Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Posts
4,816
Reaction score
684
(Kutoka gazeti la mwananchi)
MWANAZUONI aliyebobea katika sheria, Profesa Issa Shivji na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Francis Stolla wamekosoa hukumu ya Mahakama ya Rufani, iliyomrejesha bungeni, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi, wanasheria hao walisema hukumu hiyo iliyotolewa na majaji watatu wakiongozwa na Nathalia Kimaro, Salum Massati na Bernard Luanda, inapingana na sheria.

Hata hivyo, mmoja wa mawakili wa Lema, Method Kimomogoro amepinga madai hayo akisema wanaoipinga pengine hawajapata nafasi ya kuliangalia kwa undani suala la haki ya mpiga kura kupinga matokeo mahakamani.

Profesa Shivji kwa upande wake alieleza kushangazwa na maelezo ya Mahakama ya Rufani kuwa mpiga kura hana haki ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi na kusema hiyo ni sawa na kutunga sheria mpya na si kutafsiri zilizopo.
Alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi, Katiba ya nchi na Mahakama, vinampa haki mpiga kura kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi.

"Sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja (Chediel ya mwaka 1980), vinampa haki mpiga kura kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Sijaona hoja nzito ya Mahakama ya kufuta haki hiyo ya mpiga kura," alisema Profesa Shivji.

Katika shauri hilo namba 84 la mwaka 1980 lililofunguliwa na William Bakari na mwenzake dhidi ya Mgonja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mahakama Kuu Tanzania iliamua kuwa, mpiga kura ana haki kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Walalamikaji walishinda.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani katika kesi ya Lema, iliamua kwamba hukumu katika kesi ya Mgonja ilikosewa kwani si sahihi kwamba mtu yeyote bila kujali mahali alipojiandikisha na kupiga kura anaweza kupinga matokeo katika jimbo lolote nchini hata kama haki zake hazijakiukwa kwa namna yoyote.

Lakini Profesa Shivji aliitetea hukumu hiyo ya Mgonja akisema imekuwapo kwa zaidi ya miaka 30 sasa na kwamba kwa muda wote huo imekuwa ikifuatwa katika uamuzi wa mashauri mbalimbali, huku akisisitiza kuwa Mahakama haiwezi kuifuta kirahisi tu.

Profesa Shivji alisema mpiga kura ni mwananchi na kwa vyovyote ana masilahi katika uchaguzi husika na hivyo anatarajia kuona uchaguzi ambao ni huru na wa haki.
"Hivyo huwezi kusema hahusiki na nani kashinda au kashindwa kwa kuwa uchaguzi ni muhimu katika kujenga na kukuza demokrasia," alisema Profesa Shivji.

Chama cha Wanasheria
Kwa upande wake, Stolla alisema: "Nimesikiliza hata maoni ya wanasheria mbalimbali wakizungumzia kutofurahishwa na tafsiri ya Mahakama ya Rufani kuhusu haki ya mpiga kura ‘ku-challenge' (kupinga) matokeo ya uchaguzi mahakamani," alisema na kuongeza:
"Katika uamuzi wa kisheria, inaonekana Mahakama imetunga sheria mpya na wengi tunajiuliza kama siyo, sababu ya kuwa mpiga kura ni ipi nyingine inampa haki mpiga kura kupinga matokeo?"

Stolla alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi ya tangu mwaka 1985, ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, kabla ya kutungwa upya mwaka 2005, inampa haki mpiga kura kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

"Mwaka 2002, sheria zote zilifanyiwa marekebisho na baadaye mwaka 2005, Bunge likatunga sheria mpya inayoitwa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, ikafuta ya mwaka 1985. Sheria hiyo na marekebisho yake, ndiyo inayotawala uchaguzi hadi sasa," alisema.

Alisema hata kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo ya Uchaguzi ya mwaka 1985, tayari kulikuwa na uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja ambayo iliamua kuwa mpiga kura ana haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

"Uamuzi wa kesi ya Mgonja ulikuja ‘ku-reflect' (kuakisi) hata kwenye Sheria ya Bunge ya mwaka 1985. Tangu hukumu hiyo ya Mgonja hakuna uamuzi mwingine wa Mahakama ambao umeshautengua huo, ndiyo maana hata wanasheria wanashangaa uamuzi huu wa Mahakama ya Rufani," alisema.

