Prof. Soccorsi, Daktari Binafsi wa Papa afariki dunia kwa Covid-19

Prof. Soccorsi, Daktari Binafsi wa Papa afariki dunia kwa Covid-19

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
cq5dam.thumbnail.cropped.750.422.jpg

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 26 Januari 2021 amehudhuria Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumwombea Prof. Fabrizio Soccorsi aliyekuwa daktari wake binafsi kuanzia mwaka 2015-2021.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 26 Januari 2021 ameshiriki katika Ibada ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa kwenye Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Familia mjini Vatican, kwa ajili ya kumkumbuka na kumwombea Marehemu Professa Fabrizio Soccorsi, daktari binafsi wa Papa Francisko, aliyefariki dunia, Jumamosi tarehe 9 Januari 2021.

Professa Soccorsi ameaga dunia baada ya kushambuliwa na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19. Tangu tarehe 26 Desemba 2020 alikuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Agostino Gemelli, iliyoko mjini Roma kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Saratani. Ibada ya Misa Takatifu imeongozwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican na kuhudhuriwa na Baba Mtakatifu Francisko pamoja na viongozi waandamizi kutoka Vatican.

Professa Fabrizio Soccorsi, alizaliwa tarehe 2 Februari 1942 mjini Roma. Amefariki dunia wakati alipokuwa anajiandaa kuadhimisha miaka 79 tangu alipozaliwa. Ilikuwa ni tarehe 8 Agosti 2015 Baba Mtakatifu Francisko alipomteua Professa Fabrizio Soccorsi kuwa daktari wake binafsi. Alikuwa ni daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya tumbo. Baada ya kutunukiwa shahada ya uzamivu katika magonjwa ya binadamu alibahatika kutekeleza utume huu kwa uadilifu na weledi mkubwa, kiasi cha kuteuliwa kuwa mkuu wa kitengo cha magonjwa ya ndani, Hopitali ya San Camillo-Forlanini, iliyoko mjini Roma.

Professa Fabrizio Soccorsi, alibahatika kuwa ni jaalimu wa “kutupwa” mkoani Lazio lakini kwa namna ya pekee katika Chuo Kikuu cha “La Sapienza” kilichoko mjini Roma. Professa Soccorsi alikuwa ni mtaalam mshauri wa Wizara ya Afya nchini Italia, Kurugenzi ya Afya na Usafi mjini Vatican na pia Daktari mshauri wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu.

Kutokana na mchango wake mkubwa kwa familia ya Mungu ndani na nje ya Italia, lakini kutokana na uhusiano wa karibu aliokuwa nao kwa Baba Mtakatifu Francisko kama daktari wake binafsi, aliamua kuhudhuria Ibada ya Misa ya Mazishi ya Professa Fabrizio Soccorsi, kwa kimya na tafakari ya kina kuhusu hatima ya maisha ya mwanadamu hapa duniani.
 
... hili gonjwa sio la mchezo jamani. Tujikinge kwa nguvu zote; tuzingatie kanuni zote za kiafya za kujikinga acha kusikiliza maneno ya mtu. Afya ni yako, unalo jukumu la kuilinda afya yako.
 
Taarifa ya kifo kimoja tu cha corona jinsi watu wanavyokipokea ni tofauti na taarifa ya vifo vya maradhi mengine.
 
Acha kuwatisha watu kijana. Corona ni ugonjwa wa kawaida tu tofauti na kiki muzoupa.
... hili gonjwa sio la mchezo jamani. Tujikinge kwa nguvu zote; tuzingatie kanuni zote za kiafya za kujikinga acha kusikiliza maneno ya mtu. Afya ni yako, unalo jukumu la kuilinda afya yako.
 
Taarifa ya kifo kimoja tu cha corona jinsi watu wanavyokipokea ni tofauti na taarifa ya vifo vya maradhi mengine.
Corona ni tofauti na magonjwa mengine.

Sio kwamba linaua sana (just 5%) ila linaambukiza sana na nirahisi kwa kuambukiza huku wale 5% wakafikiwa popote pale walipo...

Tofauti na magonjwa mengine makali sana unapata haraka haraka unajiondokea wewe, ila hili unaweza usiondoke alafu ukawagawia mtaa mzima within masaa
 
Ndio hatari ya huu ugonjwa ni hapo kwenye kuambukiza kama mfano ebola ndio ungekuwa unaambukiza kama corona basi ingekuwa balaa.
 
Back
Top Bottom