Profesa Kabudi akutana na Balozi wa Vatican nchini Askofu Mkuu Marek Solczynski. Akubaliana kushirikiana na nchi hiyo katika kudumisha amani

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
EwiBf8RWYAYfJAr.jpg

Waziri wa mambo ya nje Prof Kabudi leo amekutana na balozi wa Vatican nchini na kupokea salamu kutoka kwa Papa.

Viongozi hao wawili wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo amani katika maeneo ya Congo na Msumbiji.

Pia wamejadili kuhusu Covid na kukubaliana waiambie dunia swala hilo lisiwe la kisiasa au kibiashara bali lishughulikiwe kwa pamoja pote duniani kwa kushirikiana.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
===
Tanzania na Vatican zimeahidi kuendelea kuhimiza amani na utulivu katika masuala yenye changamoto mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa amani na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Baba Mtakatifu katika kuhimiza amani, utulivu na usalama duniani.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) wakati alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski leo jijini Dar es Salaam.

Prof. kabudi amesema kuwa Tanzania na Vatican kwa kutambua umuhimu wa amani, zimeahidi kuendelea kushirikiana katika mikutano ya Umoja wa Mataifa kuhimiza amani, utulivu na mshikamano katika masuala mbalimbali yenye changamoto kwa binadamu duniani.

“Tumeongelea umuhimu wa kulinda amani, utulivu na usalama duniani kote hasa katika maeneo yanayokumbwa na matatizo ya vita…….. katika hilo pia tuliongela suala la amani na usalama katika ukanda wa nchi za maziwa makuu, Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika tukijua kuwa kuna maeneo yanayohitaji amani ikiwemo eneo la kaskazini mwa Masumbiji, na mashariki ya Demokrasia ya Kongo,” Amesema Prof. Kabudi.
Prof. Kabudi ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni na hata sasa dunia inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji mshikamano wa mataifa yote duniani ili kuweza kuyakabili hii ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu amani, utulivu, majanga, na magonjwa ya mlipuko kama vile Covid 19, na yale yanayohusu umasikini na hali yamaisha ya watu kubaguliwa na kuonewa.
“Mfano katika mapambano dhidi ya Uviko 19, Vatican na Baba Mtakatifu wanayo nafasi kubwa ya kutoa mchango wao katika eneo hilo katika kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya Covid 19 hayageuzwi kuwa katika masuala ya kibiashara na kisiasa na badala yake mapambano hayo yazingatie utu, undugu na imani, Ameongeza Prof. Kabudi

Kwa upande wake Balozi wa Vatican hapa Nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski amesema kuwa Vatican itaendelea kuimarisha mahusiano yake ya kidiplomasia na Tanzania kwa masuala yenye maslahi ya haki, utu, amani na utulivu.

“Maongezi yangu na Mhe. Waziri yalikuwa mazuri kwani tuliongelea masuala mbalimbali yenye maslahi kwa binadamu yakiwemo masuala ya kukuza diplomasia yetu pamoja na masuala ya amani na usalama duniani,” Amesema Askofu Mkuu Solczynski.

Baba Mtakatifu Papa Francisko alimteua, Askofu Mkuu Marek Solczyński kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Tanzania mwezi Aprili, 2017. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Solczyński alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Georgia, Armenia na Azerbaijan.

Katika tukio jingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Tate Olenasha amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria hapa nchini Mhe. Ahmed Djellal ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu kuimarisha diplomasia baina ya Tanzania na Algeria.

source: Tanzania foreign Affairs blog
 
15 March 2021

Tanzania na Vatican zimeahidi kuendelea kuhimiza amani na utulivu katika masuala yenye changamoto mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa amani na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Baba Mtakatifu katika kuhimiza amani, utulivu na usalama duniani.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) wakati alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski leo jijini Dar es Salaam.

2-36-scaled.jpg
Picha : Prof. Palamagamba Kabudi na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski

Prof. kabudi amesema kuwa Tanzania na Vatican kwa kutambua umuhimu wa amani, zimeahidi kuendelea kushirikiana katika mikutano ya Umoja wa Mataifa kuhimiza amani, utulivu na mshikamano katika masuala mbalimbali yenye changamoto kwa binadamu duniani.

“Tumeongelea umuhimu wa kulinda amani, utulivu na usalama duniani kote hasa katika maeneo yanayokumbwa na matatizo ya vita…….. katika hilo pia tuliongela suala la amani na usalama katika ukanda wa nchi za maziwa makuu, Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika tukijua kuwa kuna maeneo yanayohitaji amani ikiwemo eneo la kaskazini mwa Masumbiji, na mashariki ya Demokrasia ya Kongo,” Amesema Prof. Kabudi

Prof. Kabudi ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni na hata sasa dunia inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji mshikamano wa mataifa yote duniani ili kuweza kuyakabili hii ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu amani, utulivu, majanga, na magonjwa ya mlipuko kama vile Covid 19, na yale yanayohusu umasikini na hali yamaisha ya watu kubaguliwa na kuonewa.
“Mfano katika mapambano dhidi ya Uviko 19, Vatican na Baba Mtakatifu wanayo nafasi kubwa ya kutoa mchango wao katika eneo hilo katika kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya Covid 19 hayageuzwi kuwa katika masuala ya kibiashara na kisiasa na badala yake mapambano hayo yazingatie utu, undugu na imani, Ameongeza Prof. Kabudi

Kwa upande wake Balozi wa Vatican hapa Nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski amesema kuwa Vatican itaendelea kuimarisha mahusiano yake ya kidiplomasia na Tanzania kwa masuala yenye maslahi ya haki, utu, amani na utulivu.

“Maongezi yangu na Mhe. Waziri yalikuwa mazuri kwani tuliongelea masuala mbalimbali yenye maslahi kwa binadamu yakiwemo masuala ya kukuza diplomasia yetu pamoja na masuala ya amani na usalama duniani,” Amesema Askofu Mkuu Solczynski.

Baba Mtakatifu Papa Francisko alimteua, Askofu Mkuu Marek Solczyński kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Tanzania mwezi Aprili, 2017. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Solczyński alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Georgia, Armenia na Azerbaijan.

Katika tukio jingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Tate Olenasha amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria hapa nchini Mhe. Ahmed Djellal ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu kuimarisha diplomasia baina ya Tanzania na Algeria.
source: Tanzania foreign Affairs blog
 
Kabudi ni msanii mmoja hivi; uzuri na hawa mabalozi wengi washajua!! He doesn't mean what he's saying...usanii mtupu!!
 
Ameenda kutubu matusi ya Meko kwa mapadre na Masista.....Nafikiri siku ile alivyowananga laana ilimpiga..Ameenda kumuombea radhi

Ila wamejiabisha...wanakula matapishi yao
Umebugi men waliopika data za vifo vya makasisi na watawa unadhani wako salama kwa ugeni huo.Hahahahahahaha
 
Padre Dr Kitima anaweza kukipata alichokipata mtangulizi wake Padre Dr Wilbroad Slaa kwenye nafasi hiyo ya Kanisa Katoliki. Wote wawili wana PhD ya Canon Laws. Wote wawili wameonesha kuitumia nafasi hiyo na elimu hiyo kisiasa badala ya kiroho.
 
Mbona hawajasema kakutana na beberu tunaona tittle ya balozi?
 
Back
Top Bottom