Alisema kumekuwa na kesi nyingi mahakamani za wapiga kura kupinga matokeo na kwamba nyingine hata yeye amezisimamia na hakuna wakati ambao Mahakama imewahi kusema kuwa hawana haki hiyo.

Alitoa mfano wa kesi iliyofunguliwa na wapiga kura dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Mbulu, Phillip Marmo baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Alisema kesi hiyo ilishindwa kuendelea kutokana na wapiga kura hao kushindwa kuweka mahakamani fedha ya amana kwa ajili ya kuiendesha na si kwa sababu hawakuwa na haki.

Akizungumzia hoja ya Mahakama ya Rufani kuwa hapakuwa na ushahidi kama walalamikaji walikuwa wapiga kura, Stolla alisema hilo halikuwa na ulazima kwa kuwa halikuwa jambo lililokuwa likibishaniwa.

"Hata hivyo, kabla ya kuanza kesi Mahakama Kuu, Jaji Mujulizi (Aloyce) aliitisha vithibitisho ili kujiridhisha kama ni wapiga kura," alisema Stolla na kuongeza:
"Lakini Mahakama ya Rufani wenyewe walianza kutafuta kama liliibuka Mahakama Kuu na licha ya Mahakama Kuu kuonyesha kuwa ilijiridhisha katika hilo, wao wakakosoa kuwa uthibitisho huo ulipaswa uwe sehemu ya mwenendo."

Katika uamuzi wake Mahakama ya Rufani ilisema kumbukumbu za Mahakama hazionyeshi iwapo vitambulisho vya wapiga kura viliwasilishwa na kupokewa mahakamani na ikaenda mbali zaidi kwa kutilia shaka jinsi rekodi ya kadi hizo zilivyochukuliwa.

Ilisema kinachoonekana katika kumbukumbu za Mahakama ni kiambatisho na maelezo tu kuwa wajiburufani ni wapiga kura waliosajiliwa na kwamba badala yake wakili wao ndiye aliyejaribu kuthibitisha hilo kwa maelezo, badala ya vielelezo.

Ilisema Wakili wa wajibu rufaa, Alute Mughway aliwasilisha kadi za wateja wake kwa Jaji Aloyce Mujulizi kuthibitisha kuwa walikuwa wapiga kura halali, lakini Mahakama hiyo ikasisitiza kuwa utaratibu huo ni kinyume cha sheria kwa kuwa ushahidi kama huo ulipaswa uwasilishwe moja kwa moja mahakamani na utolewe na wamiliki wa nyaraka husika.

Ilisema hata kama ingethibitika kuwa wajibu rufani walikuwa wapiga kura waliosajiliwa, bado hawakuwa na haki kisheria kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi kwa madai ya mrufani kutumia lugha za matusi kwenye kampeni zake.

Mugway ashangaa
Wakili Alute Mughway aliyekuwa akiwatetea wajibu rufaa katika rufaa hiyo, alisema Mahakama imeacha jukumu lake la kutafsiri sheria na badala yake ikatunga sheria mpya ambayo inapingana na Sheria ya Bunge na Katiba ya nchi, Ibara ya 26 (2).

Alisema Kifungu cha 111 (1) cha Sheria ya Uchaguzi, Hukumu ya kesi ya Mgonja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinampa haki mpiga kura kufungua shauri mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi.

Alisema kwa mujibu wa kifungu hicho, miongoni mwa watu wanaoweza kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi ni aliyepiga kura au aliyekuwa na haki ya kupiga kura na kwamba tangu wakati huo kifungu hicho hakijawahi kufanyiwa marekebisho.

Wakili wa kujitegemea, Vedasto Audax alikaririwa na gazeti dada la The Citizen akisema: "Swali langu ni kwamba ni lini uamuzi wa kesi ya Mgonja ulionekana kuwa na makosa kisheria? Ni kuanzia leo baada ya Mahakama ya Rufani kutamka kuwa una makosa?"

Wakili wa Lema
Kimomogoro alisema hukumu ya kesi ya Mgonja haijitoleshelezi kwa sababu haikusema ni katika mambo gani mpiga kura ana haki ya kufungua kesi kupinga matokeo mahakamani huku akisema kwa maoni yake, anakuwa na haki pale tu haki zake kama mpiga kura zinapokiukwa.

