Profesa Issa Shivji kigoda cha Mwalim Nyerere Watilia shaka utaratibu wa Katiba Mpya

Profesa Issa Shivji kigoda cha Mwalim Nyerere Watilia shaka utaratibu wa Katiba Mpya

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
Profesa-Issa-Shivji-akichangia-mada-kama-mjumbe-wa-Ziff-2012-537x8001.jpg

Profesa Shivji

Mimi nilidhani kwamba kabla ya kuanza kwa mchakato wa kuunda Katiba Mpya kungekuwa na dira ya mpango wa maendeleo ili kujua tunataka Katiba ya aina gani,”alisema Profesa Shivji.



TAASISI za kiraia zimesema mchakato wa kuunda Katiba Mpya bila kuwa na dira ya mpango wa kitaifa unaweza kusababisha kupata Katiba itakayohusisha mawazo ya watu wachache.


Hayo yalibainishwa Dar es Salaam jana katika ufunguzi wa tamasha la 10 linalohusisha asasi mbalimbali za kiraia nchini.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji alisema kabla ya kuanza kwa mchakato wa kuunda Katiba Mpya alitegemea kungekuwa na dira ya mpango wa maendeleo katika Katiba hiyo.


Alisema bila kuwa na mpango huo kuna uwezekano wa kutengeneza Katiba itakayohusisha mitazamo ya watu wachache.


“Mimi nilidhani kwamba kabla ya kuanza kwa mchakato wa kuunda Katiba Mpya kungekuwa na dira ya mpango wa maendeleo ili kujua tunataka Katiba ya aina gani,”alisema Profesa Shivji.

Profesa Shivji alibainisha kwamba vitu ambavyo ni muhimu kuwa katika Katiba Mpya ni pamoja na haki,usawa,amani,udugu, ujamaa na uhuru binafsi.

Katika hatua nyingine Profesa Shivji alisema suala la demokrasia katika Katiba Mpya ni vyema likazingatiwa kwa kupewa kipaumbele.

Akifafanua kuhusu demokrasia alisema kuna aina mbili za demokrasia ambazo ni demokrasia shirikishi na wakilishi.
Alisema ni vyema misingi ya demokrasia wakilishi ikazingatiwa kwani hapo ndipo inatoa uwezo wa kujitawala wenyewe.
 
Mbona utaratibu mzima kuhusu jinsi ya kuunda katiba mpya ulipitishwa bungeni Dodoma, kwanini mawazo hayo hakuyapeleka wakati wabunge wetu wanawakilisha hoja za kunda hiyo katiba tangia mchakato wamwanzo? Kweli siasa ni mchezo mchafu! Lakini bada hajachelewa akapeleke maoni yake kwa wahusika.
 
Mbona utaratibu mzima kuhusu jinsi ya kuunda katiba mpya ulipitishwa bungeni Dodoma, kwanini mawazo hayo hakuyapeleka wakati wabunge wetu wanawakilisha hoja za kuunda hiyo katiba tangia mchakato wamwanzo kabisa? Kweli siasa ni mchezo mchafu! Lakini bado hajachelewa, akapeleke maoni yake kwa wanaohusika.
 
Mchakato unaoendelea ni eneo lingine ambapo mamilioni ya walipa kodi yanatafunwa bila tija yoyote. Kila mtu anatoa maoni yake, sawa ila mambo yafuatayo hayatajibika;

1. Nani anaratibu maoni yanayotolewa?

2. Watakapoyaweka kapuni na kuweka mawazo yao, nani atahoji kwa nini maoni hayakufanyiwa kazi?

3. Maoni mengine ni vichekesho tu, kuna utaratibu gani wa kuona muda hauchezewi kwa kuendekeza maigizo badala ya kupata maoni?
 
Usidhani Katiba mpya ni yakuja kumkomboa mwananchi, ndiyo inakuja kuzuia maandamano, uhuru wa vyombo vya habari, kuwabana matajiri wanaochangia upinzani, nk ni katiba ya kuuza uhuru wa wanyonge wa kumiliki ardhi.
 
Maoni ya katiba mpya ni sawa kwa kila Mtz kutoa dukuduku aliyonayo moyoni, lakini kuna wataalam waliosomea nyanja hizi, hasa wanasheria wakishirikiana na wanauchumi na wana sayansi kwa kuwashirikisha wabunge, pia na baadhi ya wasomi tulionao, tunaweza kupata katiba nzuri sana naya kisasa kabisa, kuliko kuwaachia awa ndugu zetu kuendelea na porojo za majukwaani.
 
Back
Top Bottom