Profesa Baregu aonya majungu mjadala wa rasimu ya katiba

Profesa Baregu aonya majungu mjadala wa rasimu ya katiba

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,503
MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu amewataka wajumbe wa mabaraza ya katiba kujenga hoja kuhusu muundo wa Serikali wanayoitaka badala ya kung'ang'ana wakiwalaumu wasomi kwa kudai wanaipeleka nchi kusikojulikana kutokana na wengi wao kuonyesha wanataka Serikali tatu.

Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Katiba la Wilaya ya Sumbawanga Prof. Baregu alionyesha dhairi kukerwa na kauli hiyo ya kusema "wasomi wanaipeleka nchi kusikojulikana" ambayo ilijitokeza mara kadhaa kwa watu waliokuwa wakichangia rasimu hiyo ya katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

"Hoja za kusema wasomi mnatupeleka kusikojulikana siyo sahihi kama hamtaki serikali tatu jengeni hoja ya muundo wa serikali mnazotaka. Hii ni katiba ya Watanzania wote siyo wasomi pekee.......sisi tutazichukuwa hoja zenu na kwenda kuzifanyia kazi" alisema Prof. Baregu.

Awali diwani wa Kata ya Muze, Kalolo Ntilo alisema kuwa suala muungano wa Serikali tatu ambalo rasimu imependekeza hakubaliani nalo ila anataka kuwepo Serikali mbili za Tanzania bara na Zanzibar ambazo zitaunda muungano wa nchi hizo mbili huku wakiwatupia lawama wasomi kwa kudai wanataka kuwepo Serikali tatu ambazo athari zake ni kuvunjika kwa muungano miaka kadhaa ijayo.

Diwani huyo alisema suala la serikali tatu linahitaji mjadala wa kipekee utakajumuisha Watanzania wote hivyo kwa maoni yake haoni sababu ya katiba ijayo kuwa na muundo wa Serikali hizo ambazo zinapigiwa chepuo na baadhi ya wananchi wakiwamo wasomi.

Mkazi wa Kaengesa, Lazaro Muntama alisema kuwa ili kunusuru muungano kutovunjika ipo haja ya kuwepo kwa Serikali tatu yaani ya Tanganyika, Zanzibar na Muungano ambapo alipinga hoja za baadhi ya wajumbe zinazoeleza kuendesha serikali hizo ni gharama kubwa.

"imefika wakati sasa na sisi watu wa bara tunataka Serikali yetu ya Tanganyika ili tuwe na muundo wa Serikali tatu siyo mbili huku ni kujizudhuru haki yetu.

Kwa hisani ya Mwananchi.
 
Kuna jambo moja la muhimu sana katika rasimu hii kuhusiana na muundo wa muungano linakosekana ambalo ni POLITICAL BALANCE based on individual countries CONSTITUTIONAL POWER kati ya nchi ambazo zinataka kuungana.

Huwezi kuanza kuongelea muungano gani unatakiwa uwepo wakati hata unaowauliza hujui kama wanataka huo muungano in the first place. kama ndivyo hivyo, unataka nchi gani ziungane wakati nchi inayotambulika kwa sasa kulingana na makabrasha ya constitutional law ni moja huku nchi nyingine ikiwa haipo under international law as sovereign state.

Kama kweli tunayatakia mema mataifa yaliyokuwa mawili (Tanganyika & Zanzibar ), this is the best available opportunity to settle this political huddle once and for all. Wananchi wanatakiwa kupewa SAY kuhusu mwerekeo wa mataifa yao kama wanapenda kuungana au hapana kwa njia ya KURA YA MAONI ( referendum ).

Serikali mbili zimeshindwa kupata dawa ya kisiasa kwa zaidi ya miaka 48 ili kuondoa utegemezi na malalamiko ya msingi kabisa kijamii, kisiasa na kiuchumi. Serikali tatu ni DOZE ya kisiasa kuua muungano slowly at higher political price. Serikali moja ni muungano imara lakini inatakiwa kusiwepo na UBINAFSI bali kuwepo na POLITICAL WILL kwa pande zote kitu ambacho kwa siasa za "Tanganyika" na Zanzibar bado sijaona.

