Profesa Bengesi: Wazalishaji ambao hawakuagiza Sukari 2022/2023 ndio waliochangia bei kupanda

Profesa Bengesi: Wazalishaji ambao hawakuagiza Sukari 2022/2023 ndio waliochangia bei kupanda

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kitendo cha kampuni za wazalishaji kutoagiza sukari nje ya nchi katika msimu wa 2022/2023, kulisababisha bei ya sukari kupanda na kuongeza hali mbaya ya upatikanaji wa sukari nchini.

Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Profesa Kenneth Bengesi ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya baadhi ya wadau wa sukari kuzungumzia Sakata hilo na kudai walicheleweshewa Vibali na wengine kudai hawakupewa

“Kampuni nne zilipewa vibali lakini ni kampuni moja tu ya Kilombero kati ya nne iliingiza sukari tani 2,380 licha ya wazalishaji kupewa vibali vya kuagiza sukari kwa msimu huo. Kitendo cha wazalishaji kutoingiza kiasi chote cha sukari kilichoidhinishwa 2022/23 kilisababisha upungufu na kupanda bei hadi kufikia shilingi 4,000 kwa kilo moja mwezi Juni, 2023,” Alisema Profesa Bengesi.

Katika hatua nyingine, Profesa Bengesi alisema kitendo cha kushindwa kwa wazalishaji kuingiza sukari katika msimu wa 2022/2023 kuliwapotezea sifa ya kisheria ya kupewa vibali kwa msimu wa 2023/2024, lakini bado serikali iliendelea kuwapa vibali vya kuendelea na shughuli ya uingizaji wa sukari nchini Tanzania.
 
Back
Top Bottom