"Mpiga kura hawezi kuwa na haki sawa na mgombea. Mgombea haki zake ni kubwa kuliko mpiga kura kwa sababu kwanza yeye ni mpiga kura na pili ni mgombea," alisema na kuongeza:

"Ndiyo maana mpiga kura anaruhusiwa kupiga kura katika kituo kile alichojiandikisha tu lakini mgombea huweza kupiga kura katika kituo chochote."

Alisema mwananchi wa kawaida tu ambaye hajajiandikisha hata kama akimwona mgombea akitoa rushwa hadharani, hana haki ya kufungua kesi mahakamani, lakini alipoulizwa kwa upande wa mwananchi aliyejiandikisha kupiga kura alisema hakuwa na rejea za sheria kwa kuwa alikuwa Karagwe kwa mapumziko.

Kesi ya Lema
Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, mwaka huu kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake.

Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake alikuwa akitumia lugha za matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batilda Buriani.
Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila ilimtia hatiani kwa kutumia lugha ya matusi na kutengua matokeo yaliyompa ushindi.

Lema alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupitia kwa mawakili wake, Kimomogoro na Tundu Lissu ambayo Desemba 21, mwaka huu ilimrejesha tena bungeni baada ya kuikubali.

Katika uamuzi wake, Mahakama hiyo ilisema kwa kuwa kisheria hayo ni masilahi ya umma kufikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba na kwamba mlalamikaji anapaswa kuonyesha haki zake au masilahi ambayo yameingiliwa na athari alizozipata.
"Hivyo mpiga kura hana haki ya kisheria kufungua kesi kuhoji matokeo ya uchaguzi pale ambapo haki zake hazikukiukwa," ilisema Mahakama ya Rufani.

Ilisema kwa mujibu wa Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya Tanzania, raia anakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi kwa masilahi ya jamii, kama ilivyotokea katika kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa SerikaIi ya mwaka 1995.

Ilisema kesi dhidi ya Lema haikufunguliwa chini ya Ibara ya 26 (2) ambayo inampa fursa na haki raia yeyote kufungua shauri mahakamani lenye masilahi ya umma, huku ikisisitiza kuwa madai ya wajibu rufani katika kesi hiyo hayagusi masilahi ya jamii yote.
 
Kupinga au kuunga mkono kwenye masuala ya kisheria ni jambo la kawaida ndiyo maana kukawa na upenyo wa kukata rufaa. Kimsingi masuala ya kisheria siyo sawa na hesabu ambapo moja na moja ni mbili. Kwenye sheria hakuna kukosea au kupatia hadi hukumu ya mwisho kwenye ngazi ya mwisho. Hivyo Shivji hajakosea sawa na akina Lissu wanaopingana na hoja ya Shivji.
 
Anachosema Prof Shivji ndicho nilichosema mimi awali hapa, ukiondoa mfano wa kesi ya Chediel Mgonja.

Halafu angalia washabiki wa Lema watakavyokuja kijumlajumla bila uelewa wa nini kimepingwa.

Kimomogoro anachekesha. If anything mpiga kura anatakiwa awe na haki kuliko mgombea.
 
Profesa Shivji alisema mpiga kura ni mwananchi na kwa vyovyote ana masilahi katika uchaguzi husika na hivyo anatarajia kuona uchaguzi ambao ni huru na wa haki.
"Hivyo huwezi kusema hahusiki na nani kashinda au kashindwa kwa kuwa uchaguzi ni muhimu katika kujenga na kukuza demokrasia," alisema Profesa Shivji.

Mimi siyo Great Thinker kama Gaijin, EMT, au Bu'yaka :becky: lakini hiki anachosema Shivji hata kule kwenye jukwaa la hawa ma Great Thinkers nilikisema.

Mpiga kura atakosaje kuwa na maslahi katika chaguzi za nchini mwake bana?
 
