Profesa anaposhindana na mwanafunzi

Profesa anaposhindana na mwanafunzi

geofreyngaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2014
Posts
658
Reaction score
946
Siku ya kwanza kujoin UDSM akili iliniambia sasa upo kwenye center of educational excellence, chuo ambacho kimsingi uhitaji kutamka jina lake, we sema tu nipo chuo kikuu inatosha kumaanisha chuo kikuu cha dar es salaam. Chuo ambacho kwa miaka mingi kinaheshimika na naamini wengi wetu tungependa kusoma hapo hata Jina lake tu zuri chuo kikuu cha dar es salaam au university of dar es salaam.

Siku ya kwanza darasani alikuja profesa jina nimelisahau alishangaa sana kutuona tupo wengi akasema hv, nanukuu "toka nianze kazi hapa chuo sijawai ona darasa limejaa kiasi hiki, lazima ning'oe air msae mbili humu" air msae ni mabasi yaendayo mikoani, maana yake atatufelisha wanafunzi kama 120.

Mwingine alikua ni Dr by academics, kwa ukubwa wa madarasa na idadi ya wanafunzi sirahis mwalimu kusikika bila kutumia vipaza sauti lkn aligoma kufanya hivyo siku zote za maisha yangu hapo chuo.

Wkt nikiwa nashauku ya kutembea tembea chuoni huku nikiwa nimetiwa hofu na hawa waalimu wangu ninaowategemea wanipike nipikike nikashuka kitengo cha uhandisi(faculty of engineering) nilishangaa kuona paa na kata vimeoza nilijiuliza maswali mengi kwanini imekua hivyo tena engineering faculty? Kila siku wanafunzi wahandisi wanafanya vitu kwa vitendo, wanakata mabati wanatengeneza vitu mbalimbali na vingine mwisho wa siku vinatupwa, wanajenga na kubomoa kama mafunzo, kwann wasielekezwe kutengeneza hapo panapovuja? Baada ya muda nikaanza kukumbuka kauli na vitendo vya waalimu nikaona vinaendana na mazingira nayo.

Nilimwambia Mzee wangu ambaye anakipenda na kukisifia CHUO KIKUU mpaka kesho, nasoma UDSM bcoz sina alternative otherwise I would have left and join another better college than this manzese type of university.

Haya ni machache tu lkn yapo madudu mengi tu. Kwa style hii ni vigumu kuzalisha watu wenye weledi wakutosha ili kulijenga taifa.
Kwa ujumla wake kuna matatizo kama haya mengi toka ngazi ya primary hadi vyuoni.
 
nikiona jina Prof.nikikumbuka Prof.Muhongo na mwenzako Prof.Jk nawadharau sana hawa maprofesa wote wanaona wapo hawana akili kabisa ukisoma sana mbeleni giza.
 
hayo ni matatizo ya kutojua umeenda chuo kufanya nini. unataka upikwe? chuo ni kujifunza sio kufundishwa. alafu ngwini ulienda kutafuta nini coet (foe )?
 
Huwa naenda kunywa supu ya kongoro pale coet cafeteria! Niliuliza SK 1 kuwa chuo kinashindwa ht kupiga plasta! Nikaambiwa wamereserve for history!
 
hayo ni matatizo ya kutojua umeenda chuo kufanya nini. unataka upikwe? chuo ni kujifunza sio kufundishwa. alafu ngwini ulienda kutafuta nini coet (foe )?
Nimecheka sana. Mkuu kule COET kuna madarasa yanatumika na wanafunzi wa Chuo kizima wakiwemo ngwini.
 
hayo ni matatizo ya kutojua umeenda chuo kufanya nini. unataka upikwe? chuo ni kujifunza sio kufundishwa. alafu ngwini ulienda kutafuta nini coet (foe )?

Inawezekana kabisa nilikwenda bila kujua nafata nn, lkn je tunahitaji wasomi wa namna hii?
Kuwa ngwini au injinia has nothing to do with what I've written.
Lkn comment yako imenisaidia kujua uwezo mkubwa ulionao.
Welcome my dear!
 
Mbona nilichokisema hakiusiani na profession ya mtu, why then mine?
Its ol about the misbehaviour of the so called wasomi
sasa mbona unatajataja Coet na wanafunzi wake? k\mbona chuo kuna ufisadi wa hali ya juu kwenye hostels na UDBS wapo???
 
nikiona jina Prof.nikikumbuka Prof.Muhongo na mwenzako Prof.Jk nawadharau sana hawa maprofesa wote wanaona wapo hawana akili kabisa ukisoma sana mbeleni giza.

Umesahau Prof. Mama Tibaijuka
 
sasa mbona unatajataja Coet na wanafunzi wake? k\mbona chuo kuna ufisadi wa hali ya juu kwenye hostels na UDBS wapo???

Nina Uhuru wa kuongelea kitu chochote nachokijua including coet ilimradi sivunji sheria ndugu yangu, inaelekea coet imekupumbaza akili mpaka unaiona kama mungu hutaki iguswe japo inamadhambi kibao.
Nasikia mnataka kujitenga, kweli rafiki?
Ht hivyo naogopa kuargue na watu wenye akili nyingi kama wewe.
 
Huwa naenda kunywa supu ya kongoro pale coet cafeteria! Niliuliza SK 1 kuwa chuo kinashindwa ht kupiga plasta! Nikaambiwa wamereserve for history!

hahaha reserved for history... mwisho wake patabomoka na wasipajenge waweke history
 
Nina Uhuru wa kuongelea kitu chochote nachokijua including coet ilimradi sivunji sheria ndugu yangu, inaelekea coet imekupumbaza akili mpaka unaiona kama mungu hutaki iguswe japo inamadhambi kibao.
Nasikia mnataka kujitenga, kweli rafiki?
Ht hivyo naogopa kuargue na watu wenye akili nyingi kama wewe.
tulishajitenga kitambo ndoo maana kuna uzio wa kutenga pumba na mchele toka zamani get la kutoka na kuingia
 
UDSM ndo chuo kibovu kuliko vyote tz kinaongoza kututolea viongoz virazaa wanajiita maprof kwa degree za kupewa dooooo!
 
Si bure wewe ni mwanafunzi wa Sekondari na hadithi hii kakusimulia kaka yako wakati huu wa likizo
 
Back
Top Bottom