Kwa mtaji huu, sioni kama uchaguzi mkuu 2015 utafanyika chini ya katiba mpya kwa sababu ugonjwa wa kisiasa unaoutafuna "muungano" utaendelea kuwepo huku ukichagizwa sana na marumbano yanayokuwa based on party political ideology bila kupata tiba mpaka hapo wananchi watashirikishwa moja kwa moja kupitia kura ya maoni.

Our political destiny is in our hand.
 
Kumbe hata tukijenga hoja nzito za kuukataa watakubali Muungano usiwepo ok wale mlioko kwenye mabaraza ya katiba mmemsikia Prof kinachotakiwa ni hoja zenye mashiko kuutaka,kuukataa,ama kuubolesha.
 
ccm hata wakitaka kuwepo kwa serikali 2 bado baraza la katiba litawapiga chini kwa sababu wananchi walio wengi ndio wamesema wanataka serikali tatu na siyo mabaraza ya katiba
 
Hapo anawananga chadema kiaina mana ndio vimbelembele
 
Kumbe hata tukijenga hoja nzito za kuukataa watakubali Muungano usiwepo ok wale mlioko kwenye mabaraza ya katiba mmemsikia Prof kinachotakiwa ni hoja zenye mashiko kuutaka,kuukataa,ama kuubolesha.
Mkuu, hadidu za rejea za tume ya Jaji Warioba zilikataa hata kuanza kufikiria kuuvunja huu muungano uliojaa matatizo.

Nadhani kama mabaraza ya upande wa Zanzibar yatasema hayataki mapendekezo ya serikali tatu na yale ya "Tanganyika" kwa wingi yakasema hayataki mapendekezo ya serikali tatu. Ninafikiri tume itakuwa na wakati mgumu kurekebisha ni muungano gani uwepo ambapo itabidi ikumbane na maswali yatakayotaka majibu kutoka kwa wananchi kuhusu nini wananchi wanachokitaka katika mstakabali wa mataifa yao.
 
Mabaraza ya katiba mapandikizi ya ccm tu. ccm endeleza fitna, koleza fitna,wimbo wa serikali tatu na wa mamlaka kamili utaendelea bila kikomo hadi kieleweke.
 
uliyoyasema katika hali ya kawaida ndiyo yangefanyika, wananvhi waulizwe ikiwa wanautaka muungano na wa aina gani kabla ya kuandika Katiba. Lakini tumeshatoka nhuko, kwa sababu muungano ulikuwepo na kwa sasa ni kutafuta tu njia ya kuuimarisha, kwa matajio kuwa walioungana bado tunataka kuendelea nao. Tatizo inaloliona hapa ni kuwa badala ya kushughulika na kuimarisha muungano tunapigania status quo. Hivi kwa nini chama kipiganie kubakiza muundo ambao kila siku unaonyesha una changamoto za muungano zisizotibika.

Nilitarajia sasa tungekuwa tunaongea kuwa na Serkali moja kagtika muunfdo ambao unatoa mamlaka ya ndani zaidi ya utawala kwa serkali za pande mbili za muungano.
 
Nimesikitika kuona watu wakitumia hasabu ya 1+1 = 2, halafu hawakujua kwamba 2 ni Tanganyika na Zanzibar.

Hamujui hesabu za seti. Union ina sehemu tatu, ina non union areas 2 na union area 1, yaani jula ni sehemu tatu

1 Zanzibar (Non inter sectional are)
2 Tanganyika (non inter sectional area)
3 Tanzania (inter-sectional area)

Tatizo nape na ccm wote hawajui hesabu ipi inatumila wapi?

Kawaulizeni watoto wa drasa la kwanza, watwaambia ni moja au tatu. Hakuna mbili.