Mimi nadhani mahakama ya rufani hoja yake ya msingi ingejikita katika uthibitisho je wale wapiga kura waliathiriwa vipi na mtokeo ya uchaguzi. Election has public interests.
Nakuhusu haki ya mpiga kura kushtaki mahakama ilitakiwa ieleze kwamba mpiga kura ataruhusiwa kufungua kesi endapo;
1. Haki ya mpiga kura binafsi zimeathiriwa.
2. Kama kuna vitendo vyovyote ambavyo vilifanyika na mpiga kura anaweza KUTHIBITISHA kwamba vitendo vile vilimuathiri yeye pamoja na uchaguzi kwa ujumla. Hapa akiwa na uwezo wa kuthibitsha alivyoathiriwa then he/she should have Locus stand.

N:B
Endapo kufungua kesi katika masuala ya uchaguzi itakuwa haki kamili ya mpiga kura bila kuonesha ni vipi ameathiriwa basi kutakuwa na mrundikano wa kesi ambazo zitakuwa zipo mahakaman muda mrefu maana huyu atakuwa anafungua kwa jambo hili, kesho mwingine ataibuka na jambo lingine na hii inatokana na siasa za Tanzania si za kidemokrasia bali za kukomoana.
 
Kimomogoro anachekesha. If anything mpiga kura anatakiwa awe na haki kuliko mgombea

I had to do a double take on that one coz it sure didn't make sense the first time I read it and it still didn't make sense the second time either.

"Mpiga kura hawezi kuwa na haki sawa na mgombea. Mgombea haki zake ni kubwa kuliko mpiga kura kwa sababu kwanza yeye ni mpiga kura na pili ni mgombea," alisema na kuongeza:

"Ndiyo maana mpiga kura anaruhusiwa kupiga kura katika kituo kile alichojiandikisha tu lakini mgombea huweza kupiga kura katika kituo chochote."

Really?:confused2::confused2:
 
Mimi siyo Great Thinker kama Gaijin, EMT, au Bu'yaka :becky: lakini hiki anachosema Shivji hata kule kwenye jukwaa la hawa ma Great Thinkers nilikisema.

Mpiga kura atakosaje kuwa na maslahi katika chaguzi za nchini mwake bana?
Nyani Ngabu,
Nimeupenda ule mjadala wenu kule Great Thinker.

Nilikuwa naongea na jaji mmoja TZ, naye akasema mawakili wengi wanapinga hii sehemu ya hukumu kuhusu mpiga kura. Huenda wakafungua kesi nyingine kama njia ya kurekebisha hili kosa. Sijui wanafunguaje kesi za namna hiyo ila inaelekea kuna malalamiko mengi kuhusu hili suala la mpiga kura kusema hana haki kufungua kesi.

Nimecheka sana hiyo ya kwamba mgombea ana haki kubwa kuliko mpiga kura/ labda huyo wakili wamemu quote vibaya. Ila kama kasema hivyo, mmmmhhhhh!!!!!
 
shivji anachemka katika hili

Shivja anaijadili sheria ilivyo lakini hakuangalia sheria hiyo katika uchaguzi huo wanaopinga matokea waliathiriwaje na madai yao kitu ambacho mahakama imeegemea kutoa hukumu yake. Hao wapiga kura hawakutukanwa na Lema sasa wanasimamaje kudai haki mahakamani wakati aliyetukanwa hakulalamika wala kuwa mmoja wapo wa mashahidi. Pamoja na ugwiji wa sheria katika hali kachemka sana.
 
Hili si ndiyo tulikuwa tunalijadili kule kwa akina Great Thinkers (@Kiranga, Gaijin, Zakumi, EMT na wengineo). Naona hata Shivji naye anaona dosari zilizopo katika hiyo hukumu!

Hehehe. Mwalimu wangu aliyenifundisha maana na application ya locus standi nae anapinga?

Ngoja nikakague notes za lectures zake wakati anatufindisha hii kitu kama alisema the doctrine of locus standi does not apply to election litigation, let alone mentioning the case of Mgonja.

Mgonja was a good law until the CA said in Lema it wasn't.

It does not matter that Mgonja had been binding for 30 years. Tunazo sheria za muda mrefu mbovu nyingi tuu.

May be before Lema, the CA did not have an opportunity to consider whether Mgonja was a good law.

Bado haijaniingia akilini eti mtu aliyejiandikisha na kupigia kura Chake Chake anakuja kumshtaki diwani aliyeshinda uchaguzi Ngara eti kwa sababu anayo haki ya kufanya hivyo hata kama haki zake hazijawa affected.

