Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu amefanya mazungumzo na Professa Ali Tabibu Ibouroi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Comoro alipomtembelea katika makao makuu ya Chuo hicho.
Kwa upande wake, Balozi Yakubu alipongeza ushirikiano uliopo na kuongeza kuwa fursa zaidi za ushirikiano bado zipo hususan katika shahada za uzamili na uzamivu ambazo hazijaanza kutolewa na chuo hicho.
Aidha, Balozi Yakubu alipendekeza Chuo hicho kuangalia uwezekano wa kushirikiana na vyuo vya Tanzania ili kuanzisha taasisi zitakazotoa kozi za kitaaluma kama vile Uhasibu na Tehama badala ya utaratibu wa sasa ambapo wanafunzi wa Comoro lazima kuchukua kozi za kitaaluma toka nchi za jirani.
Viongozi hao walikubaliana pia kuratibu ziara za viongozi na wadau wa sekta ya Elimu.
Prof. Ibouroi alimweleza Balozi Yakubu kuwa Chuo hicho kimeanzishwa miaka 20 iliyopita na ndio chuo kikuu pekee nchini Comoro kikiwa kina wanafunzi 12,000 na walimu 300 ambapo kina vituo vya ufundishaji 10 katika visiwa vitatu vya Ngazidja, Anjouan na Moheli.
Mkuu huyo wa Chuo alieleza pia maeneo kadhaa ya ushirikiano na Tanzania ambapo wana ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dar es salaam tangu mwaka 2008 na mwaka jana walisaini makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikiu cha Taifa cha Zanzibar ikiwemo kubadilishana walimu na wanafunzi.Viongozi hao walikubaliana pia kuratibu ziara za viongozi na wadau wa sekta ya Elimu.