paperclip.png
Attached Thumbnails
 
Naona bado watanganyika hamjajielewa ni kitu gani mnataka,tanganyika yenu?katiba yenu?au muungano wenu?huku zanzbr sie hatuna shida ya muungano wala katiba tunachohitaji ni mamlaka kamili ya jamhuri ya watu wa zanzbr full stop.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Muungano wa serikali mbili za sasa unatumia gharama kubwa kuliko serikali tatu zinazopendekezwa karika rasimu ya Katiba Mpya.
Kimesema hoja ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupinga shirikisho la serikali tatu kwa kigezo cha ukubwa wa gharama ni potofu kwa sababu mfumo unaopendekezwa utapunguza utitiri wa vyeo na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima.
Tanzania Daima imeona andishi la CHADEMA linalotarajiwa kuzinduliwa wakati wowote kuanzia sasa, ambalo ndiyo msimamo rasmi wa chama hicho kuhusu rasimu ya Katiba Mpya.
Miongoni mwa mambo mengi yanayochambuliwa kwa vielelezo ni hoja ya serikali, ambayo CCM imekuwa inahamasisha wanachama wake waikatae, na badala yake wapendekeze serikali mbili za sasa kwenye mabaraza ya katiba yanayoendelea.
CHADEMA imesema kuwa madai ya CCM kuwa serikali ni mzigo kwa taifa, hayana ukweli kwani serikali mbili za sasa zinatafuna mabilioni ya shilingi ambayo yataokolewa iwapo serikali zitakuwa tatu.
Katika kifungu cha ukubwa wa serikali, CHADEMA imesema kwa muundo wa sasa wa serikali mbili, kuna viongozi wakuu sita (6), wakati mfumo wa serikali tatu utakuwa na viongozi wasiozidi wanne (4). Imesema wabunge na wawakilishi 438, huku katika serikali tatu kutakuwa na wabunge wasiozidi 314.
Kwamba pamoja na hesabu hii, bado upo uwezekano wa idadi hii kupungua zaidi kwa kuwa mchakato wa kuandika Katiba ya Tanganyika na marekebisho/mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar kutokana na mabadiliko ya muundo wa Muungano unaweza kuja na mifumo tofauti ya uwakilishi au mgawanyo wa majimbo mapya ya uchaguzi.
“Bunge la Jamhuri ya Muungano la sasa lina idadi ya wabunge 357, ukitoa wabunge 189 wa majimbo ya uchaguzi ya Tanzania bara na 50 ya Zanzibar; 102 wa viti maalumu na 10 wa kuteuliwa na rais, watano wanaowakilisha Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mwanasheria Mkuu.
“Kwa upande wa Baraza la Wawakilishi kuna jumla ya wawakilishi 81-50 wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi, 10 wa kuteuliwa na Rais wa Zanzibar, 20 wa viti maalumu, na mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, kwa maana hiyo kwa muundo wa sasa wa Muungano, mabunge mawili tuliyonayo yana idadi ya wabunge 438.
“Idadi hiyo ni kubwa kuliko idadi ya wabunge wa mabunge matatu yatakayokuwepo chini ya muundo wa serikali tatu kwa wabunge 124,” imesema CHADEMA.
Ukweli huu unaiweka pabaya CCM ambao walidai kuwa serikali tatu inayopendekezwa na tume na kuungwa mkono na wapinzani itakomba fedha nyingi za Watanzania.
“Mapendekezo ambayo ndiyo msimamo wa chama tulishayawasilisha kwenye tume kuwa sisi tunapendekeza mfumo wa serikali mbili na siyo tatu wala moja,” alisema Nape alipokuwa akitoa taarifa ya uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyokutana usiku wa kuamkia jana kujadili suala hilo.
Kauli ya Nape inafanana na matamshi ambayo yamewahi kutolewa na baadhi ya wanasiasa wakongwe ambao ni makada wa CCM, wakiwamo mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na John Malecela, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na baadhi ya wabunge ambao mara kadhaa wamekaririwa wakipinga pendekezo la serikali tatu.
Hata hivyo, wabunge wa Zanzibar, akiwemo Mbunge wa Uzini, Mohamedi Seif Khatibu na Mjumbe wa Kamati ya Halmashauri Kuu ya CCM, Balozi Seif Idd, walisema watu watakaopinga serikali mbili wafukuzwe Chama Cha Mapinduzi.
Ifuatayo ni sehemu ya msimamo wa CHADEMA kuhusiana na uendeshaji wa serikali tatu:
Kwanza, hadi sasa hakuna mtu yeyote au taasisi yoyote iliyofanya uchambuzi wa uangalifu wa gharama za kuendeshea serikali, iwe moja, mbili au tatu katika nchi yetu. Kwa sababu hiyo, hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba kuendesha serikali tatu ni ghali zaidi kuliko kuendesha serikali mbili.
Pili, Kama suala la gharama za kuendeshea serikali ndio jambo muhimu zaidi katika kuamua muungo wa Muungano, wanaopinga shirikisho la serikali tatu wangeeleweka kama wangependekeza muundo wa serikali moja tu, badala ya serikali mbili za sasa wanazoziunga mkono, au hata tatu zinazopendekezwa na rasimu.