Kesi ya Lema itazuia wanasiasa wenye uchu wa madaraka kujificha nyuma ya wapiga kura wa kawaida kufungua kesi halafu wakishindwa wanawakana inapofikia muda ya kulipia gharama za kesi.
 
Mpiga kura ana haki ya kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi, lakini katika mazingira yapi????

Malalamiko yaliyowasilishwa mahakamani na wapinga matokeo binafsi niliyaona yana walakini.

Wapiga kura wanalalamika kwamba mgombea wao alishindwa kwa vile alitukanwa kwamba ni side dish ya waziri mkuu wa zamani!!!!
Sasa sijui tamko hilo linamnyima kura vipi mgombea na linampa kura vipi aliyetamka na zaidi linawanyima haki wapiga kura vipi.

Kuna watu tunawaheshimu kwa mvi zao, lakini nadhani wakti umefika naamini wanatakiwa wakakojoe walale.
 
1. Mahakama inaweza kutunga sheria kutokana na hukumu zake. Wakina shivji wakasome hukumu za judge Demining wa uingereza jinsi hukumu zake zilivhotengeneza sheria nyingi za jumuia ya madola. Kama kulikuwapo na hukumu ya 1980 inamaana haiwezi kutenguliwa tena?
2. Mahakama haikusema wapiga kura hawana haki ila hicho walichofungulia kesi ndio kina ulakini. Kumbuka wale wanaharakati waliofungua kesi ya kugomea malipo ya dowans mahakama ilisema wazi kuwa hawana haki kwa vile sio party to the contract. Lakini hao wanaharakati na watanzania wote ni walipa kodi na tuna haki wao hawakuliona hilo? Mahakama zimeweka utaratibu kuwa lazima uwe muadhirika au ufungue kesi kwa niaba ya mwadhirika kwa ridhaa yake. Au mtu ukiona jirani amewekewa X unaweza kwenda mahakamani kupinga kwa vile utapoteza jirani? Mwadhirika wa kesi hakwenda mahakamani na kesi ya kutukana kama ni kweli wangepaswa wapeleke polisi ili jamhuri imfungulie shitaka la jinai. Kama mwanachi anaweza kufungua mashitaka ya jinai basi hata wanachi wafungue kesi za watuhumiwa wa epa si wote ni waadhirika na tuna haki na kodi zetu?
 
Halafu angalia washabiki wa Lema watakavyokuja kijumlajumla bila uelewa wa nini kimepingwa.
Wengine hatukushiriki sana kwenye huo mjadala lakini everytime I come across such blanket statement kama hii yako, I lose interest. Jaribu kuwapa breathing space watu usiokubaliana nao...mara wapenzi wa Chadema, mara wapenzi wa Dr. Slaa na sasa imeongezeka wapenzi wa Lema, duh, eti hawana uelewa wa nini kinachoongelewa. Kiranga nakuheshimu na nisingependa tujiingize kwenye nani zaidi bali tubakie kwenye kupingana kwa hoja...ni hayo tu, sasa tuendeleee. How I wish some of us had more time to participate kwenye mijadala mbalimbali but then...

Binafsi naamini kuna mambo ya kipuuzi tunayoyapa kipaumbele while in actual fact ni non issues from the word go. Sisi tuliobahatika kupata exposure kwa wenzetu ambako demokrasia imekomaa, no voter would dream of going to court to challenge an election result based on mgombea anayemtaka kushindwa uchaguzi kwa sababu alikashifiwa kwenye kampeni huku mhusika hayuko tayari hata kuwa shahidi mahakamani...it is stupid, ridiculous and makes no sense. Nina hakika hata mahakama ililiona hili kwamba ku"entertain" kitu kama hicho ni kuidhalilisha mahakama. Naamini hukumu iliyotolewa ilizingatia hilo.
 
Mimi sio mwanasheria lakini kwa kutumia akili kufikiria suala hili inaonekana wazi kwamba walalamikaji walishawishiwa tu kufungua kesi mahakamani bila kutafakari mwongozo wa kesi ya Mgonja na ile ya mchungaji Mtikila, na hata mwanasheria wao nae alitayarishwa tu harakakaraka kwenda mahakamani kufungua kesi.

