Profesa chuo cha Oxford asifu uchumi Tanzania

Profesa chuo cha Oxford asifu uchumi Tanzania

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
552
1582205041089.png


TANZANIA imetajwa kuwa miongoni mwa nchi tatu zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambazo hazipo katika hatari kubwa ya kudodora kiuchumi kutokana na kuwa na kiwango cha chini cha madeni. Hali hiyo imebainishwa jijini Dar es Salaam juzi na Mchumi kutoka Chuo cha Oxford cha Uingereza, Profesa Christopher Adam.

Alisema hayo wakati akitoa mada katika kongamano la wazi, lililofanyika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na kuwahusisha watu mbalimbali wakiwemo wahadhiri wa chuo hicho. Katika mada yake hiyo, mchumi huo alisema katika utafiti huo, uliofanyika mwaka jana, Tanzania, Senegal na Uganda ndizo nchi pekee zilizokuwa katika msimamo salama wa uwiano wa madeni katika nchi nyingi, zilizopo katika ukanda huo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka jana.

Katika kongamano hilo ambalo mada kuu yake ilikuwa “Je! Ni kwa kiasi gani nchi za Afrika zinakabiliwa na tatizo jipya la madeni” ikilenga kupata mtazamo kwa wataalamu mbalimbali, mchumi huyo alisema zipo baadhi ya nchi ndani ya bara hilo, ambazo zimekuwa na madeni makubwa, kiasi cha kushindwa kuyamudu. Hivi karibuni, Serikali ya Tanzania imekuwa ikisisitiza kuwa deni la kitaifa ni himilivu, na kwamba mikopo zaidi bado inahitajika ili kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha, katika kulitekeleza hilo hivi karibuni, pia serikali ilisaini makubaliano ya mkopo wa Sh trilioni 3.3 na Benki ya Standard Chartered Tanzania ili kufadhili ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaoendelea kufanywa.

Katika hafla ya utiaji saini wa mkopo huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisisitiza kwamba deni la taifa bado ni himilivu, na serikali itakopa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ili kukuza uchumi.

Awali akielezea sababu nafasi ya Tanzania kukopa kutokana na hali hiyo, Profesa Adam alisema deni la Tanzania linaiwezesha kuendelea kukopa, na ni muhimu kwa serikali kufanya hivyo kutokana na kuwa na uchumi mdogo. “Kwa uchumi mdogo kama Tanzania ni muhimu kukopa ili kuharakisha maendeleo zaidi ya kiuchumi na hivyo kuendana na kasi ya uchumi wa dunia kwa sasa,” alisisitiza Profesa Adam.

Ili kufikia malengo hayo, alisema ni muhimu kuwekeza katika miundombinu mbalimbali muhimu kama barabara na reli, sambamba na kuwekeza katika mitaji, kama kweli nchi inataka kupata faida hasa kutokana na kuwa rasilimali za asili zinazogunduliwa kama vile gesi. Aidha, Profesa Adam alitaja nchi zilizopo katika ukanda huo, ambazo zipo hatari kubwa kutokana na madeni kuwa makubwa ni Gambia, Msumbiji, Sudani Kusini, Sudan na Zimbabwe. Nchi zingine zilizopo katika hatari ya kati ni Benin, Kongo, Kenya, Libya, Madagasca na Nigeria.
 
Ni sawa...lakini tuendelee pia kuvutia mitaji binafsi itayovutia ukuaji wa uchumi bila kulipa riba.
 
Ni vyema huyo msomi akakaa kitako na zitto maana nae ana takwimu mchicha! Zake!
 
Back
Top Bottom