Tatu, kama mapendekezo ya rasimu juu ya mambo ya Muungano yakichukuliwa kuwa kigezo cha kupima ukubwa wa serikali na gharama za kuiendesha, basi gharama za serikali ya Muungano zinaweza kuwa ndogo sana.
Nne, kama mambo saba ya Muungano yanayopendekezwa na rasimu, hakutakuwa na zaidi ya wizara nne za Serikali ya Muungano. Hivyo kwa mfano kutakuwa na Wizara ya Katiba na Sheria itakayoshughulikia masuala ya katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano; Wizara ya Ulinzi itakayokuwa na majukumu ya ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano na Wizara ya Fedha itakayoshughulikia masuala ya sarafu, Benki Kuu na ushuru wa bidhaa na mapato yatokanayo na mambo ya Muungano, na Wizara ya Mambo ya Nje.
Masuala yaliyobaki yaani uraia na uhamiaji na usajili wa vyama vya siasa hayastahili kuwa na wizara zinazojitegemea, kwa hiyo yanaweza kuwekwa chini ya wizara zilizotajwa.
Aidha aya ya 93(2) ya rasimu inapendekeza ukubwa wa Baraza la Mawaziri wasiozidi kumi na tano. Hata hivyo aya ya 93(3) inaelekeza kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na wizara kwa kuzingatia mamlaka ya serikali kwa mujibu wa katiba hii, kwa namna nyingine ukubwa wa serikali lazima uzingatie mambo saba ya Muungano. Kwa sababu hiyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano haiwezi kuwa na mawaziri wengi kuliko mambo saba ya Muungano.
Kwa mtazamo huo huo, aya 93(3) na orodha ya mambo ya Muungano kama kipimo cha ukubwa wa Srikali ya Muungano haiwezekani katibu mkuu kiongozi na makatibu wakuu wanaopendekezwa katika aya za 98 na 99 za rasimu kuwa zaidi ya wanne.
Kwa kuzingatia idadi ya makatibu wakuu wenyewe, kamati maalumu ya makatibu wakuu inayoelekezwa katika aya ya 100 na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri inayotarajiwa katika aya ya 101 hazina maana wala umuhimu wowote kikatiba.
Kwa kuzingatia mapendekezo ya rasimu kuhusu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika aya ya 105, kwa idadi ya sasa ya mikoa ya Tanzania bara na wilaya za Zanzibar, Bunge la Jamhuri ya Muungano litakuwa na wabunge 75 kwa mapendekezo ya muundo wa serikali tatu, endapo Bunge la Zanzibar litakuwa na wabunge 50 wa majimbo ya sasa ya uchaguzi.
Kwa maana hiyo muundo wa Muungano wa serikali tatu utakuwa na mabunge matatu yenye jumla ya wabunge 314. Upo uwezekano wa idadi hii kupungua zaidi kwa kuwa mchakato wa kuandika katiba ya Tanganyika na marekebisho/mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar kutokana na mabadiliko ya muundo wa Muungano unaweza kuja na mifumo tofauti ya uwakilishi au mgawanyo wa majimbo mapya ya uchaguzi.
Kwa kulinganisha Bunge la Jamhuri ya Muungano la sasa lina idadi ya wabunge 357, ukitoa wabunge 189 wa majimbo ya uchaguzi ya Tanzania bara na 50 ya Zanzibar; 102 wa viti maalumu na 10 wa kuteuliwa na rais, watano wanaowakilisha Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mwanasheria Mkuu.
Kwa upande wa Baraza la Wawakilishi kuna jumla ya wawakilishi 81-50 wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi, 10 wa kuteuliwa na Rais wa Zanzibar, 20 wa viti maalumu, na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, kwa maana hiyo kwa muundo wa sasa wa Muungano, mabunge mawili tuliyonayo yana idadi ya wabunge 438. Idadi hiyo ni kubwa kuliko idadi ya wabunge wa mabunge matatu yatakayokuwepo chini ya muundo wa serikali tatu kwa wabunge 124!
Taasisi nyingine za Muungano zinazopendekezwa kama vile Tume ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali, na Tume ya Utumishi wa Umma haziwezi kuwa kubwa sana kwa kuzingatia ukubwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa rasimu.
Taasisi nyingine kama vile Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji, Tume ya Haki za Binadamu hazipo kwenye orodha ya mambo ya Muungano na uwepo wao kwenye rasimu unakinzana na matakwa ya aya za 59 na 60 za rasimu.
Kama majukumu ya taasisi hizo hayahusu mambo ya Muungano, tume haziwezi kugharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Hata hivyo baada ya kukubalika kwa pendekezo la kuyaingiza masulala hayo katika orodha ya mambo ya Muungano, bado gharama zinaweza kupunguzwa kwa kuweka mfumo wa utekelezaji wa taasisi husika kupitia makubaliano na washirika wa Muungano.
Majukumu ya utekelezaji wa mambo mengine ya Muungano kama uchaguzi na usajili wa vyama vya siasa yanaweza kutekelezwa na taasisi husika za washirka wa Muungano kwa makubaliano na masharti maalumu chini ya aya ya 59(3) ya rasimu. Hii nayo itapunguza gharama za kuendesha Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(Tanzania Daima, 2013)
 