Mahakama ya Rufaa ina watu kama akina mama Kimaro ambao hawajapanda kufika hapo bure tu na mzee Shivji anakuwa anauliza swali la "integrity" yao katika kutoa maamuzi waliyoyafikia na hili ni tusi.

Majaji hawa wametoa uamuzi wao kwa misingi kwamba walalamikaji hawakutumia kifungu cha Ibara ya 26 (2) na kwamba majibu ya rufani hiyo hayagusi maslahi ya jamii yote yaani Arusha nzima bali ile jamii ya Arusha mjini.

Halafu inakuwaje kesi ya Mgonja na Mtikila ziwe sheria na zisiwe miongozo katika kujadili kesi mahakamni?

Kwa hili naona mzee Shivji amekurupuka kutoa maelezo yake.
 
Bado haijaniingia akilini eti mtu aliyejiandikisha na kupigia kura Chake Chake anakuja kumshtaki diwani aliyeshinda uchaguzi Ngara eti kwa sababu anayo haki ya kufanya hivyo hata kama haki zake hazijawa affected

Kuwa na haki na kuwa na sababu ni vitu viwili tofauti.
 
Shivji kaamua kuchafua hewa kwa makusudi kabisa na hii ni dhambi ambayo itamrudia tu.
Hii ni 2012 awareness ya binadamu inazidi kuongezeka kila sekunde inayopita.
Tutarajie kuna madudu mengi kutoka kwa watu wenye majina kama Shivji.
 
1. Mahakama inaweza kutunga sheria kutokana na hukumu zake. Wakina shivji wakasome hukumu za judge Demining wa uingereza jinsi hukumu zake zilivhotengeneza sheria nyingi za jumuia ya madola. Kama kulikuwapo na hukumu ya 1980 inamaana haiwezi kutenguliwa tena?

I beg to differ. Parliament should always make law and the courts should interpret the law.

We should respect and observe the fundamental constitutional principles to avoid abuse.

Lord Denning was perhaps the greatest law-making judge of the last century and the most controversial.

His achievement was to shape the common law according to his own highly individual vision of society.

He stepped down from the House of Lords to a much more influential post - Master of the Rolls so that he could do his thing without interference.

During his 20 years as Master of the Rolls, he could choose his own cases and the judges who were to sit with him. So on most issues, he effectively had the last word.

But in seeking justice Lord Denning, considered himself entitled to get round - or even change - any rule of law that stood in his way. There was no need to wait for legislation.

"Parliament does it too late," he argued. "It may take years and years before a statute can be passed to amend a bad law.

"The judge ... should make the law correspond with the justice that the case requires."

Although he saw himself as champion of the underdog - the ordinary citizens, the consumers, the deserted wives - he supported employers against trade unions, education authorities against students, and the Home Office against immigrants.

But his 1982 book "What Next in the Law" was his downfall. In it, he seemed to suggest some black people were unsuitable to serve on juries.

Lord Denning's prejudices demonstrate the risks of letting one man dispense justice.

BBC News | UK | Denning: A life of law
 
EMT,

..lakini malalamiko dhidi ya Mgonja yalihusisha masuala ya rushwa.

..wakati hii ya Lema inahusisha matamshi aliyoyatoa wakati wa kampeni ambayo wapiga kura watatu wanaamini ni kashfa na wameathirika.
 
Last edited by a moderator:
Mahakama ya Rufaa ina watu kama akina mama Kimaro ambao hawajapanda kufika hapo bure tu na mzee Shivji anakuwa anauliza swali la "integrity" yao katika kutoa maamuzi waliyoyafikia na hili ni tusi.

Hapana! Pamoja na kwamba sikubaliani na argument ya Prof. Shivji sidhani kama amewatusi majaji waliotoa hukumu.

It is normal in the legal field to criticise court judgements. Ndiyo maana kwenye nchi za watu controversial decision kama hii inazalisha articles hata 500 within the first few months, some applauding, others, criticising, the decision.

It is normal kabisa na kufanya hivyo haina maana kuwa mtu ana-question intergrity ya jaji aliyetoa hukumu.

Tumefundishwa kukubaliana kutokubaliana. Kwa vile sijakubaliana na wewe haina maana kuwa nimekudharau au nimekutusi.

You will still be my learned brother/sister. lol.
 
Back
Top Bottom