafasi yake.Nafasi ya waziri wa mambo ya Nje ni nafasi kubwa sana huwezi kuilinganisha na wizara ya ustawi wa jamii au mazingira. Kwa hakika hata ukitazama mataifa makubwa kama USA hii ni moja ya wizara nyeti na inayoheshimika sana.Mtu wa hovyo hovyo hawezi kupewa nafasi hii (secretary of state) hata huko UK ni hivyo hivyo.
Marehemu Dr Mahiga aliimudu Wiraza ya Mambo ya Nje kwa viwango vyote ajabu aliondolewa bila shaka mteuzi hakuridhishwa kwakuwa hakuwa mtu wa kufoka foka au kukurupuka. Dr Mahiga licha ya uzoefu mkubwa aliokuwa nao katika masuala ya kimataifa pia alihudumu UN katika nafasi za juu sana, sidhani kama yupo Mtanzania aliyehudumu katika nafasi za juu kumzidi Marehemu Dr Mahiga.
Baada ya Prof Kabudi kuchukua mikoba ya Dr Mahiga tulishuhudia papara nyingi na matamko yasiyokuwa na diplomasia wala staha. Mfano suala la Makonda kuzuiliwa kuingia Marekani tulimsikia Prof. akitunisha misuli badala ya kujikita kwenye hoja na hali halisi. Tungetegemea Prof Kabudi atoe ushauri na suluhisho ambalo lisingeacha maswali badala yake alitumia lugha ambayo haikuwa na tofauti na lugha za wabeba mizigo wa Kariakoo.