uliyoyasema katika hali ya kawaida ndiyo yangefanyika, wananvhi waulizwe ikiwa wanautaka muungano na wa aina gani kabla ya kuandika Katiba. Lakini tumeshatoka nhuko, kwa sababu muungano ulikuwepo na kwa sasa ni kutafuta tu njia ya kuuimarisha, kwa matajio kuwa walioungana bado tunataka kuendelea nao. Tatizo inaloliona hapa ni kuwa badala ya kushughulika na kuimarisha muungano tunapigania status quo. Hivi kwa nini chama kipiganie kubakiza muundo ambao kila siku unaonyesha una changamoto za muungano zisizotibika.

Nilitarajia sasa tungekuwa tunaongea kuwa na Serkali moja kagtika muunfdo ambao unatoa mamlaka ya ndani zaidi ya utawala kwa serkali za pande mbili za muungano.
Mkuu Getstart muungano ulikuwepo lakini haukuwepo kwa sababu wananchi walitaka uwepo bali umakuwepo kwa sababu viongozi walitaka uwepo, ndiyo maana baada ya wananchi kufunguliwa midomo kisheria wameanza kuhoji sababu na madhumuni ya kuwepo kwake pasipo kupata majibu mbadala kutoka kwa wale wanaoushikiria na kuukambia muungano (viongozi).

Kuna uwezekano mkubwa ukawa mzizi wa tatizo la muungano siyo matatizo ya muungano uliopo au aina ya muungano bali ni tatizo ni kuwepo kwa muungano.

Sioni ubaya wa kurudi kwenye drawing board mpya kama iliyokuwepo pre-April 1964 ili tuanze upya kama mataifa mawili tofauti.
 
Last edited by a moderator:
Tanganyika ilikufaje?kuna haja ya kufufuliwa na maiti yake kuchunguzwa.
 
Mimi nadhani wasomi ndiyo watu wenye kupashwa kutuonyesha njia, na kama wameona serikali tatu zinafaa, sisi tusiosoma tuna ufahamu gani hadi tuwalaumu kwa hilo? au nasi tunalishwa mawazo na kundi jingine la watu tofauti na wasomi?
 
Mimi nadhani wasomi ndiyo watu wenye kupashwa kutuonyesha njia, na kama wameona serikali tatu zinafaa, sisi tusiosoma tuna ufahamu gani hadi tuwalaumu kwa hilo? au nasi tunalishwa mawazo na kundi jingine la watu tofauti na wasomi?
Mburula nao wana haki.
 
Muungano mungano kila jobs wanini? Kama kweli tunahita ndoa hii idumu jila mwandoa ajulikane ametoka kwa wazazi wake na niwakinani.ili kesho ndoa inapokuwa irreparable wanandoa akila mmoja zake. Serikali tatu may suluhisho. Tunataka Tanganyika yeti wimbo wetu,bendera yeti na uraia wetu. Ccm niwanafiki wamekwisha walisha sumu wajumbe wa mabaraza ya hats ili wakatai mapendekezi ya tume
 
Back
Top Bottom