Profesa Bengesi: Serikali haikuchelewesha Vibali vya Kuagiza Sukari, Wazalishaji wenyewe walichelewa kuvichukua

Profesa Bengesi: Serikali haikuchelewesha Vibali vya Kuagiza Sukari, Wazalishaji wenyewe walichelewa kuvichukua

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
BODI ya Sukari Tanzania imekanusha taarifa za kuchelewa kutoa vibali vya uagizaji wa sukari kwa kampuni za wazalishaji nchini, badala yake baadhi ya kampuni hizo zilichelewa zenyewe kuchukua vibali hivyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania, Profesa Kenneth Bengesi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, baada ya kuwepo taarifa za baadhi ya wadau wa sukari nchini kudai Serikali haikuwapa vibali kwa wakati.

“Napenda kuuhabarisha umma wa watanzania kuwa, si kweli kwamba wazalishaji wa sukari nchini walicheleweshwa kupewa vibali, isipokuwa wao ndiyo walichelewa kuchukua vibali,” Alisema Profesa Bengesi.

Aidha Profesa Bengesi alisema wazalishaji walipewa vibali kabla ya kampuni za wafanyabiashara wanazoziita za “vocha” zilizopewa vibali baada ya kuona mwenendo wa uingizaji wa sukari wa kampuni za wazalishaji kuwa sio mzuri.

Profesa Bengesi alisisitiza kuwa kitendo cha wadau kusema Bodi ilitoa vibali vya sukari kwa wafanyabiashara kwanza kabla ya kuwapa wazalishaji, ni upotoshaji wa makusudi ili kuzua taharuki kwa Watanzania.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Sukari inaonyesha kampuni za wazalishaji zilipewa vibali vyake mwanzoni mwa mwezi Januari, wakati kampuni za wafanyabiashara zilipewa vibali hivyo mwishoni mwa mwezi January na mwezi Aprili.

Wazalishaji kutoagiza sukari 2022/2023 kulipandisha bei ya bidhaa

Kitendo cha kampuni za wazalishaji kutoagiza sukari nje ya nchi katika msimu wa 2022/2023, kulisababisha bei ya sukari kupanda na kuongeza hali mbaya ya upatikanaji wa sukari nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Profesa Kenneth Bengesi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya baadhi ya wadau wa sukari kuzungumzia Sakata hilo licha ya kukosa taarifa za kutosha.

“Kampuni nne zilipewa vibali lakini ni kampuni moja tu ya Kilombero kati ya nne iliingiza sukari tani 2,380 licha ya wazalishaji kupewa vibali vya kuagiza sukari kwa msimu huo. Kitendo cha wazalishaji kutoingiza kiasi chote cha sukari kilichoidhinishwa 2022/23 kilisababisha upungufu na kupanda bei hadi kufikia shilingi 4,000 kwa kilo moja mwezi Juni, 2023,” Alisema Profesa Bengesi.

Katika hatua nyingine, Profesa Bengesi alisema kitendo cha kushindwa kwa wazalishaji kuingiza sukari katika msimu wa 2022/2023 kuliwapotezea sifa ya kisheria ya kupewa vibali kwa msimu wa 2023/2024, lakini bado serikali iliendelea kuwapa vibali vya kuendelea na shughuli ya uingizaji wa sukari nchini Tanzania.
1720209098769.jpeg

1720209110956.jpeg



View: https://www.youtube.com/live/Hi4-bR9IpJo?si=KeB_vUNNDnL8jgoL
 
Kumbe Mpina alikuwa sahihi kuhusu ile kampuni ya Itel
 
Back
Top Bottom